Kumbukumbu ya Hayati Magufuli isiwe sikukuu ya kitaifa, ifanywe na CCM

Kumbukumbu ya Hayati Magufuli isiwe sikukuu ya kitaifa, ifanywe na CCM

Afadhali kuwa mjinga kuliko kuwa mpumbavu. Mjinga anaweza kufundishwa akaondoa ujinga lakini mpumbavu kama wewe hufundishiki ni sifa kama ufupi na urefu. Wewe tayari Mungu alishakupa upumbafu hivyo utakufa nao hauwezi kubadirika. Hongera kwa kuwa MPUMBAFU.
Umezidiwa hoja unarusha matusi[emoji2][emoji2][emoji2]
 
CCM IWEKE KUMBUKUMBU YA JPM NA SIO TAIFA!!!

Kuna wito unatolewa na wabunge na makada wa ccm kuwa Rais mwendazake John P. Magufuli atengewe sikukuu ya kitaifa kuenzi mchango wake kwa taifa,hoja ikiwa kwamba amefanya mambo mengi sana mazuri kiasi cha kumuwekea siku maalum ya kumkumbuka ambayo itakua sikukuu ya kitaifa Kama ilivyo siku ya Karume ama JK Nyerere,hili linapaswa kufanywa zaidi na ccm kuliko taifa zima, nitaeleza!!!

Ukiuangalia uongozi wa Magufuli unamuona mtu aliyetafuta kujijenga yeye zaidi kiutawala na kujenga zaidi chama chake (ccm) kuliko kujenga taifa, taifa sio tu nchi,taifa ni watu,nchi na vyote vilivyomo na labda unaweza kusema angeenda Mbali zaidi kujenga nchi kuliko taifa, ni falsafa pana!

Mtu anayejijenga yeye kiutawala huhakikisha anarundika madaraka mengi mikononi mwake ama kikatiba ama kwa kuvunja Katiba,huzima sauti zote mbadala ambazo zitampinga kufanikisha hilo', huzima bunge, hudhibiti mahakama,huzuia uhuru wa vyombo vya habari na kufunga midomo ya vyama pinzani na wapinzani, miaka mitano ya utawala wa JPM haya yote yakifanyika kwa ufanisi mkubwa.

JPM alijikita katika kuhakikisha ccm inakua haina mpinzani,aliapa kwa kauli zake jukwaani,alitekeleza kwa vitendo, chaguzi za serikali ya mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 ulidhihirisha kuwa hakua akitania alipojiapiza kuwa ifikapo 2020 Tanzania itakua haina chama cha upinzani, na kufuta siasa za vyama vingi Tanzania haikua agenda ya kitaifa,ilikua agenda yake binafsi, ikiinufaisha zaidi ccm kuliko kujenga utangamano wa kitaifa

JPM alikua mtetezi na mpigania ccm zaidi kuliko kuwa mjenzi wa taifa,hivyo ccm ndio waweke siku maalum ya kumkumbuka Kama wanavoikumbuka February 5 ya kila mwaka siku chama hicho kilipoundwa!!!

Kama taifa ni nchi,Watu na vyote vilivyomo basi Watu hao ni pamoja na wapinzani, Freeman Mbowe,Zitto Kabwe na wengineo.

Watu ni pamoja na wananchi wa kimara mbezi ambao nyumba zao zilibomolewa bila fidia,mamia wakiachwa bila makazi,Watu ni pamoja na wakulima wa korosho kule kusini ambao soko la zao lao tegemezi liliharibiwa baada ya JPM kuamuru korosho yote ichukuliwe na serikali,watu hao ni wakazi wa Kagera waliopata janga la tetemeko la ardhi wakaachwa bila msaada hata walipochangiwa fedha,fedha hizo zilichukuliwa na serikali ya JPM.

Vipi kuhusu wafanyabiashara ambao fedha zao zilichukuliwa kwa Nguvu benki hata waziri mteule wa fedha Mwigulu Nchemba amelazimika kushawishi Watu kurejesha imani ya kuhifadhi fedha benki,mifano ni mingi,Watu wote hawa sidhani Kama kwao JPM ni shujaa,kuulazimisha ushujaa wa JPM kwao ni kuwaonea na kuutusi ufahamu wao!

Hakuna wakati taifa limepata mpasuko na sintofaham ya kutojua kesho itakuaje Kama wakati wa JPM, hakuna wakati Tanzania imesemwa vibaya kwa ukiukwaji wa haki za kiraia katika vyombo vya kimataifa kushinda watangulizi wote kuliko wakati wa JPM.

Wale wanaotaka tuweke kumbukumbu ya kudumu juu yake nje ya kumbukumbu za jumla za kihistoria,nashauri wafanye hivyo kupitia chama tawala CCM ,chama chake alichokipigania sana,Au waanzishe klabu za kumbukumbu mitandaoni na kwingineko,wamkumbuke huko kwa furaha zao,lakini wengine tuachwe kuwakumbuka Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,waasisi wa taifa letu!!!

Kwani JPM alikuwa wa CCM pekee!?
 
Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume , tujifunze kudumisha Uafrika wetu na Utanzania wetu wa heshima kwa marehemu wetu!, marehemu hasemwi vibaya!. Mwacheni JPM apumzike kwa amani, na kwa taarifa yenu, kuna vitu wengi hamjui kumhusu JPM ,, saa hizi yuko na Baba yake kule kwa Baba yake!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Maadam alikuwa ni kiongozi wa taifa, ikianuliwa na yeye aenziwe kwa kutengewa siku yake, then itakuwa ni siku ya kitaifa, ila tufanye kwa wote, tuanze na Mwinyi Day, Mkapa Day, Kikwete Day, tuje Magufuli Day na muda wa Samia ukiisha pia tunakuwa na Samia Day na maadhimisho ya siku hizo sio lazima ziwe ni public holiday!.
P
Kikwete atengewe siku ya kukumbukwa kwa lipi?
 
Mimi sio CCM ila nitafurahi tukiwa na Magufuli national day.
Lile jembe nalikubali mpaka kesho.

Umeona ukisema ww ni CCM huu utetezi wako utakosa mashiko? Yule dhalimu akumbukwe na ccm maana ndio waliona faida yake.
 
Sasa Kama Karume anaenziwa pamoja na kuwa Dikteta,kwanini Magufuli asienziwe kitaifa?
Lamba ndimu za buku kwa Mangi hapo gengeni ili upunguze uchungu dhidi Marehemu Magufuli,nitalipa
 
Tatizo letu sisi watanzania au wengi wetu tunataka kubembelezwa na kupetiwa petiwa kama wanawake na watoto.

Hoja za mleta mada ni makundi madogo sana yalioathirika na uongozi wa Magufuli kati ya makundi mengi na uma kwa ujumla ambao faida yake inaonekana sio jana wala leo tu bali hata kesho na kesho kutwa.

Kama kiongozi wa china wakati ule mao Zedong angekua anabembeleza watu kama ambavyo wengi wetu tunavyo penda na kutamani, china isingekuwa hapa ilipo sasa.

Haja ya kuwepo kwa siku ya taifa ya Magufuli sio ya muhimu wala ya upekee ili kuoa wakati maana tunapoteza muda kwa mambo mengi yasiyo na faida, lakini kama taifa , nchi , na watu wote kwa ujumla wetu tunapaswa kujifunza katika mema ili ktmutenda mema zaidi na katika mabaya ili kutorudia mabaya.

Kama binadamu, Magufuli alikua na mapungufu yake mengi ya kiuongozi na pia alikua na mazuri yake, tena hayo mazuri yalikuwa ya mezidi ya walio wengi.

Hivyo badala kila siku kulaumu, kulaani, kutukana, kwaajili ya jana iliopita, ni bora tungejifunza walao moja positive litujenge kwaajili ya kesho inayo tukabili.
 
Back
Top Bottom