Kumbukumbu ya miaka 16 tangu kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Swali hili ni kufuatia hali halisi iliyopo CCM, kama watu kama Kingunge Ngombale Mwiru na Juma Mwapachu, wameamua kuachana na CCM, Jee Nyerere angebaki?!.
Pasco

This is an insult,,,,Nyerere kamwe hawezi kulinganishwa na hawa uliowataja hapo. Unless utuletee wakina Hamza Mwapachu ama Oscar Kambona ama Dossa Aziz...hawa wa level hii ndugu.

Halafu yule mzee angelikuwa hai sijui fate ya "mtu wetu huyu" ingelikuwaje by now!!!!!
 

Si kulikimbia tatizo, ila yapo matatizo mengine huwezi kuyatatua ukiwa ndani. Lazima utoke nje ndio uyatatue, somehow. ni sawa na kusukuma gari au kuzima moto.
 
Aliishaikataa ccm tangu akiwa hai. Naamini anaikataa hata huko aliko
 

Kingunge halinganishwi na Mwalimu Nyerere. Tayari Kingunge alishanasa kwenye mtego wa mafisadi. Hata hivyo, jambo moja nalijua kuwa hakika, Edo asingethubutu kugombea urais kama mwl angelikuwepo
 
Mbona unauliza swali kinyume? Uliza je Kingunge angehama CCM? Na je Lowassa angegombea urais?
 
Kingunge halinganishwi na Mwalimu Nyerere. Tayari Kingunge alishanasa kwenye mtego wa mafisadi. Hata hivyo, jambo moja nalijua kuwa hakika, Edo asingethubutu kugombea urais kama mwl angelikuwepo
Kingunge amejidhalilisha sana, aina yake ndiyo wale Mwalimu alikuwa anawaambia wasiwe wajinga kama Lowassa.
 
MIAKA 16 BILA MWALIMU… NANI ATAMRITHI?
Ni mwaka wa 16 tangu alipotutoka Baba wa Taifa letu Mwl. Julius Kambarage Nyerere 14/10/1999. Je ni nani atamrithi Mwl. Nyerere baada ya uchaguzi?
· Mwalimu alichukia rushwa na kuikemea wazi wazi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikuwa anapenda sana kufanya kazi, alishiriki kilimo na hata ujenzi … nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alichukia mafisadi na kuwapinga wazi wazi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikuwa kiongozi msafi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu hakuwahi kujilimbikizia mali za umma… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikemea udini, ukabila na ukanda… nani atamrithi Mwalimu?
 

Mtetezi wetu na mrithi wa haya yote ni Dkt John MAGUFULI hili halina ushindani wowote Kwakuwa tumeshaona jinsi alivyoanza kufuata nyayo katika katika wizara mbalimbali....
 
HATUFAI
Mtu yoyote,anayeonekana anapenda sana kwenda ikulu,hata yupo tayari kununua kura kufika ikulu ni wa kukwepa kama ukomaa:Mwl 1922-1999
 
Na ndio maana nasema, Magufuli ni nyerere wa pili
 
 


Tuwe makini na hawa wanaoitafuta IKULU kwa kuhonga, kudanganya na kuhangaika kuhama hama vyama mradi tu waipate IKULU.
 
 
Huyu jamaa hafai kuwa RAIS
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…