Hili lipo na linatokana na Kleruu mkristu mlutheri mchaga wa Mwika Marangu aliwezaje kuipa kisogo siku ya Krisimasi huku familia yake ikiandaa mapochopocho ya sikukuu! Mkewe na watoto hawakujua baba ameenda wapi, hakuaga na hakutaka ulinzi japokuwa miaka hiyo hawakuwa na ulinzi wa maana.
Nirudi kwa mzee Kisoky aliyetoka kwenye udc, huyu na alifanya alichofanya Mwamwindi, alimpiga risasi na kumuua mkewe dogodogo ukiacha mke wa kwanza, hakuchukuliwa hatua yoyote.
Mhindi wa bima, huyu alimuua mkewe akamuweka ndani ya gari na kuiporomosha kwenye milima ya Likumburu*(sic), jina nimelihifadhi.