Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Mohamed Said tunapata elimu hapa lakini"mmejaa hasad na wivu katika nyoyo zenu,mnataka hata kisicho chenu" hii ni lugha ya mipasho waachie watu wa vijiweni
Hiyo lugha siku zote hutumia pale penye challenge
Hatakoikabisa kupata challenge, anachotaka ni watu kusoma tuu kama riwaya!!

'Hasad na wivu katika nyoyo zenu'' wivu wa kitu gani wakati ni historia
'Mnataka kisicho chenu' akina nani na wanataka nini ikiwa ni historia ya nchi

Halafu anasema alikuwa Cambridge, sijui huko huwa hawana hoja au hawafanyi 'critique'
 
Mzee Mohamed
Vijana tunasoma endelea kutufundisha na tunapokuuliza maswali tambua wazi ni katika kutaka kujua
,,, maana hatuna uwezo wa kukujibu
Well anataka nijibu yatokanayo na historia ya Kivukoni, sasa nitamjibu nini ikiwa sikuwahi kushiriki kuandika historia hiyo? Kama huna uwezo ni wewe, unaposema hatuna , na akina nani?
 
Mohamed Said tunapata elimu hapa lakini"mmejaa hasad na wivu katika nyoyo zenu,mnataka hata kisicho chenu" hii ni lugha ya mipasho waachie watu wa vijiweni
Jackline,
Hii hasad ipo sana wala si kama nasema lugha ya vijiweni.

Maana ya hasad ni kutaka ile neema ambayo Allah kamjalia mja wake
imuondoke.

Wanataka historia hi iwe siyo.

Kitabu kimechapwa miaka 20 iliyopita na nimesema yote niliyotaka
kusema.

''Reviews,'' zimefanywa nyingi tena katika, 'journals,'' maarufu.
Yeye kakalia hapa JF bugudha kila kukicha na kejeli.

Hivi haoni kama sisi ni watu tofauti sana?

Mimi na yeye tunacheza viwanja viwili tofauti mimi niko katika kurasa
za vitabu yeye akiwa anataka na aje huku.

Nini kinamshinda?

Historia ya TANU hiyo iliyoandikiwa siyo hii hapa historia ya TANU tena
naandika historia ya wazee wangu.

Wewe uandike maisha ya babu au baba yako mimi inichome.
Inaingia akilini?

Tatizo liko wapi?
Vipi mtu awashwe kiasi hiki?

Una historia kinyune ya hii yangu si uandike?
Tatizo liko wapi?
 
Hiyo lugha siku zote hutumia pale penye challenge
Hatakoikabisa kupata challenge, anachotaka ni watu kusoma tuu kama riwaya!!

'Hasad na wivu katika nyoyo zenu'' wivu wa kitu gani wakati ni historia
'Mnataka kisicho chenu' akina nani na wanataka nini ikiwa ni historia ya nchi

Halafu anasema alikuwa Cambridge, sijui huko huwa hawana hoja au hawafanyi 'critique'
Nguruvi3.
Critique...
Inakuchoma hiyo Cambridge...
Vipi hii hapo chini?:

USYpyXxAvbPJ-x8FmYCkzGWfUSzH1ezSW5XLiuzA66wetSq_okOXJtaKeS9umn4iB3x_KNZoIVVE3Zn90mpOTXuwwgbM4XRiFC1mfG302-B-AvjcvztdTDT6hVjtujuDjnPp8YmWV18OYHDzs7Q23LXwaXphruAdHdJVYoPUFU30IoAXjyfSivSc6V8Ls4Pfmyw9k3aloTQIPIsi1uHiq57papIRnXCmpIwTt2TtZ-SMyExLX-yPvizh7aI_BTLiiixixs9sv28SY0lIGjPI4UeouIwlU_6NZH3EAmeJWvEf1YCKTOxTxcP2tmI7Umv3uy7XWJut82QwGHC1D_Xlcy6viiozqgnNdFV1bVygWjUHHDoA8rA1ijwB7cIgJnSelA9NEolzWxJNTRQXdINI4rw1PGPacoWJ2CQz_GK7ecv_LwcVSUdW-o7eW4Y94H9IyY5NPxX1R3DX4jcDWXePSvZgc3Sqz_5_803vgStsNpEPkNBdg1X3LUtDu7zwSMY75s6Y4Pyb4FUOS3iykJNx3_dVBEdih3Gkk0RNU83Nei-DZjAKQJB0iVredZF0WlCr7vRTVT5PWrndksleb8Jp-y2DhwT7OYYekQZGzvpJgBZn-7y092aSgvnVxKgX1M9Y15dIMH0lcLtiAc-ZgChQ0pWShfsqyTTS5r2Q1cfD80NxXB4=w480-h360-no


Junior Mwang'ombe Northwestern university ni chuo kizito Sana marekani katika vyuo kumi bora nacho kimo Asante kwa history hii mzee wetu
Like
· Reply · 9 hrsManage

Mohamed Said Salum
Junior Northwestern University Department of African History walinialika hapo na nikafanya mhadhara katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane.
Like
· Reply ·
1
· 4 hrsManage

Junior Mwang'ombe
Mohamed Said Salum Mashallah
Like
· Reply · 4 hrs
 
Nilicho kiona kwenye mjadara huu yerickot anataka kushindama na Mohammed said ndilo tatizo lake na ukiona mtu hataki kukosolewa ujue ana matatizo je kitabu kitakuaje kama muandishi hataki kuelekezwa kitabu kitakuwa mapungufu mengi kitasomwa na watu mbugira mbugira alimradi wao ni kusoma bila kujua wanasoma nini hongera mzee wetu Muhammad saidi kwa kazi unayo ifanya mungu atakulipa ingawa unaitwa mdini usihuzunike kwa kuwa history iko hivyo inaonyesha waislam ni asilimia kubwa ndio walianzisha vugu vugu la kudai uhuru sasa ukisema kweli baadhi ya wakristo wenzangu hawapendi wewe tuelimishe dini yako baki nayo wewe sisi tupe history ili watoto wetu tuje kuwafundisha history ya kweli ya tanganyika nakupenda sana mzee wetu kwa elimu unayo tupatia

Sent using Jamii Forums mobile app
Isk,
Ahsante sana.
Hebu soma hii hapo chini:

KUTOKA JF: WAHARIRI WA DAILY NEWS NA UHURU WALIVYOTATAZIKA NA ABDUL SYKES 1988
Mohamed Said June 14, 2014 0

1. Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
grey10.gif
By THE BIG SHOW
Moh said.


Tulishakuambia sisi tunakesha humu.

Hatubanduki labda ubanduke wewe.


Popote pale ulipo wewe sisi tunaweka kambi.

Shusha Vituu.

abdulwahid-1.jpg


image+%252811%2529.jpg


abdulwahid-3.jpg

The Big Show,
Tumeishia pale ambapo 1988 Africa Events ilipochapa kumbukumbu
ya Abdul Sykes kuadhimisha miaka 20 baada ya kifo chake mwaka
1968.

Kuna kisa cha bibi moja wa Kiingereza anaitwa Paula Parks.
Bibi huyu alikuwa mmoja wa waandishi wa Africa Events.

Kisa chake utakiona hapo chini.
Baada ya Africa Events kuchapa ile kumbukumbu...

Tuendelee.

Ukoo wa Sykes wakanunua nafasi katika magazeti ya Daily News
na Uhuru kuchapa kumbukumbu ya Abdul Sykes.

Hebu soma hapo chini nini kilitokea:
''In response to Kiwanuka’s criticism the author published a short
biography of Abdulwahid to commemorate twenty years of his
death.[1] This was followed by a memorial by the family in the
Party and Government papers.[2] This was not to pass without
incident. The editor of the Daily News, the government paper,
rang up the family late in the night informing them that he
would not publish Abdulwahid’s memorial the following day
until he got permission from Party headquarters in Dodoma.
The reason given was that his life history touched important
events and personalities in the history of the nation.
But somehow
the memorial was published in both the Party and government dailies
the following morning.

Two years earlier in 1986, after a silence of almost twenty-five
years, Ally Sykes gave an interview to a British journalist, Paula
Park.
Park wrote a full page article on the family’s political history. [3]
When the article was published Ally Sykes received telephone calls
from both friends and business associates asking him if he was
quoted correctly. Shortly after, Park was quietly asked by immigration
officials to leave the country.''

Kitu ambacho ningependa kueleza hapa ni kuwa ingawa kumbukumbu
zilichapwa lakini uhariri wake ulikuwa mkali sana.

Mambo muhimu katika maisha ya Abdul Sykes yalikatwa.

Wanajamvi,
Kitu cha kujiuliza ni hiki:

Ni kitu kipi kinasababisha hii hofu katika maisha ya Abdul Sykes?

[1] See M. Said, ‘Founder of a Political Movement: Abdulwahid K.
Sykes
1924-1968’, Africa Events, London September, 1988, pp.
38-41.

[2] See Daily News, 23 rd October, 1988. Also Uhuru, 23 rd October,
1988.

[3]" ‘An Unsung Hero?’ Africa Events, London, November 1986 p.48.
Last edited by Mohamed Said; Today at 06:38.
 
Well anataka nijibu yatokanayo na historia ya Kivukoni, sasa nitamjibu nini ikiwa sikuwahi kushiriki kuandika historia hiyo? Kama huna uwezo ni wewe, unaposema hatuna , na akina nani?
''Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walifahamiana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora. Chama hakiwezi kupinga ukweli kwamba Kasella Bantu alikuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waasisi wa TANU. Hali kadhalika chama hakiwezi, kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ‘’kuandika’’ ile katiba ya TANU. Kasella Bantu anakerwa sana na kupotoshwa kwa historia. Kila alipopata fursa kuanzia alipokuwa ngíambo uhamishoni na hata baada ya kurudi nyumbani kutoka uhamishoni, Kasella Bantu ameeleza kuhusu mambo haya mawili ya kihistoria, kuwa ‘’aliandika,’’ katiba ya TANU na ni mmoja wa waasisi wa TANU. Bantu kama waanzilishi wengine wengi anahisi kwamba mchango wake katika harakati za uhuru wa Tanganyika haujathaminiwa.''

''Jopo la wana-historia wa Chama Cha Mapinduzi waliopewa jukumu la kutafiti na kuandika historia rasmi ya TANU, hakuna hata sehemu moja waliyotaja jina la Abdulwahid katika kitabu kizima.Dhana inayojaribiwa kuenezwa katika kitabu kile ni kuwa kabla ya kutokea kwa Julius Nyerere mwezi Aprili, 1953, alipochaguliwa kuwa rais wa TAA, chama hicho hakikuwa na mwelekeo wowote wa siasa. Kitu cha ajabu ni kuwa kitabu hicho wala hakielezi huo urais wa TAA, Nyerere aliupataje au aliuchukua kutoka kwa kiongozi gani wa wakati ule. Kitendo hiki kimeondoa hadhi na heshima ya wazalendo wengi waliopigania nchi hii na halikadhalika kimeiondolea TAA heshima ya kuitwa chama cha siasa. Wanahistoria wazalendo pamoja na wanasiasa wa sasa hawataki kabisa kuipa TAA hadhi ya chama cha siasa. Kambona aliiita African Association chama cha majadiliano:

‘’Sasa inakaribia mwaka mmoja toka iundwe Tanganyika African National Union na katika kipindi hiki chama kimekua kikipata nguvu siku hadi siku, wakati mwingine chini ya upinzani mkubwa. Kama mnavyofahamu chama hiki ni badala ya Tanganyika African Union ambayo ilikuwa sawasawa na chama cha majadiliano.’’


Ulotu anaieleza TAA kuwa ilikuwa chama cha ustawi wa jamii. Wengine wameieleza TAA kama taasisi ya jamii: Nyerere (1976), halikadhalika Japhet na Seaton (1966). TAA wakati mwingine inaelezwa kuwa ilikuwa chama cha vuguvugu za upinzani dhidi ya ukoloni, lakini upinzani wake haukuwa dhahiri: Kaniki (1974), Nyerere (1953) aliieleza TAA kama chama cha vuguvugu la siasa lakini si za dhahiri. Julius Nyerere alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 7 Machi, 1955 alisema:

''Tanganyika African National Union kwa mtazamo mmoja ni chama kipya, lakini kwa mtazamo mwingine ni chama kikongwe. TANU imechukua nafasi ya Tanganyika African Association ambayo ilianzishwa mwaka 1929, kama chama cha kijamii. Tanganyika African National Union, chama kilichochukua nafasi ya African Association miezi kumi iliyopita ni chama kipya kwa maana ni chama cha siasa, wakati TAA ilikuwa chama cha siasa nusunusu.


Wasomi wengine wameishusha TAA kufikia daraja la kuwa klabu: Mwenegoha (1976) anaandika: ëMwaka 1954, baada ya miaka ishirini na tano ya kutoweza kufanya lolote, Nyerere aliigeuza TAA kutola chama cha kijamii kuwa chama cha siasa chenye kuogopwa kilichoitwa Tanganyika African National Unioní.


Abdulwahid ambae alitoa mchango wa pekee katika kuunda TANU alikuwa anaiona TAA kama chama cha siasa (1951). Katika kundi la waandishi na wasomi walioandika kuhusu African Association kisha wakabadili mawazo yao kuhusu nini hasa chama kile kilikuwa, ni Nyerere na Hatch ndiyo waliobadili misimamo yao ya awali. Nyerere alipoandika barua kwa Gavana wa Tanganyika, Edward Twining tarehe 10 Agosti, 1953 alieleza kuwa TAA ni chama cha siasa. Lakini baadae alibadili msimamo na kusema kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe. Kauli hii ilitawala hotuba za Nyerere na maandishi yake kwa kipindi kirefu. Katika miaka ya hivi karibuni amesikika akisema kuwa TAA kilikuwa ëchama cha siasa kisichokuwa na katiba ya siasaí. Hatch (1976) ameieleza TAA kama chama cha starehe sehemu moja na chama cha siasa sehemu nyingine. John Kabudi ameieleza African Association kama ëchama cha watu binafsi wananchi kilichokuwa na mwelekeo wa kitaifa.''

Joseph Kimalando kwa Hon. General Secretary, 9 Septemba, 1953. ‘’Government Circular on Membership of Political Associations.’’ Maktaba ya CCM. File 168 Folio 2.

Pacha anayo muhtasari ya ule mkutano mkuu wa Julai, 1954 lakini hakuwa na rasimu ya katiba ambayo haikuweza kupatikana Maktaba ya CCM Dodoma. Bukoba ilipokea rasimu hiyo, angalia barua ya M. Lugazia kwa katibu Tawi la Bukoba DC/ HQ/ LP/ 897 Mei, 1854. Felio 16 TANU 16 lakini rasimu ya katiba iliyotajwa humo haimo ndani ya barua hiyo.

M. Lugazia kwa katibu Tawi la Bukoba DC/HQ/BK/LP/897 May, 1954 (tarehe haikutolewa) TANU folio 16 Party Archives, Dodoma. Rasimu ya katiba iliyotajwa hapo imekosekana.

Uongozi wa TAA haukurasimu katiba mpya. Katiba ya TANU ilinukuliwa neno kwa neno kutoka Convention People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah, kwa kutia TANU mahali pa CPP. Maelezo kutoka kwa Tewa Said Tewa.
 
"
Mohamed Said, post: 22753614, member: 12431"]' Hali kadhalika chama hakiwezi, kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ‘’kuandika’’ ile katiba ya TANU.

Dhana inayojaribiwa kuenezwa katika kitabu kile ni kuwa kabla ya kutokea kwa Julius Nyerere mwezi Aprili, 1953, alipochaguliwa kuwa rais wa TAA, chama hicho hakikuwa na mwelekeo wowote wa siasa.

Kitu cha ajabu ni kuwa kitabu hicho wala hakielezi huo urais wa TAA, Nyerere aliupataje au aliuchukua kutoka kwa kiongozi gani wa wakati ule.

Wanahistoria wazalendo pamoja na wanasiasa wa sasa hawataki kabisa kuipa TAA hadhi ya chama cha siasa. Kambona aliiita African Association chama cha majadiliano:

Ulotu anaieleza TAA kuwa ilikuwa chama cha ustawi wa jamii.

Wengine wameieleza TAA kama taasisi ya jamii: Nyerere (1976), halikadhalika Japhet na Seaton (1966).

TAA wakati mwingine inaelezwa kuwa ilikuwa chama cha vuguvugu za upinzani dhidi ya ukoloni, lakini upinzani wake haukuwa dhahiri: Kaniki (1974), Nyerere (1953) aliieleza TAA kama chama cha vuguvugu la siasa lakini si za dhahiri.

Julius Nyerere alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 7 Machi, 1955 alisema:

TANU imechukua nafasi ya Tanganyika African Association ambayo ilianzishwa mwaka 1929, kama chama cha kijamii. Tanganyika African National Union, chama kilichochukua nafasi ya African Association miezi kumi iliyopita ni chama kipya kwa maana ni chama cha siasa, wakati TAA ilikuwa chama cha siasa nusunusu.

Wasomi wengine wameishusha TAA kufikia daraja la kuwa klabu: Mwenegoha (1976) anaandika: ëMwaka 1954, baada ya miaka ishirini na tano ya kutoweza kufanya lolote, Nyerere aliigeuza TAA kutola chama cha kijamii kuwa chama cha siasa chenye kuogopwa kilichoitwa Tanganyika African National Unioní.
Hizo sentensi nilizonukuu hapo ni muhimu sana na nashkuru umezileta

Swali la msingi linaloweza 'ku-test' nadharia za wote waliozungumza ni moja
Je, kabla ya Nyerere kuandika katiba , ni wakati gani na nani mwingine aliyewahi kufanya hivyo

Nyerere alishirikiana na Kasela Bantu kwa mujibu wako. Swali linabaki pale pale kuwa kabla ya Uongozi wa Nyerere ni akina nani wengine waliandika katiba ya chama iwe AA au TAA au vinginevyo
Abdulwahid ambae alitoa mchango wa pekee katika kuunda TANU alikuwa anaiona TAA kama chama cha siasa (1951).
Abdul Wahid kuona TAA kama chama cha siasa si lazima iwe hivyo

Mtazamo wa Abdul ni maoni yake, na angeweza kusema ni chama cha Wa-south Africa.
Ni maoni yake. Unapojaribu kuyafanya kama ukweli ni kupotosha umma

Tuambie chama cha AA au TAA kilikuwa na mwongozo gani wa kukifanya kiwe cha siasa nje ya maono ya Abdul. Tukifuata maoni ya watu Watoto wa Mkwawa na Mirambo wanaweza kusema Iringa na Tabora vilikuwa ''vyama vya siasa'' Tufuate ukweli kama historia ilivyoonyesha
Uongozi wa TAA haukurasimu katiba mpya. Katiba ya TANU ilinukuliwa neno kwa neno kutoka Convention People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah, kwa kutia TANU mahali pa CPP. Maelezo kutoka kwa Tewa Said Tewa.
Swali lipo pale pale, kabla ya Nyerere ni nani mwingine aliyekuwa na mawazo japo ya kunukuu neno kwa neno ili aandike katiba na ni lini.
 
Ni rahisi kumwamsha aliyelala kuliko yule anaejifanya kalala.

Andika kitabu ndugu yangu mimi na wewe tuko mbali mbali sana.

Andika jinsi Baba wa Taifa alivyounda TANU.
Huu utakuwa mchango mkubwa kutoka kwako.

Hii kila kukicha tunakirejea kitabu kilichoandikwa miongo miwili iliyopita unajichosha pasi na sababu ya maana.

Mimi nimeandika vitabu kadhaa na paper nyingi tu wewe unaandika JF.

Hivi ni viwanja viwili tofauti.

Huku kwangu ziko adabu zake.
Hapa JF ni mpata mpatae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi kumwamsha aliyelala kuliko yule anaejifanya kalala.

Andika kitabu ndugu yangu mimi na wewe tuko mbali mbali sana.

Andika jinsi Baba wa Taifa alivyounda TANU.
Huu utakuwa mchango mkubwa kutoka kwako.

Hii kila kukicha tunakirejea kitabu kilichoandikwa miongo miwili iliyopita unajichosha pasi na sababu ya maana.

Mimi nimeandika vitabu kadhaa na paper nyingi tu wewe unaandika JF.

Hivi ni viwanja viwili tofauti.

Huku kwangu ziko adabu zake.
Hapa JF ni mpata mpatae.
Maelezo yote haya hayajajibu swali la msingi

Ni nani kabla ya Nyerere aliwahi kuandika katiba ya chama iwe AA au TAA japo kwa kunukuu za wenzake

Bila swali kupata majibu, nadharia (theory) yoyote kuhusu AA au TAA inaweza kuwa sahihi. Ili tufungue macho kwa pamoja, majibu ni muhimu

Ni muhimu kwa jamvi na muhimu sana kwa vijana wanaodhani 'unashambuliwa'
Nao pia mnaweza kuungana kuja na majibu

Ndiyo maana nakuuliza, katika nadharia zote tufanye test ili kujua ukweli upo wapi

Swali lipo pale pale , nani aliandika katiba kabla ya Nyerere na ni kwa chama gani na ilikuwa lini
 
Kifua kimejaa joto.
Joto linapofusha.

Unaruka huku na huku mfereji umeuweka kati.

Tewa keshatuambia kuwa walinakili katiba ya Nkrumah.

Hutaki.
Basi andika wewe kitabu chako.

Huna uwezo huu mwaka wa sita nakusihi.
Ati mie niungane na watu kukukabili wewe.

Kwa ujanja upi uliokuwanao?

Ati anaandika neno la Kiingereza ananiwekea maelezo ilhali kitabu kizima nimeandika kwa lugha hiyo.

Unadhani nababaisha?

Niko kwenye mradi wa Oxford University Press wa kufundisha lugha ya Kiingereza katika shule za Afrika ya Mashariki na nimeandika vitabu viwili kimoja ni Anthology nimejimuika na waandishi wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Roho inakuuma kwa husda.

Mwezi wa Ramadhani nimemaliza translation ya kazi kubwa sijapatapo kupewa maishani.

Bado.
Roho inakwenda mbiyo kwa wivu.

Zidisha hasad na kejeli.

Nakudokeza kitu kuhusu hiyo katiba unayodhani itanikomoa.

Unamjua mwanasheria Earle Seaton?
Unajua kuwa alikuwa rafiki yake Abdul Sykes?

Unajua alikuwa katika Political Subcommittee ya TAA ya Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Chaurembo, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Stephen Mhando na John Rupia lakini jina lake hulioni?

Hii ilikuwa 1950.

Haikuingii akilini kuwa hapo kwa Seaton ndipo palipotoka mengi pamoja na hiyo katiba ya CCP na mapendekezo ya Constitutional Development Committee iliyopelekwa kwa Gavana Twining?

Unajua kama hili document halionekani na aliyelichukua kutoka Secretariat hajulikani?

Ufungue macho na Mohamed Said.

Mimi ndiyo mwenye ufunguo uliofungua historia ya TANU inayokuchoma roho.

Au hukuona nyaraka zilizokuwa zimenyofolewa katika mafaili ya TANU?

Nina kitu nimeandika kuhusu hizo nyaraka.
Mhariri alinikatalia mie kusema zimeibiwa.

Ingia katika kitabu cha Abdul Sykes yote nimeeleza hayo.

Andika kitabu ujanja ujanja utaishia humu humu unajitekenya na kujichekesha mwenyewe.

Bookseller mmoja kanipigia simu ananiuliza mbona ghafla upya kitabu kinanunuliwa kama maandazi ya moto?

We bakia na maswali yako ya msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkubwa, vuta subra kidogo. Pata funda la maji kaa kitako ujitulize
Joto na wahka umekupanda najisikia mnyonge! Nisamehe Mohamed, lakini siombi radhi kwa hoja. Dawa chungu lakini tufanyeje, ndio utabibu wenyewe. Tuliza joto
"Mohamed Said, post: 22755546, member: 12431"]Kifua kimejaa joto.
Joto linapofusha.Unaruka huku na huku mfereji umeuweka kati.
Hutaki.Basi andika wewe kitabu chako.Huna uwezo huu mwaka wa sita nakusihi.
Ati mie niungane na watu kukukabili wewe.Kwa ujanja upi uliokuwanao?
Ati anaandika neno la Kiingereza ananiwekea maelezo ilhali kitabu kizima nimeandika kwa lugha hiyo.Roho inakuuma kwa husda.Roho inakwenda mbiyo kwa wivu.
Zidisha hasad na kejeli.Ufungue macho na Mohamed Said.
Mimi ndiyo mwenye ufunguo uliofungua historia ya TANU inayokuchoma roho.
Andika kitabu ujanja ujanja utaishia humu humu unajitekenya na kujichekesha mwenyewe.
Mohamed, naogopa akina Hadija Kopa wasijetushtaki kwa kuiba kazi zao
Una hati miliki weye! Mimi sina!

Tukirudi kwenye mada hadi hapo juu hujaeleza umma, katiba ya AA au TAA iliandikwa na nani, mwaka gani na ilitumiwa wakti gani. Hili ndilo swali
Bookseller mmoja kanipigia simu ananiuliza mbona ghafla upya kitabu kinanunuliwa kama maandazi ya moto?
Huwezi jua huenda wanafuatilia na kugundua walichokuwa hawakioni.
Yaweza kuwa ni watu wa taarabu wamevutiwa na mashairi . Yote kheri kama kitabu kinauzika
Tewa keshatuambia kuwa walinakili katiba ya Nkrumah.
Tewa 'kasema' si Abdul tena! unanikumbusha kitu kinaitwa pendulum .

Je ilikuwa nukuu kutoka wapi na nani alinukuu. Kabla ya hapo kulikuwa na katiba gani ambayo AA au TAA ilitumia
Unadhani nababaisha?
Ukisema Tewa kasema, Abdul kasema si ndio kubabisha kwenyewe? au!
Niko kwenye mradi wa Oxford University Press wa kufundisha lugha ya Kiingereza katika shule za Afrika ya Mashariki na nimeandika vitabu viwili kimoja ni Anthology nimejimuika na waandishi wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Kiingereza changu ni cha Darsa la VB ukiona naweka maneno ujue najitutumua. Ahsante kwa mradi unaofanya, Watanzania tunajivunia manguli kama wewe

Je, haya ndiyo majibu ya nani aliandika au alinukuu katiba ?
Na kabla ya Nyerere nani mwingine alinukuu au kuandika katiba na kuiweka hadharani?
Tafadhali usije niambia Abdul alisema!
Mwezi wa Ramadhani nimemaliza translation ya kazi kubwa sijapatapo kupewa maishani.
Mashallah, jambo jema hongera sana.
Nakudokeza kitu kuhusu hiyo katiba unayodhani itanikomoa.
Hee !unadokeza kwa kuogopa nini, eleza kwa ufasaha kuhusu katiba.

Hilo si kosa la madai au jinai ndiyo starehe ya mnakasha na elimu.
Ukidokeza utawanyima vijana wako faida, eleza
Unamjua mwanasheria Earle Seaton?Unajua kuwa alikuwa rafiki yake Abdul Sykes?
Ahaa! lakini Abdul hakuwa mwanasheria kutokana na urafiki na mwanasheria
Seaton ndipo palipotoka mengi pamoja na hiyo katiba ya CCP na mapendekezo ya Constitutional Development Committee iliyopelekwa kwa Gavana Twining?
Kabla ya hapo kulikuwa na katiba gani.
Kumbuka hayo ni mapendekezo ya mwaka 1950
Unajua kama hili document halionekani na aliyelichukua kutoka Secretariat hajulikani?
Aliyechukua arudishe, ingawa haituelezi kuanzia 1950 kurudi nyuma katiba gani ilitumika, nani aliandika na kwa utaratibu gani.
Au hukuona nyaraka zilizokuwa zimenyofolewa katika mafaili ya TANU?
Nyaraka hizo zitatueleza kabla ya Nyerere katiba gani ilitumika?
We bakia na maswali yako ya msingi.
Ndiyo yananisaidia kuelewa bahti mbaya yanapandisha presha!

Nani alinukuu katiba ya kwanza ya TANU? Kabla ya hapo katiba gani ilitumiwa na AA au TAA?
Hapo ndipo tulipo, makabrasha yamenyofolewa, yameibiwa fulani alisema ni irrelevant the least to say!
 
Mkubwa, vuta subra kidogo. Pata funda la maji kaa kitako ujitulize
Joto na wahka umekupanda najisikia mnyonge! Nisamehe Mohamed, lakini siombi radhi kwa hoja. Dawa chungu lakini tufanyeje, ndio utabibu wenyewe. Tuliza joto Mohamed, naogopa akina Hadija Kopa wasijetushtaki kwa kuiba kazi zao
Una hati miliki weye! Mimi sina!

Tukirudi kwenye mada hadi hapo juu hujaeleza umma, katiba ya AA au TAA iliandikwa na nani, mwaka gani na ilitumiwa wakti gani. Hili ndilo swali Huwezi jua huenda wanafuatilia na kugundua walichokuwa hawakioni.
Yaweza kuwa ni watu wa taarabu wamevutiwa na mashairi . Yote kheri kama kitabu kinauzika Tewa 'kasema' si Abdul tena! unanikumbusha kitu kinaitwa pendulum .

Je ilikuwa nukuu kutoka wapi na nani alinukuu. Kabla ya hapo kulikuwa na katiba gani ambayo AA au TAA ilitumiaUkisema Tewa kasema, Abdul kasema si ndio kubabisha kwenyewe? au! Kiingereza changu ni cha Darsa la VB ukiona naweka maneno ujue najitutumua. Ahsante kwa mradi unaofanya, Watanzania tunajivunia manguli kama wewe

Je, haya ndiyo majibu ya nani aliandika au alinukuu katiba ?
Na kabla ya Nyerere nani mwingine alinukuu au kuandika katiba na kuiweka hadharani?
Tafadhali usije niambia Abdul alisema! Mashallah, jambo jema hongera sana. Hee !unadokeza kwa kuogopa nini, eleza kwa ufasaha kuhusu katiba.

Hilo si kosa la madai au jinai ndiyo starehe ya mnakasha na elimu.
Ukidokeza utawanyima vijana wako faida, elezaAhaa! lakini Abdul hakuwa mwanasheria kutokana na urafiki na mwanasheriaKabla ya hapo kulikuwa na katiba gani.
Kumbuka hayo ni mapendekezo ya mwaka 1950 Aliyechukua arudishe, ingawa haituelezi kuanzia 1950 kurudi nyuma katiba gani ilitumika, nani aliandika na kwa utaratibu gani.Nyaraka hizo zitatueleza kabla ya Nyerere katiba gani ilitumika? Ndiyo yananisaidia kuelewa bahti mbaya yanapandisha presha!

Nani alinukuu katiba ya kwanza ya TANU? Kabla ya hapo katiba gani ilitumiwa na AA au TAA?
Hapo ndipo tulipo, makabrasha yamenyofolewa, yameibiwa fulani alisema ni irrelevant the least to say!
Una mambo ya kutosha kuandika kitabu kaka.
Andika kitabu.

Hicho ndicho kipimo si hizi kejeli za joto la hasad
na maswali ya kurudiarudia ukitaka majibu ya kukupendeza.

Mimi nilipoona historia ya TANU siyo niliandika sikuenda Kivukoni
kufanya ugomvi wala sikupita CCM.

Kitabu hiki kipo na hakiwezi kuondoka kwa kuwa hakijakufurahisha.
 
Una mambo ya kutosha kuandika kitabu kaka.
Andika kitabu.

Hicho ndicho kipimo si hizi kejeli za joto la hasad
na maswali ya kurudiarudia ukitaka majibu ya kukupendeza.

Mimi nilipoona historia ya TANU siyo niliandika sikuenda Kivukoni
kufanya ugomvi wala sikupita CCM.

Kitabu hiki kipo na hakiwezi kuondoka kwa kuwa hakijakufurahisha.
Mohamed it's simple, jibu hoja tuendelee. Maswali ya kujirudia ni kwasababu hutaki yajirudie, na pili huna majibu ya kutosha na hivyo hutaki kuyasikia

Kabla ya Mwalimu Nyerere ni katiba gani ilikuwepo, na kama haikuwepo wanaosema vyama vilikuwa 'vilabu' ambayo wewe unasema si kweli, wanakosea wapi?

Sina maana wapo sahihi, bali kuna nadharia mbili, wanaosema AA na TAA vilikuwa vilabu vya siasa na wanaosema vilikuwa vyama vya siasa kama wewe

Ili kupata ukweli wa makundi hayo mawili, inatubidi tufante 'test' ya nadharia hizo

1. AA na TAA zilikuwa na wanachama ambao tunawajua viongozi wao na wanachama wao
Hili linatueleza mikusanyiko ya wanachama hao ilikuwa na 'common interest'

Makundi yote mawili yanakubaliana na hilo.

2. Je, mikusanyiko hiyo ya wanachama ilikuwa na viongozi?
Makundi yote mawili yanakubaliana kwasababu alikuwepo Kleist, Abdul n.k. kwa ushahidi

3. Je, viongozi hao walikuwa na miongozo ya jumuiya au mikusanyiko yao?
Hapa ndipo suala la katiba linaingia

Tujiulize,AA au TAA zilikuwa na katiba? Kama zilikuwepo nani aliandika? Kama hazikuandikwa zilinukuliwa na nani na kutoka wapi? Katiba hizo zilitumika wakati gani?

TANU ilikuwa na katiba? Nani aliandika au kunukuu katiba yake? Ilikuwa mwaka gani na chini ya uongozi wa nani?

Kwa mantiki ya maswali hayo ya MSINGI, inabidi turudi kwa mzee wetu wa Cambridge utusaidie kujenga hoja zenye ushahidi na si hadithi au mantiki za kuunganisha

Karibu sana mzee Said
 
Ndugu yangu unanitafuta nini kaka?
Hasad inakula moyo wa binadamu na kwako imejitokeza wazi.

Cambridge inakuchoma sana na inakula na kukukata maini.

Wewe ni wa kuepukwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu unanitafuta nini kaka?
Hasad inakula moyo wa binadamu na kwako imejitokeza wazi.

Cambridge inakuchoma sana na inakula na kukukata maini.

Wewe ni wa kuepukwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
pale anayejiita nguli wa historia ya tanganyika anapokimbia maswali![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom