Kumbukumbu ya kuzama kwa MV Bukoba tarehe 21 May, 1996

 
Mungu azilaze pema roho za marehemu na wale waliopoteza ndugu zao Mungu awatie faraja.
Tuliobaki tukumbuke kuwa, uzembe ndio chanzo kikubwa cha ajari nyingi, na meli hiyo ilizama kwa sababu za uzembe na pengine rushwa na magendo!
Pamoja na tukio hilo baya sana, bado uzembe umeendelea kuonekana, mfano kule Zanziba tumeshuhudia ajari za meli zilizoaababishwa na uzembe ulele! Mungu atuponye Watanzania!
 
Ajali ya MV bukoba haikutoa funzo kwa mamlaka husika japo ajali haina kinga lakini ya MV spice iliozama mkondo wa Nungwi ni somo kubwa sana lililoacha maumivu ya hali ya juu hadi sasa! Udhaifu wa uokozi na utoaji taarifa mapema ni vitu ambavyo vinge kopiwa toka mv bukoba lkn ndio hivyo tena yale yale
 

Duh🙁 mwaka 96 cm za mkononi zilikuwepo mkuu? Au unamaanisha cm ya namna gn?
 

Marekani ni mshenzi sana, ajali zote zinazotokea ktk nchi yake huwa nafurahia mno maana kapoteza innocent people wengi mno, yaani natamani vile vigorofa viwili vilivobakia pale new york vipitiwe na vibaraka wao isis or Alqaida!!
 
Wapo wanaodai ilikua kafara ya mkapa ctaki kuamin juu ya hilo
na kumbuka nilimpoteza mjomba Wang Aliamin abubakary kachwamba...mungu amulaze mahali pema peponi.. ameen

Poleni sana mkuu, na pole kwa wote waliofiwa...hakuna atayebakia wote njia moja
 

Sio kwa sababu ya umasikini jombaa... titanic na concordia pia ni kwa sababu ya umasikini?
 
naumia sn nchi yngu,yan tumesahau kbsaaa! juz ile gari kigamboni tumehenya kweli kuitoa,seuse madudu makubwa( meli) tutaeza kuokoa watu kwa wkt? tupotupo tu.
 
Haya mambo buana achana nayo, Serikali imelala doro wamemuachia Matata.
Nae Flaviana leo katangaza kuwa mwaka huu ndiyo mwisho kujishughulisha na kumbukumbu hiyo na kuomba wadau wengine wajitokeze kuchukua kijiti chake.
 
Duh🙁 mwaka 96 cm za mkononi zilikuwepo mkuu? Au unamaanisha cm ya namna gn?
Kwa mwaka huo 1996 simu za mkononi tayari zilikuwepo na huduma zake zilikuwa zinatolewa na kampuni ya Mobitel. Kipindi hicho ni watu wachache tena wenye uwezo ndiyo waliweza kumiliki simu hizo. Binafsi kwa mkoa wa Mwanza na kwa mara ya kwanza niliona mtu ninaemfahamu akimiliki simu ya mkononi mwishoni mwa 1996. Baadae na mimi nikadunduliza na kununua ya kwangu mwanzoni mwa mwaka 1998.

Kwa kuangalia hizo facts hapo juu utaona kwamba kuna uwezekano wa huyo jamaa kuwasiliana na ndugu zake kwa simu ya mkononi akiwa ndani ya meli wakati wa ajali hiyo May 1996.
 
Namkumbuka dada Zaynab Mussa, ilikuwa akirudi likizo kutoka Rugambwa ss tunapiga nae prac za kemia kibaha sec, ile anamaliza pepa anarudi toka Bukoba anazama na mv Bukoba!dah nililia sana coz nilikuwa nampenda sana
 
Nae Flaviana leo katangaza kuwa mwaka huu ndiyo mwisho kujishughulisha na kumbukumbu hiyo na kuomba wadau wengine wajitokeze kuchukua kijiti chake.
Nimeshangaa kweli baada ya kujua ni mtu na si wizara ndio inaratibu maazimisho haya
 
0



Mkuu nashkuru sana nilikuwa sijui hilo,
 
Nilikuwa kwenye kumbukumbu kwana walio nusurika na hiyo ajali walikuwa wanasimulia kwa uchungu sana na tena hii ajali ilipoteza watu wengi sana wa bukoba katika marafiki wangu watano wahaya unakuta wanne hii ajali iliwagusa kama siyo baba na mama kaka ndugu wa karibu
 
Tar 21.5.1996 watanzania na watu wengine hawataisahau ikiwa walipoteza wapendwa wao kwenye ajali ya meli ya MV bukoba, je tumejifunza nini? Kuna marekebisho yoyote yanafanywa au tahadhari kuchukuliwa yasitokee maafa kama haya kwenye vyombo vyetu vya usafiri au tunangoja maafa yatokee tena ndio tuanze kujipanga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…