Kumbukumbu ya Hayati Magufuli isiwe sikukuu ya kitaifa, ifanywe na CCM

Ni kweli alimuua mama yako. Nasikia mama yako alikuwa anauza madawa ya kulevya maeneo ya mbezi beach au vipi?
Sasa muuza madawa ya kupevya ndo Hana haki ya kuishi. Nani alimpa madaraka jpm ya kutoa uhai wa mtu kisa anauza madawa ya kupevya. Ndo maana ghadhabu yamungu ilimshukia Kama mwewe na akamfuta kwenye uso wa dunia maana ingekuwa vilio na kusaga meno
 
Jembe! lilikulimia nini labda akumbukwe kwa ukatiri wake
20221019_090652.jpg

Miaka michache nyuma hapa palikuwa kama tandahimba.
 
Mimi sio CCM ila nitafurahi tukiwa na Magufuli national day.
Lile jembe nalikubali mpaka kesho.
Naunga mkono ikizingatiwa pia jinsi alivyoliongoza Taifa vema kipindi cha corona! Kuna mataifa yalidondoka kabisa kiuchumi hadsi leo kutokana na walivyoshughu;lika na corona! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe!
 
Mimi sio CCM ila nitafurahi tukiwa na Magufuli national day.
Lile jembe nalikubali mpaka kesho.
Kijana kumbuka hii ni JF na inatunza kumbukumbu. Uchawa wako haufichiki kirahisi namna hiyo. Hizo akili mwisho wake mlango wa kutokea ofisi ya CCM. Wadanganye watotot wenzio.
 
Hili povu ni kwa sabàbu mimi namkubali Magufuli?
 
Mtapinga sana lakini tayari tumeshajenga Makumbusho yake hapo Chato. Hatuwasikilizi wenye vyeti fake na mafisadi tunajua aliwanyoosha sana hamuwezi kumkubali kwa kuwa aliwazuia ulaji wenu wa kiwizi.
Hapo kwenye vyeti weka nukta tuongeze idadi⛷️⛷️
 
CCM IWEKE KUMBUKUMBU YA JPM NA SIO TAIFA!!!

Kuna wito unatolewa na wabunge na makada wa ccm kuwa Rais mwendazake John P. Magufuli atengewe sikukuu ya kitaifa kuenzi mchango wake kwa taifa,hoja ikiwa kwamba amefanya mambo mengi sana mazuri kiasi cha kumuwekea siku maalum ya kumkumbuka ambayo itakua sikukuu ya kitaifa Kama ilivyo siku ya Karume ama JK Nyerere,hili linapaswa kufanywa zaidi na ccm kuliko taifa zima, nitaeleza!!!

Ukiuangalia uongozi wa Magufuli unamuona mtu aliyetafuta kujijenga yeye zaidi kiutawala na kujenga zaidi chama chake (ccm) kuliko kujenga taifa, taifa sio tu nchi,taifa ni watu,nchi na vyote vilivyomo na labda unaweza kusema angeenda Mbali zaidi kujenga nchi kuliko taifa, ni falsafa pana!

Mtu anayejijenga yeye kiutawala huhakikisha anarundika madaraka mengi mikononi mwake ama kikatiba ama kwa kuvunja Katiba,huzima sauti zote mbadala ambazo zitampinga kufanikisha hilo', huzima bunge, hudhibiti mahakama,huzuia uhuru wa vyombo vya habari na kufunga midomo ya vyama pinzani na wapinzani, miaka mitano ya utawala wa JPM haya yote yakifanyika kwa ufanisi mkubwa.

JPM alijikita katika kuhakikisha ccm inakua haina mpinzani,aliapa kwa kauli zake jukwaani,alitekeleza kwa vitendo, chaguzi za serikali ya mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 ulidhihirisha kuwa hakua akitania alipojiapiza kuwa ifikapo 2020 Tanzania itakua haina chama cha upinzani, na kufuta siasa za vyama vingi Tanzania haikua agenda ya kitaifa,ilikua agenda yake binafsi, ikiinufaisha zaidi ccm kuliko kujenga utangamano wa kitaifa

JPM alikua mtetezi na mpigania ccm zaidi kuliko kuwa mjenzi wa taifa,hivyo ccm ndio waweke siku maalum ya kumkumbuka Kama wanavoikumbuka February 5 ya kila mwaka siku chama hicho kilipoundwa!!!

Kama taifa ni nchi,Watu na vyote vilivyomo basi Watu hao ni pamoja na wapinzani, Freeman Mbowe,Zitto Kabwe na wengineo.

Watu ni pamoja na wananchi wa kimara mbezi ambao nyumba zao zilibomolewa bila fidia,mamia wakiachwa bila makazi,Watu ni pamoja na wakulima wa korosho kule kusini ambao soko la zao lao tegemezi liliharibiwa baada ya JPM kuamuru korosho yote ichukuliwe na serikali,watu hao ni wakazi wa Kagera waliopata janga la tetemeko la ardhi wakaachwa bila msaada hata walipochangiwa fedha,fedha hizo zilichukuliwa na serikali ya JPM.

Vipi kuhusu wafanyabiashara ambao fedha zao zilichukuliwa kwa Nguvu benki hata waziri mteule wa fedha Mwigulu Nchemba amelazimika kushawishi Watu kurejesha imani ya kuhifadhi fedha benki,mifano ni mingi,Watu wote hawa sidhani Kama kwao JPM ni shujaa,kuulazimisha ushujaa wa JPM kwao ni kuwaonea na kuutusi ufahamu wao!

Hakuna wakati taifa limepata mpasuko na sintofaham ya kutojua kesho itakuaje Kama wakati wa JPM, hakuna wakati Tanzania imesemwa vibaya kwa ukiukwaji wa haki za kiraia katika vyombo vya kimataifa kushinda watangulizi wote kuliko wakati wa JPM.

Wale wanaotaka tuweke kumbukumbu ya kudumu juu yake nje ya kumbukumbu za jumla za kihistoria,nashauri wafanye hivyo kupitia chama tawala CCM ,chama chake alichokipigania sana,Au waanzishe klabu za kumbukumbu mitandaoni na kwingineko,wamkumbuke huko kwa furaha zao,lakini wengine tuachwe kuwakumbuka Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,waasisi wa taifa letu!!!
Yule mzee alikuwa na roho mbaya Sana kwakweli,. Nikikumbuka fedha za wale wahanga wa kagera,waliovunjiwa nyumba kimara, na mengine mengi,hafai hata kukumbukwa kabisa
 
Naunga mkono hoja. Tena aenziwe na wanaccm wa Chato pekee siyo wanaccm wa nchi nzima hadi Mtama na Bumbuli.

Heil Magufuli!
imhotep
 
Mtapinga sana lakini tayari tumeshajenga Makumbusho yake hapo Chato. Hatuwasikilizi wenye vyeti fake na mafisadi tunajua aliwanyoosha sana hamuwezi kumkubali kwa kuwa aliwazuia ulaji wenu wa kiwizi.
Sasa Yuko wapi? Mungu kamfykelea mbali. Sasa hivi ni Mkuu wa mashetani.

Mpaka leo wanaishi vipi au ni wewe unawalisha? Tunamtaka Been na Azron wauwaji wakubwa.
 
Shujaa wa Afrika, baba wa Uchumi wa Tanzania. 🙌
Eiav3EwXkAAVrju.jpeg
 
Yule mzee alikuwa na roho mbaya Sana kwakweli,. Nikikumbuka fedha za wale wahanga wa kagera,waliovunjiwa nyumba kimara, na mengine mengi,hafai hata kukumbukwa kabisa
Ndugu usinikumbushe ya mbezi. Yaani niliona Kama kipindi chake kilikuwa na mkosi. Watu wengi Sana walirudi nyuma na wengi walikufa kwa kukosa matumaoni.

Wale watoto wazazi wao waliovunjowa nyumba jinsi walovyohangaika ile ni sumu kwa ccm.

Aliomba kitengo Cha kusimamia hakujua anamkejeli mungu. Alisema watanzania watamkumbuka ni wangapi watamkumbuka Leo zaidi ya kudai watu wao waliotekwa na waliopotea.

Hakuwa kiongozi alikuwa muuwaji.
 
Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume , tujifunze kudumisha Uafrika wetu na Utanzania wetu wa heshima kwa marehemu wetu!, marehemu hasemwi vibaya!. Mwacheni JPM apumzike kwa amani, na kwa taarifa yenu, kuna vitu wengi hamjui kumhusu JPM ,, saa hizi yuko na Baba yake kule kwa Baba yake!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Maadam alikuwa ni kiongozi wa taifa, ikianuliwa na yeye aenziwe kwa kutengewa siku yake, then itakuwa ni siku ya kitaifa, ila tufanye kwa wote, tuanze na Mwinyi Day, Mkapa Day, Kikwete Day, tuje Magufuli Day na muda wa Samia ukiisha pia tunakuwa na Samia Day na maadhimisho ya siku hizo sio lazima ziwe ni public holiday!.
P

Mwisho wa siku Taifa litakapokuja kuwa na viongozi kama 180 au 360 tunakuwa na siku 360 za sikukuu, hamna kufanya kazi kila siku ni sikukuu!! Huu ni upumbavu!!!

Heshima ya sikukuu pekee iende kwa Nyerere na Karume kama waasisi wa Taifa la Tanzania inatosha.

Wengine tutaendelea kuwakumbuka kwa mazuri yao!!

Ina maana Magufuli alifanya kazi kubwa kuliko watangulizi wake Mkapa na Kikwete!! ?
 
Mimi sio CCM ila nitafurahi tukiwa na Magufuli national day.
Lile jembe nalikubali mpaka kesho.
Sio Magufuli pekee aliyetoa mchango kwa taifa hili. Huo ni ubaguzi, marais wengine pia wana mchango mkubwa tu. Nyerere anapewa kwa sababu ni mwanzilishi na ni rais wa kwanza.
Wapo watu wengine ambao si marais walitoa mchango mkubwa tu hatuwezi na ma so and so days mengi...
Labda angekuwa amekufa kwa sababu ya kulitetea taifa sawa. Apewe mabarabara na mataasisi yanatosha
 
Ndugu usinikumbushe ya mbezi. Yaani niliona Kama kipindi chake kilikuwa na mkosi. Watu wengi Sana walirudi nyuma na wengi walikufa kwa kukosa matumaoni.

Wale watoto wazazi wao waliovunjowa nyumba jinsi walovyohangaika ile ni sumu kwa ccm.

Aliomba kitengo Cha kusimamia hakujua anamkejeli mungu. Alisema watanzania watamkumbuka ni wangapi watamkumbuka Leo zaidi ya kudai watu wao waliotekwa na waliopotea.

Hakuwa kiongozi alikuwa muuwaji.
Hakuwa binadamu wa kawaida yule, satan
 
Back
Top Bottom