Kumbukizi ya miaka 2 bila Hayati Magufuli inazidi kuchangamsha 2025

Kama unamjua aliyetekeleza yale na kama mnashirikiana na CCM kufuta legacy yake. Kuna kigugumizi gani asitajwe aliyetekeleza?

Au bado marehemu anawafuata huko kuwatisha kuwa ole wenu mumtaje aliyemfanyia unyama Lisu?
 
CCCM Kwa kushindwa kumuenzi Magu Kwa MAZURI yake na kuachia makundi haya kukua.

Hawana budi kutuletea bila kupenda kiongozi aina ya Magu hapo 2025.
 
CCCM Kwa kushindwa kumuenzi Magu Kwa MAZURI yake na kuachia makundi haya kujua.

Hawana budi kutuletea bila kuipenda kiongozi aina ya Magu hapo 2025.
Kiukweli si sahihi kumleta kiongozi aina ya Magu kwa sababu tumeshatambua kuwa CCM huwa haiheshimu mfumo.

Tunachotaka ni katiba mpya ambayo kila raia (iwe namba moja mpaka sifuri) atawajibika kwayo.

Tunahitaji taasisi zenye nguvu za kikatiba

Tunahitaji maslahi ya nchi yaanishwe na kulindwa kikatiba

Tunahitaji Katiba inayomtambua Mtanzania kama sehemu ya heshima ya nchi.

Hayo ya kutuletea mtu ni hadaa na ramli wanayoitumia CCM kuendelea kuimega nchi
 
Ndo tuipambanie Kwa JASHO,

Haiji soft Kwa maridhiano kama tunavyoaminishwa.

Bei za Bidhaa zinazidi kupanda, mafuta hayashuki Bei, mfumuko wa Bei haudhibitiwi.

Mambo haya ndo yanatupa wasiwasi juu ya AGENDA za maridhiano.

Why maridhiano hayabadili chochote kuhusu Hali ngumu ya wananchi?

Magu anakumbukwa na hapakuwa na Katiba mpya sababu Alijitahidi kupunguza mzigo wa maskini, unafuu kwenye mfumuko wa Bei ulikuwepo.
 
Awamu ya 4 nakumbuka mauwaji ya Mwandishi Mwangosi hadharani lakini pia siwezi sahau mateso makali kupita kiasi aliyoyapotia Doctor Ulimboka alikuwa kiongozi wa chama cha Madaktari aliyeokotwa msitu wa Mabwe pande.Yote hayo watu wanajifanya kuyasahau
 
Hapa umegonga nyundo pahali pake.Watapita kimya kimya
 
Kivuli cha marehemu kinawafuata nyuma [emoji16][emoji16][emoji16]
 
@Tsh njoo uone hizi enzi za 2006-2010 zilikuwa ni mjadala mkali sana.Hapa umegusiwa kidogo tu
 
@Tsh unakumbuka swali ulilouliza jana na majibu niliyokupatia?
 
Hapa umegonga nyundo pahali pake.Watapita kimya kimya
Lazima wapite kimya kimya, unaona ht nliekua nampa somo kapotea mafichoni...wanampigia JPM kelele kwakua either ni viongozi wa kisiasa wana ID fake, vyeti fake and the like wenye personal agenda...nenda Youtube channel ya JF uone maoni tofauti na ya humu ndani...humu ndani unakuta mtu ana ID 10 ana log na ku log off kujijibu alichochangia...ndo maana unaona watu ni wale wale na hoja zao za akwelina na saa8 utadhani mwangosi yy hakufariki kwa kipigo cha police.
 
Na huu ndiyo ujinga wao,wanadhani wapo smart kuliko wengine lakini kwa sisi wenyeji wa hili jukwaa,tulishaona pattern yao ya uandishi tu na unajua kabisa hapa ni multiple ID's zinafanya kazi.Ahsante sana Mkuu kuwapa somo hawa vijana wanaojifanya much know kwenye kila kitu.

Nimecheka sana kwenye jibu la zitto junior baada ya kuitwa na Msanii kwenye moja ya comment zako.Dogo katoa majibu mepesi sana kwenye maswali magumu.I wish kina Mzee Mwanakijiji Nyani Ngabu na wengine warejee tena waungane na nyie kurejesha heshima ya mijadala ya kutumia nguvu ya hoja.
 

Mna maoni Gani hapa? Channel ya jamii forums hii.

Then story iliyotrend wiki hii ni kuhusu Simba.... Bob junior je Ina views ngapi?

Je tuseme Bob Junior ni maarufu kuliko JPM? Mind you video ya bob Junior ni zaidi ya 40 minutes ila watu 150k wamekomaa nayo sembuse video za dakika Moja Moja hapo JF viewers hawafiki hata 1000 kwa screenshot nliloweka hapo.

Mnachekesha sana
Cc Carlos The Jackal Nyamizi
 
Kama unamjua aliyetekeleza yale na kama mnashirikiana na CCM kufuta legacy yake. Kuna kigugumizi gani asitajwe aliyetekeleza?

Au bado marehemu anawafuata huko kuwatisha kuwa ole wenu mumtaje aliyemfanyia unyama Lisu?
Mbona Lissu ameshamtaja ni JPM tokea akiwa hai!! Kama asingekua yeye, Polisi au TISS kwanini waligomea kufanya uchunguzi Hadi Leo wakidai mpaka Lissu arudi Tanzania mara sijui dereva aje!!?
 
Mbona Lissu ameshamtaja ni JPM tokea akiwa hai!! Kama asingekua yeye, Polisi au TISS kwanini waligomea kufanya uchunguzi Hadi Leo wakidai mpaka Lissu arudi Tanzania mara sijui dereva aje!!?
Haya JPM keshatangulia.

Je ndiye aliyefyatua risasi?

Kwa nini tusijue washirika wake kwenye hii murser attempt? Au alituma robots kufanya hayo mashambulizi?
 
Mkuu unaona mbali sana.

Hapa wanachokifanya ni kutuonesha wana uwezo wa kujadili na kujibu huja. Kumbe ni watupu na wameshafilisika kichwani.
 
Mkuu
Unajitahidi lakini bora ungetafakari kwanza kabla ya kujibu hoja za GT wa JF.

JF siyo mamlaka ya serikali na sidhani kama walikosea kuweka hiyo ishu ya Bob. Sisi tunazungumzia CCM na Serikali ambao wana online media channels na wanao wakuu wa itifaki.

Kujifanya kujitenga na JPM ni picha ya nini kinachogubika tamati yake.
 
Hapa umegonga nyundo pahali pake.Watapita kimya kimya
Two wrongs don't make a right.... Huwezi justify JPM sio dikteta simply sababu ameua sawa tu na Mkapa!! That's madness!!

Kipindi Cha JPM ndio zimeletwa sheria kali za kubana uhuru wa maoni.

1. Sheria ya huduma ya habari.

2. Regulations za TCRA kwenye leseni za online Tv. Ilitakiwa upeleke ratiba ya vipindi Ina advance, ulipie million 1 kupata leseni n.k yote haya ku discourage watu kusikiliza bloggers wanaomkosoa JPM.

3. Sheria ya takwimu Ili mtu binafsi asichapishe utafiti huru au takwimu mpaka apate "vibali" yote hizi kupunguza tafiti mfano za Twaweza.

4. Sheria ya vyama vya siasa iliyompa mamlaka Msajili kuingilia internal procedure za chama.

5. Kufungia mikutano ya kisiasa ambayo ni haki kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.

6. Kwa mara ya kwanza 90% ya wagombea wa upinzani walienguliwa kwenye uchaguzi wa TAMISEMI.

7. Kwa mara ya kwanza ripoti ya bunge ilikabidhiwa kwa Rais yaani walikua hawawezi kupitisha maazimio juu ya wizi wa Tanzanite. More so alitoa order kwa Spika kuwatimua wapinzani Ili aje awashughulikie huku nje.

8. Hili ndio kubwa zaidi... Alituondoa kwenye open governance initiative Ili serikali isiwajibike kwa bunge au wananchi. Yaani Kulikua na usiri mkubwa sana wa mambo.

9. Alianzisha parallel bar Ili kuwaengua mawakili wa serikali TLS yote haya kuepuka "uanaharakati" wa TLS. yaani hofu ya kukosolewa akaona aunde parallel body!!

10. Alipunguza bajeti ya CAG kwa nusu Ili isiweze kuwa na capacity ya kukagua serikali. Ukisoma performance audit ya CAG wanasema licha ya bajeti ya NAO kupangwa na kamati ya bunge ila serikali ilitoa nusu pekee ya pesa yote Ili tu kuvuruga ukaguzi.

11. JPM alizuia utekelezaji wa sheria ya TEITI iliyotaka mikataba yote ipelekwe bungeni. Ieleweke ilipitishwa 2016 yeye akiwa Rais ila alipinga mikataba kuwekwa wazi kwa kuhofia wapinzan kupata pointi bungeni.

Mifano ni mingi ila udikteta wa JPM unapimwa kwa mengi tu aliyowazidi JK na Mkapa na sio vifo pekee.

Cc Carlos The Jackal Nyamizi Msanii

Naomba mjibu hizi hoja one by one na mtueleze why asiwe dikteta.
 
Haya JPM keshatangulia.

Je ndiye aliyefyatua risasi?

Kwa nini tusijue washirika wake kwenye hii murser attempt? Au alituma robots kufanya hayo mashambulizi?
Mbona Lissu kaeleza Kila kitu kuwa alikua anafuatiliwa na gari ya Nissan Patrol ila Polisi walipuuza in fact hata JF humu mlimtukana kuwa anatafuta kiki.

Later JPM alikuja ku order kwamba tunapokua vitani Kuna wasaliti sijui wanaropoka jeshi mnajua jinsi ya kudeal na hilo!!

Few days later akashambuliwa na risasi na tokea hapo Lissu Kila akisema uchunguzi ufanyike jeshi linagoma why?? Sasa unataka Lissu atoe evidence wapi wakati ushahidi wa kimazingira upo.

Kesi za jinai burden of proof haipo kwa aliyepigwa risasi kutoa ushahidi sijui kwanini mnaforce "sisi" ndio tutoe ushahidi ilihali wenye mamlaka maCCM ndio wameukalia mpaka Leo.

Insanity
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…