"Mohamed Said, post: 22753614, member: 12431"]''Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walifahamiana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora. Chama hakiwezi kupinga ukweli kwamba Kasella Bantu alikuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waasisi wa TANU. Hali kadhalika chama hakiwezi, kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ‘’kuandika’’ ile katiba ya TANU. Kasella Bantu anakerwa sana na kupotoshwa kwa historia. Kila alipopata fursa kuanzia alipokuwa ngíambo uhamishoni na hata baada ya kurudi nyumbani kutoka uhamishoni, Kasella Bantu ameeleza kuhusu mambo haya mawili ya kihistoria, kuwa ‘’aliandika,’’ katiba ya TANU na ni mmoja wa waasisi wa TANU. Bantu kama waanzilishi wengine wengi anahisi kwamba mchango wake katika harakati za uhuru wa Tanganyika haujathaminiwa.''
''Jopo la wana-historia wa Chama Cha Mapinduzi waliopewa jukumu la kutafiti na kuandika historia rasmi ya TANU, hakuna hata sehemu moja waliyotaja jina la Abdulwahid katika kitabu kizima.Dhana inayojaribiwa kuenezwa katika kitabu kile ni kuwa kabla ya kutokea kwa Julius Nyerere mwezi Aprili, 1953, alipochaguliwa kuwa rais wa TAA, chama hicho hakikuwa na mwelekeo wowote wa siasa. Kitu cha ajabu ni kuwa kitabu hicho wala hakielezi huo urais wa TAA, Nyerere aliupataje au aliuchukua kutoka kwa kiongozi gani wa wakati ule. Kitendo hiki kimeondoa hadhi na heshima ya wazalendo wengi waliopigania nchi hii na halikadhalika kimeiondolea TAA heshima ya kuitwa chama cha siasa. Wanahistoria wazalendo pamoja na wanasiasa wa sasa hawataki kabisa kuipa TAA hadhi ya chama cha siasa. Kambona aliiita African Association chama cha majadiliano:
‘’Sasa inakaribia mwaka mmoja toka iundwe Tanganyika African National Union na katika kipindi hiki chama kimekua kikipata nguvu siku hadi siku, wakati mwingine chini ya upinzani mkubwa. Kama mnavyofahamu chama hiki ni badala ya Tanganyika African Union ambayo ilikuwa sawasawa na chama cha majadiliano.’’
Ulotu anaieleza TAA kuwa ilikuwa chama cha ustawi wa jamii. Wengine wameieleza TAA kama taasisi ya jamii: Nyerere (1976), halikadhalika Japhet na Seaton (1966). TAA wakati mwingine inaelezwa kuwa ilikuwa chama cha vuguvugu za upinzani dhidi ya ukoloni, lakini upinzani wake haukuwa dhahiri: Kaniki (1974), Nyerere (1953) aliieleza TAA kama chama cha vuguvugu la siasa lakini si za dhahiri. Julius Nyerere alipohutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, tarehe 7 Machi, 1955 alisema:
''Tanganyika African National Union kwa mtazamo mmoja ni chama kipya, lakini kwa mtazamo mwingine ni chama kikongwe. TANU imechukua nafasi ya Tanganyika African Association ambayo ilianzishwa mwaka 1929, kama chama cha kijamii. Tanganyika African National Union, chama kilichochukua nafasi ya African Association miezi kumi iliyopita ni chama kipya kwa maana ni chama cha siasa, wakati TAA ilikuwa chama cha siasa nusunusu.
Wasomi wengine wameishusha TAA kufikia daraja la kuwa klabu: Mwenegoha (1976) anaandika: ëMwaka 1954, baada ya miaka ishirini na tano ya kutoweza kufanya lolote, Nyerere aliigeuza TAA kutola chama cha kijamii kuwa chama cha siasa chenye kuogopwa kilichoitwa Tanganyika African National Unioní.
Abdulwahid ambae alitoa mchango wa pekee katika kuunda TANU alikuwa anaiona TAA kama chama cha siasa (1951). Katika kundi la waandishi na wasomi walioandika kuhusu African Association kisha wakabadili mawazo yao kuhusu nini hasa chama kile kilikuwa, ni Nyerere na Hatch ndiyo waliobadili misimamo yao ya awali. Nyerere alipoandika barua kwa Gavana wa Tanganyika, Edward Twining tarehe 10 Agosti, 1953 alieleza kuwa TAA ni chama cha siasa. Lakini baadae alibadili msimamo na kusema kuwa TAA kilikuwa chama cha starehe. Kauli hii ilitawala hotuba za Nyerere na maandishi yake kwa kipindi kirefu. Katika miaka ya hivi karibuni amesikika akisema kuwa TAA kilikuwa ëchama cha siasa kisichokuwa na katiba ya siasaí. Hatch (1976) ameieleza TAA kama chama cha starehe sehemu moja na chama cha siasa sehemu nyingine. John Kabudi ameieleza African Association kama ëchama cha watu binafsi wananchi kilichokuwa na mwelekeo wa kitaifa.''
Joseph Kimalando kwa Hon. General Secretary, 9 Septemba, 1953. ‘’Government Circular on Membership of Political Associations.’’ Maktaba ya CCM. File 168 Folio 2.
Pacha anayo muhtasari ya ule mkutano mkuu wa Julai, 1954 lakini hakuwa na rasimu ya katiba ambayo haikuweza kupatikana Maktaba ya CCM Dodoma. Bukoba ilipokea rasimu hiyo, angalia barua ya M. Lugazia kwa katibu Tawi la Bukoba DC/ HQ/ LP/ 897 Mei, 1854. Felio 16 TANU 16 lakini rasimu ya katiba iliyotajwa humo haimo ndani ya barua hiyo.
M. Lugazia kwa katibu Tawi la Bukoba DC/HQ/BK/LP/897 May, 1954 (tarehe haikutolewa) TANU folio 16 Party Archives, Dodoma. Rasimu ya katiba iliyotajwa hapo imekosekana.
Uongozi wa TAA haukurasimu katiba mpya. Katiba ya TANU ilinukuliwa neno kwa neno kutoka Convention People's Party (CPP) ya Kwame Nkrumah, kwa kutia TANU mahali pa CPP. Maelezo kutoka kwa Tewa Said Tewa.