Kumbukumbu: Leo ni miaka 10 tangu Simba amfunge Yanga 5-0

Siku hiyo nilikuwa Kinondoni B. Kuna jamaa yangu alikuja kutoka Dom kwenye Shughuli zake za kibiashara sasa akafikia Gheto langu hapohapo Kinondoni. Mida ya saa 7 jamaa akaniambia twende Taifa tukacheki game.

Muda huohuo kulikuwa na game ya Man U (Sikumbuki ilikuwa vs nani) nikasema siwezi kwenda Taifa niache Match ya Man U. Kwakuwa mie ni Simba na Man U. Na hata hivyo pressure za watani wajadi huwa sizipendi kabisa. Jamaa yangu yeye alikuwa Simba pia.

Baada ya game jamaa ananiambia nilikuambia twende ukakataa unaona sasa.

Nilijilaumu sana.
 
Asante kwa kumbukumbu murua kabsa hii

Itadumu milele na milele ameeen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…