Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba usiulize mambo ya zamani,Hivi ulipata wapi ujasiri wa kumuuliza nyerere wa pili masuala ya kikatiba siku ile kwenye mkutano na waandishi wa habari?
Happy Nyerere Day!Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo
Happy Nyerere Day.
Paskali
Leo tarehe 14 October ni siku ya Nyerere Day, tumuenzi kwa kujikumbushe tuliwahi kusema nini, kumhusu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Wanabodi,
Leo tunaadhimisha miaka 16 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere, swali langu ni kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai hadi leo, jee angeendelea kuwepo CCM?!.
Niliwahi kupandisha uzi humu, kuelezea kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai hadi leo, angemuunga nani mkono, mode wakaufuta huo uzi, japo mimi kama mwana jf, siruhusiwi kuingilia mamlaka ya mode kuifunga thread yoyote, ila pia tufike mahali, mwanajf yoyote ambaye ni thread starter, awe na the right to information kuwa thread yako imefutwa na kuelezwa sababu za ni kwa nini imefutwa!.
Swali hili ni kufuatia hali halisi iliyopo CCM, kama watu kama Kingunge Ngombale Mwiru na Juma Mwapachu, wameamua kuachana na CCM, Jee Nyerere angebaki?!.
Pasco
Mwakani 2025 tutamchagua Nyerere MwanamkeNaomba usiulize mambo ya zamani,
Na kwa vile jana ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.
Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.
Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
Jf,
Mwalimu Nyerere alitutoka siku kama ya leo, RIP.
Leo tunamkumbuka kwa mambo meeeengi sana ma hasa wakati tukielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais wabunge na madiwani.
Machache makubwa ni kama yafuatayo;
1) Alikemea sana rushwa na ufisadi.
2) Alikemea matajiri kuendesha nchi.
3) Alisema waziwazi ikulu sio pango la walanguzi na wafanyabiashara. Wafanyabiashara wanataka kwenda ikulu kufanya nini.?
4) Alimkataa waziwazi LOWASA na kumkemea kuwa hana maadili ana harufu ya rushwa, na hivyo ajitenge kabisa na uongozi wa juu wa nchi.
5) Alijitoa maisha yake yote kwa ajili ya wananchi. Hata familia yake haikufaidika na chochote.
6) Alisema mgombea urais ambae ni mkabila , mdini au mbaguzi wa aina yoyote hafai kupewa uongozi
LEO HII TUTAFAKARI KWA HAYA MACHACHE NA KAMA KUNA MENGINE ONGEZENI
Cc. Lizabon, mzee mwanakijiji