Kumbukizi ya miaka 59 toka Said Mwamwindi amuue RC Dkt. Kleruu siku kama ya leo mwaka 1971

Namimi toka mwanzo ndio nimeuliza, ni kwanini hiyo hoja haikujibiwa, yaani kwanini upore mashamba waliyovuja jasho wengine wakati mapori bado yamejaa, kwanini msiwape hao wengine mapori ili na wao wakahenyeke kung’oa visiki? Why?!

Ujamaa unaendeshwa na sera za uporaji(looting) kutoka kwa walio nacho kwenda kwa wasio nacho kwa dhana ya kuleta usawa kwenye umiliki wa mali katika jamii(egalitarian distribution of wealth) ambapo kwa nchi kama Tanzania ilikuwa ni sawa na kuwafanya watu wote kuwa maskini.

Kwa sababu za chuki za kijima, sera za uporaji zinachukua kipaumbele juu ya malengo ya muda mrefu ambayo hata hivyo hayana tija kwenye maendeleo ya binadamu zaidi ya kuridhisha nafsi(ego) za waasisi na watekelezaji vipofu wa hii dhana.

“From each according to his ability, to each according to his needs”.

Absurd!
 
Hebu basi tueleweshe zaidi angalau tukuelewe. Maana naona unatetea kitu, unatuona tuko gizani lakini lakini kutupa mwanga hata kidogo hutaki.

Uchumi unatakiwa uwe wazi na wenye ushindani. Watu wahangaike kutafuta Mali kwa njia halali.

Serikali unakuja tu kuweka mipaka na kusimamia. Vitu kama umeme, maji, bara bara, hospitali hazitakiwi kuwa binafsi. Au kwa ajili ya faida.

Huo ndio uchumi ulikuepo mwanzo na ambao baba etu. Aliuvurugu.
 
Juhudi ni Ile aliyokuwa nayo mkulima said Mwamindi.
Wakati wengine wakilala yeye alienda kufyeka mapori na kuyalima.
Sawa
Wakati wa vita baridi hakukuwa na any proven economic system that worked out somewhere.

Dunia ilikuwa kwenye TRIAL and ERROR.

Hakuna mtu yeyote aliyekuwa anajua mfumo upi ni bora na mfumo upi ni mbaya.

Na ndio maana kila pembe ya dunia walikuwa wanachagua mfumo wao kulingana na wanavyoona wao.

Sasa tatizo la vijana wa sasa hivi huwa wanazungumzia hii mifumo utafikiri Nyerere aliifanya haya maamuzi mwaka 2,000.

Ndio maana mimi nawauliza.

Je, Ujamaa ulikuwa umeshindwa wapi na sisi tukakopi licha ya kuonekana umeshindwa?

Mifumo mingine ni ipi iliyokuwa imeonesha mafanikio makubwa na sisi tukaamua kuupuza?
 
Baba hebu rudia vitabu vyako vya historia vizuri. Maana unavyoongea nikama vile uchumi wa sasa ulianza baada ya WW2

Bwana Smith (baba wa uchumi wa kibepari ) alitoa kitabu cake change kwanza mwaka gani?

Karl max ( baba wa ujamaa) ulitoa majarida yake ya kwanza mwaka gani? ?

Hapa hatumshutumi na kumkashifu Nyerere. Tonachojaribu kusema ni kwamba na yeye pia alikua na madudu yake na alikosea pia. Na yeye pia alikiri kwa bahati nzuri.

Hatuwezi kusonga mbele bila kujifunza makosa yetu ya nyuma. Hii mambo ya kificha ficha mambo haisaidii kitu.
 
Mimi ni wapi nimesema Nyerere hakukosea?

Nyerere alikosea kwa mengi tu na hata yeye mwenyewe alikiri, mpaka kuandika kitabu cha TUJISAHIHISHE.

Hapa ninachotofautiana na nyie ni kutupia LAWAMA zote kwa mfumo wa KIJAMAA as if huo mfumo ni mbovu kwa 100%.
 
Mi naona hii historia iwe inatolewa wakati hawa MaRC na MaDC wanapopewa semina ya uongozi. Wana la kunifunza hapa.

Kwamba ukiwa kiongozi, fanya kazi haswa ili kuleta maendeleo lakini huku ukimumbuka kwamba unaongoza wananchi wenye mawazo, akili na mtazamo tofauti ambao unaweza kuwa bora kuliko wako. Haikua na maana sana kuchukua mashamba ya wananchi waliojiandalia wenyewe kisha ugawie wale waliokuwa wakicheka wenzao wakati wanatokwa jasho kuandaa mashamba.

Pia kiongozi awe na akiba ya maneno. C kila raia anaogopa kukupasua ukimletea lomoni.

NAWASALIMU KWA JINA LA MNYALU MWAMWINDI
 
Itoshe kusema MNYALU katuachia kumbukumbu mujaraaaab
 
Yule jamaa aliepewa kazi ya kynyonga alikua jasiri kweli
Kumbe ukimaliza kunyonga unapelekwa mahakama ya kimchongo, unasomewa kesi ya kimchongo, unahumumiwa kuua kimchongo, unaendelea kunyonga.

Wanahukumiwa kwa kunyonga ili nini ss wakati ni kazi wanayopewa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sheria bhana. Learned brothers tusaidieni
 
Hii Ni kukuondolea hatia ya kuua, yaani kukutoa ktk hatia ya kiroho na kimwili hivyo hatakuwa na sononeko la nafsi!!
Tofauti na yule anayeua tu damu ya yule mtu lazima mlilie tu
 
Baada ya hili tukio hadi kunyongwa kwa huyu bwana, Isimani sasa ni kama ilipata laana tokea hapo, kwa sababu ninapozungumza isimani ni moja ya sehemu ambazo huwa zinakumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula kila mwaka
Kibilia damu ikimwagika mahali,ujue inadai kisasi na ni laana!
Kwahiyo inawezekana,mpaka watu wa eneo hilo waombe toba!
 
Kibilia damu ikimwagika mahali,ujue inadai kisasi na ni laana!
Kwahiyo inawezekana,mpaka watu wa eneo hilo waombe toba!
Sana..

Imagine kule isimani unaweza kulima eka 1 ya mahindi ukavuna debe 2 tu.

Sehemu ambayo tunaambiwa ilikuwa inalisha hadi nchi za jirani.?,
 
Sana..

Imagine kule isimani unaweza kulima eka 1 ya mahindi ukavuna debe 2 tu.

Sehemu ambayo tunaambiwa ilikuwa inalisha hadi nchi za jirani.?,
Yaani ni balaa!
Wazazi wangu walianzia huko maisha!
Walikuwa wana shamba wanalima, mpk,Rais Julias Nyerere alikuwa anaenda kuwatembelea miaka ya themanini na......,imagine!
Yaani mama ananisimulia mpk nashangaa,isimani iliyokuwa ndani ya 'the big five' ! Wao wenyewe wanashangaa hawaamini wanachokiona!

Yaani wewe ndo umenifungua akili aisee,inawezekana kabisa ikawa kweli!
Damu ya mtu ni kitu kingine!
 
Ardhi ni mali ya serikali, lakini si mnafidiwa?
 
Siasa ya nyerere ya ujamaa ilipelekea wasomi wazuri kukimbilia ughaibun hii nchi ingekua mbali Sana kiuchumi. Ndio Mana alinusurika kupinduliwa mara nyingi.afu wajinga flan wanataka awe mtakatifu
 
Kiongozi mtoa uzi kama hutojali tumegee ya huyo mhindi aliyekuwa anapindua magari alipwr BIMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…