= mahaliDah!
Huyo mzee kyaruzi nikikuwa namfahamu sana kabla hajafariki, makazi yake yalikuwa pale maeneo ya uwanja wa ndege manispaa ya bukoba,alikuwa ananipa historia nabaki nimeduwaa!
Mungu amlaze mahari pema.
Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Namsubili Yericko aje kujibu hizi hoja.
Shikamoo bibi FaizaFoxy= namsubiri
Ndiyo wale wale.
Ulishamlipa haki yake yule kijana aliyekuja JF kulalamika kuwa umemtapeli?Shikamoo bibi FaizaFoxy
Unamzungumziaje Kleist Sykes aliyebadili dini kutoka ukatoliki safi akaacha kula nguruwe na kuwa muislamu ambapo leo mnalilia usiku na mchana?Ulishamlipa haki yake yule kijana aliyekuja JF kulalamika kuwa umemtapeli?
Mkuu Nguruvi3Wala nisingependa uwe tofauti na unavyojitambua
Nina uhakika wanaotusoma kuna kitu kinawashangaza hasa wakiona hoja za 'umanyema'
Kinachowaduwaza ni mahusiano ya Umanyema, Uislam, Uhuru na mada iliyopo
Ipo mantiki ya mambo hayo. Kwanza, Mohamed siku zote anaeleza mchango wa Waislam katika kupigania Uhuru.
Ni kweli mchango huo haupaswi kubezwa au kufutwa katika historia
Hata hivyo Mohamed anakuwa na ''jicho pembe'' kwa kutotambua michango ya wengine
Mohamed ana link Quran , Uislam na Kiswahili kwa makusudi kabisa.
Na hapa asiulize mtu tofauti ya Quran na Uislam, ieleweke ipo dhahiri
Mohamed 'anaukana' Umanyema kwasababu kujinasibisha nao kutaondoa ' uhalali' ;
1. Kwamba ni Wageni tu kama alivyokuwa Nyerere
2. Kwamba Umanyema ukiingia, basi kutakuwa na Udengereko, Uzaramo n.k.
Ukitaka kuandika historia kwa jicho la Udengereko, Uzaramo , Uluguru au Umanyema utakuwa umepunguza nguvu ya hoja ya 'Uislam na Uhuru'.
Ili kujenga hoja hiyo ni lazima 'kuua' hoja za makabila, kwa upande wake Umanyema
Hapo ndipo Mohamed anapata hoja ya kabila la Waswahili lenye mahusiano na lugha ya kiarabu iliyobeba Quran inayotumiwa na ''Waislam'' na iliyofanikisha Uhuru
Ndiyo maana lugha anyoijua ni Kiswahili na Kiarabu
Ni kwa ufupi tu
Boyswise,Mkuu Nguruvi3
Kwani wewe bado ni mgeni na kazi za Mzee Mohamed Said katika Historia ya Uhuru wetu?
Kwanza nikupongeze kwa kukubali kwako kuwa nikweli upo mchango wa baadhi ya Waislamu katika uhuru wetu na bila shaka Mzee Mohamed Said amekusaidia sana katika hili.
Mzee Mohamed Said ameeleza wazi kuwa alichukua jukumu la kuufahamisha umma kuhusu mchango wa Waislamu baada ya kuwa hapakua na popote katika Historia ya Tanu na Uhuru ulipotajwa sasa kwa hili ulitaka awataje na wasiokua Waislamu?
Lakini pia itakua vema kama nawe utakuja na majibu ya kuwa kwanini mchango wa Waisamu umepuuzwa na hata baadhi yao kufikwa na madhila baada ya huo uhuru kupatikana.
Boywise
Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani wewe ni mgeni katika majadiliano baina yetu na Mohamed."boywise, post: 22685677, member: 423208"]Mkuu Nguruvi3
Kwani wewe bado ni mgeni na kazi za Mzee Mohamed Said katika Historia ya Uhuru wetu?
Kwanza nikupongeze kwa kukubali kwako kuwa nikweli upo mchango wa baadhi ya Waislamu katika uhuru wetu na bila shaka Mzee Mohamed Said amekusaidia sana katika hili.
Historia haiandikwi kwa utashi wa mtu, maono au chaguo 'cherry-pick'Mzee Mohamed Said ameeleza wazi kuwa alichukua jukumu la kuufahamisha umma kuhusu mchango wa Waislamu baada ya kuwa hapakua na popote katika Historia ya Tanu na Uhuru ulipotajwa sasa kwa hili ulitaka awataje na wasiokua Waislamu?
Kuna vitu viwili unachanganya katika hili.Lakini pia itakua vema kama nawe utakuja na majibu ya kuwa kwanini mchango wa Waisamu umepuuzwa na hata baadhi yao kufikwa na madhila baada ya huo uhuru kupatikana.
bravo!Nadhani wewe ni mgeni katika majadiliano baina yetu na Mohamed.
Akitoa toleo la kwanza wengine tulishahoji kitambo sana kuhusu historia iliyokuwepo
2011 tulipoanza kujadili vitabu vyake, sikumbuki mtu aliyekataa mchango wa Waislam
Ni kutokana na ukweli mji mkuu ulikuwa Pwani wakazi wengi Waislam
Haina maana mapambano ya uhuru yalikuwa Pwani peke yake, la hasha.
Kwingine kulikuwa na vugu vugu la kukataa udhalimu.
Huko walipokuwepo bado walitoa mchango mkubwa Historia haiandikwi kwa utashi wa mtu, maono au chaguo 'cherry-pick'
Huwezi kuandika historia ya dunia ukamweka Hitler pembeni kisa humpendi
Huwezi kuandika historia ya Tanganyika ukaondoa watu wengine kisa hawahusiki
Ni makosa yale yale uliyosema yaliwaondoa Waislam katika historia kwa kutotajwa ndiyo unapigia upatu wa kuondoa makundi mengine kama afanyavyo Mohamed. Umeona!
Historia ni mtiririko wa matukio kama yalivyotokea na kujidhihiri
Ukiandika historia na kumwacha John Rupia, Cecil Matola, Vedastus Kyaruzi na wengine kwasababu si Waislam historia haikamiliki. Haikamiliki kwasababu kutakuwa na matundu
Ni kwa mantiki hiyo, hakuna kitu kinaitwa historia ya Waislam kupigania uhuru ukiacha wahusika wasio waislam. Kuna Historia ya Tanzania ambayo ndani yapo makundi
Kuna vitu viwili unachanganya katika hili.
Kwanza, kuna kupigania uhuru na pili kuna yatakanayo baada ya kupata uhuru.
Uhuru ulipoiganiwa ilikuwa ni suala la kiutu na kibinadamu.
Mohamed Said amenukuu Aabdul Sykes akieleza kuhusu hili.
Hivyo jitihada za ''kujikomboa zililenga kurudisha utu na heshima ya Mwafrika''
Baada ya uhuru kukaja suala la kujitawala.
Hapa tukaondoka katika harakati za utu na ubinadamu tukaingia katika siasa.
Ilikuwa ni dhahiri Waislam walitaka kuchukua haki ya kupigania Uhuru na kuifanya haki ya kisiasa, rejea hotuba ya Rehan Bilal Waikela, moto wa Waislam ukiwaka
Kisiasa hakuna anaye vumilia matishio katika utawala, bila shaka Nyerere hakuwa tofauti.
Lakini pia utambue tulihitaji umoja wa Taifa kwani tulikuwa hatuna Utaifa kwa kuanzia.
Kundi moja linapochukua mapambano ya uhuru na kujimilikisha halikuwa jambo sahihi
Kuna nchi zilijaribu zimeishia katika matatizo makubwa heri yetu sisi tuliojaribu vinginevyo
Historia ni reflection ya yaliyotokea. Dunia ya sasa inazungumzia historia kama kumbu kumbu kwavile asilimia zaidi ya 90 hawakuwepo wakati huo na ni vizazi vya 3 au 4
Tatizo linaljitokeza katika maandishi ya Mohamed, ni kuhamasisha watu kuhusu 'umiliki' wa historia ili kujenga hoja katika msingi wa historia.
Inaweza kuonekana ni jambo jema kwa wakati huu, siku za mbeleni ni jambo lenye athari kubwa kwa jamii ile ile anayoizungumzia
Unapopandikiza fikra kuwa babu au bibi walipigania uhuru na hivyo unapaswa kubebwa na historia ni kujidumaza. Historia itumike katika reflection kwa mambo mazuri
Kwamba kama yupo aliyetoa mali zake kusaidia uhuru, kwanini wasiwepo wanaotoa mali zao kubadilisha hali za jamii kielemu, uchumi au utamaduni? Hiyo ndiyo kazi ya historia
Athari za mantiki iliyotafsiriwa na jamii ni kuwa wapo waliopigania uhuru wanaonewa
Mohamed kajenga historia kwanza, halafu katumbukiza mbegu hizo(rejea takwimu za elimu kuhusu mitihani) na nafasi za kazi kwa mujibu wa mijadala tuliyokuwa nayo
Jamii inaondoa focus kwenye 'real problem' na kudhani suluhisho ni historia.
Huwezi ku qualify kuwa mwandishi mzuri kama Mohamed kwasababu ya historia kama ambavyo huwezi kuwa Eng., Entrepreneur, Mhasibu, Daktari au professor kwa historia
Ikiwa wazee wetu waliji organize wakaondoa tofauti na kupigana na mkoloni, kwanini kiwepo kizazi kinachotaka kusimama katika mabega yao bila kizazi hicho kuweka miguu chini ili kingine kijacho kijifunze kutoka kwao?
Nguruvi3 na Mtanganyika,bravo!
Boyswise,
Ahsante kaka.
Soma kitu hiki kutoka kwa marehemu Ally Sykes akieleza katika mswada
wake wa kitabu, ''Under the Shadow of British Colonialism," harakati zake
dhidi ya Waingereza wapi alipata mafunzo:
''...in Burma I had known Waruhiu Itote popularly known as “General” China with whom I had served in the K.A.R. General China came to be one of the leaders the Mau Mau force fighting the British in the Aberdeen Mountains. At the beginning I did not realise how deep Kariuki was involved in that underground movement and if he had at all taken the Mau Mau oath. The oath I later came to learn was the driving force behind the success of the Mau Mau movement because once taken one was to obey and undertake whatever assignment given. Usually the assignment was to kill white settlers. It was at the Central Hotel that I came to meet Jomo Kenyatta, Bildad Kaggia, Tom Mboya, W.W. Awori and other Kenyan nationalists. I used to talk about my father and his activities in Tanganyika to further many issues of African interests. Mboya was a keen listener and he used to urge me to return home and help in the struggle...''
Mzee Mohamed SaidBoywise,
Nguruvi3 anasema ati wewe mgeni katika mjadala huu.
Kaguswa na ukweli uliomueleza tena kwa utulivu.
Nataka nikuongezee kitu kutoka hicho kipande ambacho Ally Sykes anamueleza
baba yake Kleist Sykes.
Msome Kleist Sykes kama nilivyomwandika katika Dictionary of African Biography
(DAB):
Kleist na wanawe watatu wote walishiriki katika siasa za uhuru wa Tanganyika na kuunda TANU
Xungura na Boywise,Kwenye huu mjadala
Yeriko ni mdini na nguruvuvi pia maana hawajibu hasa kwa nini hostoria ya waislamu ilifichwa na sababu gani ilifanywa historia yao ifichwe
Sent using Jamii Forums mobile app
Inaweza kuwa ni kweli sisi ni wadini,Kwenye huu mjadala
Yeriko ni mdini na nguruvuvi pia maana hawajibu hasa kwa nini hostoria ya waislamu ilifichwa na sababu gani ilifanywa historia yao ifichwe
Sent using Jamii Forums mobile app