Kumbukizi ya miaka 59 toka Said Mwamwindi amuue RC Dkt. Kleruu siku kama ya leo mwaka 1971

Kumbukizi ya miaka 59 toka Said Mwamwindi amuue RC Dkt. Kleruu siku kama ya leo mwaka 1971

Hili lipo na linatokana na Kleruu mkristu mlutheri mchaga wa Mwika Marangu aliwezaje kuipa kisogo siku ya Krisimasi huku familia yake ikiandaa mapochopocho ya sikukuu! Mkewe na watoto hawakujua baba ameenda wapi, hakuaga na hakutaka ulinzi japokuwa miaka hiyo hawakuwa na ulinzi wa maana.
Nirudi kwa mzee Kisoky aliyetoka kwenye udc, huyu na alifanya alichofanya Mwamwindi, alimpiga risasi na kumuua mkewe dogodogo ukiacha mke wa kwanza, hakuchukuliwa hatua yoyote.
Mhindi wa bima, huyu alimuua mkewe akamuweka ndani ya gari na kuiporomosha kwenye milima ya Likumburu*(sic), jina nimelihifadhi.
Tungeipata pia hii simulizi ya Kisoky ingekuwa poa sana
 
Akimuelezea tena Kawawa kwa uvumilivu huo Nyerere kwny Kitabu chake cha Siasa yetu na Hatma ya Tanzania anasema 'Hutokea mara chache sana Mungu kuumba watu wa roho kama ya Kawawa' maneno haya ukiyatafakari utajua Kawawa alibebeshwa vipi mizigo ya lawama
Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania
 
Kumbukizi nzuri ila umemkata ndugu,
mjengwamajjid hapa yuko huko ndio kwanza yuko kati ya investigation report ya huyohuyo Mwamwindi na kakaa sana huko.
Alikua anaandaa kitabu chake cha history ya huyo jamaa na Dr kleruu.
Mi nimekaa huko
Hanidanganyi mtu kitu.
Sasa tungempa nafasi japo mjengwa auze kitabu chake.
Hajatoa story yote tumeijua.
Sasa si tunaharibu ugali wake?
Hii story ungeleta zamani hakuna ambae angeuliza.
Lakini now,?huyu mwandishi majjid yuko chimbo ndio anafukunyua mambo we ushaweka hapa.
Tuwe tunafikiriana.
Umeandika kwa hisia mtu anaweza akadhani kuwa wewe ni Maggid Mjengwa mwenyewe, au japo mtu wake wa karibu sana
 
Mwandishi kazi nzuri sana, inaonekana watu walikuwa wachapa kazi na walianza kuendelea miaka mingi sana ila siasa za kijamaa zikaturudisha nyuma sana, somo zuri kwa watu wasio na adabu, waonezi na ubabe wa kifala kama Makonda na Sabaya
 
Kwa sababu nachukia uvivu na wanaopromote uvivu, hasa kampuni za betting na hizo sera za kijamaa, yaani wengine wasafishe mapori we uje ulime tu, na mapori bado yamejaa, kwanini wasiende kusafisha?
Kampunj za kubeti unazionea tu wala hazipromote uvivu ila zinapromote free market economy coz huwez kubet kama Huna hela na ili upate hela ni lazima uitafute.

Wale wadau wa kubet lazima tukupinge kwa nguvu kwa hoja hiyo.
 
Asante kwa historia nzuri kama hii! Kwa mazingira yale kibinadamu Muuaji hakuwa na namna!
 
Kampunj za kubeti unazionea tu wala hazipromote uvivu ila zinapromote free market economy coz huwez kubet kama Huna hela na ili upate hela ni lazima uitafute.

Wale wadau wa kubet lazima tukupinge kwa nguvu kwa hoja hiyo.
Betting ni kazi? Kama ni kazi, inazalisha bidhaa / huduma ipi?

Maana kazi ni lazima izalishe kimoja wapo (bidhaa au huduma).
 
Hebu basi tueleweshe zaidi angalau tukuelewe. Maana naona unatetea kitu, unatuona tuko gizani lakini lakini kutupa mwanga hata kidogo hutaki.

Uchumi unatakiwa uwe wazi na wenye ushindani. Watu wahangaike kutafuta Mali kwa njia halali.

Serikali unakuja tu kuweka mipaka na kusimamia. Vitu kama umeme, maji, bara bara, hospitali hazitakiwi kuwa binafsi. Au kwa ajili ya faida.

Huo ndio uchumi ulikuepo mwanzo na ambao baba etu. Aliuvurugu.
Unajichanganya tuu naona, na akili kama zako ndio maana hatuna umeme wala maji na Hospitals zetu ni za ovyo kabisa, Acha watu wafanye kazi wamiliki hayo makampuni ya umeme na mahospitali, serikali ikusanye Kodi na kusimamia haki na Sheria zilizopo ili biashara na uzalishaji viende vizuri
 
Kwa msiojua, Rashid Mfaume Kawawa akiwa waziri mkuu wakati huo alikwenda Kyela Mbeya, baada ya kufika huko akaamuru kufunga maduka binafsi ili wananchi wafungue maduka ya ushirika! Vijana wa Kyela wa wakati huo hawakukubali wakakusanya mawe na kumpopoa Rashid, Nyerere akamwambia Rashid sikukutuma ufunge maduka ulitakiwa ufungue maduka ya ushirika halafu hayo ya binafsi yangejifunga yenyewe.
Ilibidi aje Mzee Nyerere mwenyewe, lakini akastukia mchezo akamtuma Rashid Kawawa. Wazee wa Kinyakyusa wakajipanga kumsubiri Nyerere wakashangaa kwenye Land Rover anashuka kawawa.

Wakakasirika mno wakaanza kusema "Kapimba" kumaanisha mtu mfupi amekuja kufanya nini hapa wakati sisi tunamtaka Nyerere mwenyewe. Kawawa kafanyiwa fujo, na baadaye hapo uwanjani zikaja NYUKI zikaanza kumfukuza, ambapo alikimbia kweli mzee wa watu hadi kwenye Land Rover lake huyo akaondoka.

Nyerere akaona haitoshi, hawa Wanyakyusa jehuri waliokataa UJAMAA ni kuwakomesha. Akamteua rafiki yake MARWA, kijana wa Kikurya Machachari awe RC Mbeya.

Marwa akaanza mbwembwe kama za Kreluu, kuwatishia Wanyakyusa kwamba yeye kaaga kwao na atawanyoosha. Wazee wa Kinyakyusa wakasema huyu kijana anatutukana sisi, tutaona.

Marwa katika jitihada zake za kulazimisha Ujamaa kwa Wanyakyusa alijikuta anatangulia peponi mapema. Siku moja RC yuko kwenye sherehe chakula kipepikwa, baada ya hapo tumbo likaanza kuvimba.

RC anakunywa maji wapi, tumbo linavimba tu na kiu haikati. Kijana wa watu wa kikurya akafia njiani, na ndiyo jitihada za kulazimisha UJAMAA kwa Wanyakyusa zikafia hapo.

Mzee Nyerere alifura mno kwa hasira na kutuma polisi kuwafanyia vurugu Wanyakyusa, ambapo watu walisulubishwa kwelikweli kwasababu wamemuua RC jehuri.​
 
Ujamaa unaendeshwa na sera za uporaji(looting) kutoka kwa walio nacho kwenda kwa wasio nacho kwa dhana ya kuleta usawa kwenye umiliki wa mali katika jamii(egalitarian distribution of wealth) ambapo kwa nchi kama Tanzania ilikuwa ni sawa na kuwafanya watu wote kuwa maskini.

Kwa sababu za chuki za kijima, sera za uporaji zinachukua kipaumbele juu ya malengo ya muda mrefu ambayo hata hivyo hayana tija kwenye maendeleo ya binadamu zaidi ya kuridhisha nafsi(ego) za waasisi na watekelezaji vipofu wa hii dhana.

“From each according to his ability, to each according to his needs”.

Absurd!
e166efdc8ae654466de987716921dc11 (1).jpg
 
Kumbukizi nzuri ila umemkata ndugu,
mjengwamajjid hapa yuko huko ndio kwanza yuko kati ya investigation report ya huyohuyo Mwamwindi na kakaa sana huko.
Alikua anaandaa kitabu chake cha history ya huyo jamaa na Dr kleruu.
Mi nimekaa huko
Hanidanganyi mtu kitu.
Sasa tungempa nafasi japo mjengwa auze kitabu chake.
Hajatoa story yote tumeijua.
Sasa si tunaharibu ugali wake?
Hii story ungeleta zamani hakuna ambae angeuliza.
Lakini now,?huyu mwandishi majjid yuko chimbo ndio anafukunyua mambo we ushaweka hapa.
Tuwe tunafikiriana.
Ye aendelee tu kuandaa kitabu, kila siku wasomaji wapya na wenye kutaka kujua kilichotokea kwa kleruu na mwamwindi wanaibuka,

Mfano me mwenyewe bado kuna vitu naamini hatujavijua au kujulishwa vizuri juu ya tukio hilo hivyo kama kutakuja kitabu kipya nitakinunua tu kwani kuna mengi sn ya kujifunza.
 
Back
Top Bottom