Kumbukumbu ya Hayati Magufuli isiwe sikukuu ya kitaifa, ifanywe na CCM

Hayupo mtu wakufutilia mbali... unajidanganya tu wewe fisadi mkubwa!
 
Pascal Mayalla nasikitika unahubiri tuwe wafuasi wa unafiki. Mimi sio muumini wa imani hiyo sababu kujipendekeza sio hulka yangu.

Ulijitahidi kumpamba kwa kila rangi alipokuwa hai ili upate wasaa wa kuteuliwa, lakini akaendelea kukuchinjia baharini.

Weee mwenzangu unasifu na kuabudu ili upate uteuzi serikalini, nafsini mwako kamwe huwezi kuwa mfuasi wa kweli na haki kwani nafsi yako inaongozwa na tamaa.

Magufuli ana mema yake, lakini hayafuniki ubaya wake. Magufuli aendelee kuenziwa na chama chake, hakuacha alama yoyote kwenye siasa za kiushindani.

Aliwazima na kuwafunga mdomo hata watu wa ndani ya chama chake. Je ana nini cha kutufundisha kuhusu demokrasia?
 
Kwani wewe una nini cha kuwafundisha watz kumzidi Magufuli anayekubalika na zaidi ya 90% ya Watanzania?
 
Hata huko CCM atakumbukwa na wachache. Wengi wanamwona kama mtu aliyeleta udikteta wa ajabu ndani ya chama.

Ni huyu Magufuli ndiye ambaye mwaka 2020 alikata robo tatu ya majina yote yaliyopendekezwa na wajumbe ili wawe wagombea wa ubunge kupitia CCM. Akawapachika watu ambao aliwataka yeye, mara nyingi aliwapenda watu wanafiki au wenye upeo na akili kidogo ambao hawawezi kuhoji chochote anachokifanya, hata kiwe cha hovyo kiasi gani.

Kule Nyanda za Juu Kusini ambako alisababisha mahindi na mbao vikose, watu wakaunguza mitaji yao, hata kufikia gunia la mahindi la kilo 100 kuuzwa kwa sh 20,000, alikuwa na ushujaa gani?

Ushujaa ule wa kuteka watu, kuua na kuwapoteza wasiotaka kumsifu? Wengi wanaomwona alikuwa shujaa ni wale ambao au ni wanafiki, waliiba na kufaidika naye au wana upeo na akili iliyo chini ya wastani.
 

Mkuu pole sana kwa msongo wa mawazo! Walio hai wasiteswe na waliokufa
 
mkuu umeandika facts tupu hatuitaj kufat hisia za watu kwny inshu za kitaifa tunatakiwa kutumia akil kwny inshu za kitaifa
 
Wakifanya huu ujinga Rais Mwingine wa upinzani aje azifutilie mbali huu upuuzi..

Kuna siku ya mashujaa ilishaga puuzwa na maccm na Wala sio public holiday ila ujinga kama huu ndio wanataka uwe public holiday?

Mkuu pole sana tuzidi kuwaombea walio hai wasiteswe na wafu
 
Hebu tueleze 1.5 trilion zilienda wapi , yule aliweza kudanganya wajinga wajinga tu kama wewe

Iwekwe siku ya kuwakumbuka viongozi wa hovyo, waliowahi kutikisa utengamano wa Taifa.

Siku hiyo iwe siku ya kuweka msisitizo wa nchi kuwa na mifumo mizuri ambayo haitaruhusu viongozi wabaya kama Magufuli kupenya kwenye nafasi za uongozi.
 
Mbona Iddi Amin bado mnamsema vibaya?
Au kuna ubaguzi wa marehemu?
 
Ukweli kuhusu wizi, udikteta, uonevu, chuki, mauaji na upendeleo wa awamu ya tano na Magufuli mwenyewe umewekwa wazi kwa kiwango kidogo tu kwa vile wengi wa washirika wake bado wako madarakani.
Iko siku yote yatawekwa wazi na ndio hapo sio kufikiria siku ya kitaifa tuu kutaisha bali hata vyote mlivyo vipa majina yake mtafuta na kurudisha majina asili kama ilivyo Ujerumani hakuna kitu kinaitwa Hitler ingawa alisimamia miradi mingi, Sadam kule Iraq au Mobutu hapo DRC nk

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…