Kumbukumbu ya miaka 16 tangu kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Kumbukumbu ya miaka 16 tangu kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Mkuu iko hivi;

Ukawa watakuwa kwenye kampeni kama kawaida yao na wata-play zile clip za Mwal. Walizoedit kitoka kwenye hotuba zake...
Mfano;

"" watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata..wasipoyapata ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm""


"" ccm sio Baba yangu"


"Mpinzani wa kweli atatoka ndani ya ccm""


"" chama kitakacho puuza maamudhi ya wananchi kitalia kilio na kikakosa mtu wa kukipangusa machozi ""



Zile clip za RUSHWA na UDINI hazitaguswa.....

Vice versa yake Ccm wanazigusa?
 
Mwalimu alitumia muda mwingi kukemea RUSHWA na UFISADI. Leo vyama vyenye muungano kivuli UKAWA vilivyoanzishwa kwa busara za Mwl ndio makuwadi wa RUSHWA NA UFISADI.

Napenda kusahihisha hiyo historia ya Mwalimu. Mwalimu alikuwa waziri mkuu wa Tanganyika kuanzia Desemba 09 1961 hadi Januari 1962 alipoacha wadhifa wa uwaziri mkuu na kumwachia ndg Rashid M.Kawawa. Kufuattia uchaguzi wa mosi Nov.1962 ?Mwalimu aluchaguliwa kuwa rais wa Tanganyika kufuatia luapishwa kwake 09 Desemba 1962 na Tanganyika kuwa jamhuri siku hiyihiyo. Pia Mwalimu alikuwa hatembei kwenda shuleni bali alikuwa mwanafunzi wa bweni alikuwa akitembea siku ambazo shule imefungwa au kufunguliwa kadhalika ni umvali wa kilomita 50 kati ya Butiama na Mwisenge na si Km 30. Watoto wa Nyerere Burito walikuwa 27 na sio 26
 
Lowassa hafai kabisa ndo mana mikutano yako wanaudhuria watu 7
 

Attachments

  • 1444838262262.jpg
    1444838262262.jpg
    46.5 KB · Views: 116
Aliishaikataa ccm tangu akiwa hai. Naamini anaikataa hata huko aliko[

Si kweli, ninachokumbuka ni kwamba alikataa viongozi wabovu, wasio na maadili. Na pia alikataa matendo ya ovyo yanayokwenda nje ya misingi ya uongozi, chama ni kama gari ambayo unaweza kubadili mfumo wa kutumia mafuta ukatumia gesi mzee

MIAKA 16 BILA MWALIMU… NANI ATAMRITHI?
Ni mwaka wa 16 tangu alipotutoka Baba wa Taifa letu Mwl. Julius Kambarage Nyerere 14/10/1999. Je ni nani atamrithi Mwl. Nyerere baada ya uchaguzi?
· Mwalimu alichukia rushwa na kuikemea wazi wazi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikuwa anapenda sana kufanya kazi, alishiriki kilimo na hata ujenzi … nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alichukia mafisadi na kuwapinga wazi wazi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikuwa kiongozi msafi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu hakuwahi kujilimbikizia mali za umma… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikemea udini, ukabila na ukanda… nani atamrithi Mwalimu?

Magufuli tu
 
Mwalimu alikua ni mtu mhimu sana alikemea ufisadi alikemea rushwa alikemea ukabila lakini haitosi alikua anachukia sana umasikini lakini tizama leo baadhi ya viongozi waliohamia vyama pinzani wamekua wakilitafuna hili taifa na kudai kujisafisha mwl bora ungekuwepo
 
MIAKA 16 BILA MWALIMU… NANI ATAMRITHI?
Ni mwaka wa 16 tangu alipotutoka Baba wa Taifa letu Mwl. Julius Kambarage Nyerere 14/10/1999. Je ni nani atamrithi Mwl. Nyerere baada ya uchaguzi?
· Mwalimu alichukia rushwa na kuikemea wazi wazi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikuwa anapenda sana kufanya kazi, alishiriki kilimo na hata ujenzi … nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alichukia mafisadi na kuwapinga wazi wazi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikuwa kiongozi msafi… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu hakuwahi kujilimbikizia mali za umma… nani atamrithi Mwalimu?
· Mwalimu alikemea udini, ukabila na ukanda… nani atamrithi Mwalimu?
Dr John Pombe Magufuli
 
Mwl nyerere
1.alikua anachukia rushwa
2.alikua anachukia umasikini
3.alikua anachukia ufisadi
4.alikua anachukia viongozi wasio na maadili mema
Haya yote yalikua ni mambo ambayo mwalimu alicgukia na ilifikia mda hata kuwakata baadhi ya viongozi walioonekana wanatumia vibaya madaraka Tizama leo baadhi ya viongozi waliokatwa mwaka 1995 na mwalimu nyerere wameamua kudiriki kugimbea nyadhifa za juu wakati hawana sifa za kuwa viongozi,wamejawa na tamaa na uchu wa madaraka
mungu inusuru nchi yetu tupate kiongozi bora magufuli ambaye ataliendesha taifa letu vizuri na kutufikisha mbali kimaendeleo
 
Daah napata shida sana kukufikiria ila labda umecomment Kwa kutumia akili za Mr Zero(Sumaye)
mda mwingine unapokutana na vijana kama hao usipate tabu anakua hatumii akili yake ya kawaida bali anaendeshwa na akili za ki CDM ambazo hazifikiri wala kutafakari ukweli wa mambo
 
Ikiwa leo ni siku tunakumbuka kifo cha Baba wa Taifa hili hatuna budi kumuenzi kwa kuyafuata yale aliyokuwa akiyapigania

1. kupambana na Rushwa na Ufisadi (Uhusani kwenye uchaguzi tuwakatae MAFISADI)

2.Tupige vita UDINI (Hususani kwenye UCHAGUZI, Kiongozi mwenye nasba na Udini tumkatae)

3. Tuepuke UKABILA (hUSUSANI KWENYE UCHAGUZI, Kiongozi mwenye nasaba na ukabula tumuogope kama ukoma

4.Tusiwape nafasi genge la wala MATAJIRI (MAFISADI) Kutawala nchi yetu
View attachment 298685
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, 13 Aprili 1922 -na alipoteza maisha London, Uingereza, 14 Oktoba 1999)

Alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "baba wa taifa". Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule.

Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha.

Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu."

Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muungano wake na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.

Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.
View attachment 298691
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Kumbukumbu ya Hayati Baba Wa Taifa.

Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
View attachment 298686
Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945. Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).

Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.
View attachment 298687
Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.

Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza. Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi. Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi. Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.
View attachment 298688
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.
View attachment 298689
Mwalimu alizikwa nyumbani kwake Mwitongo katika Kijiji cha Butiama karibu na makaburi ya wazazi wake na mahali alipozaliwa na familia ya Mwalimu ilisema aliagiza azikiwe hapo.

REST IN PEACE BABA WA TAIFA

Nyerere alisema wananchi wa tz ni maskini, pamoja na Lowassa
 
Mwl Nyerere alitufunza mengi, ila kuna jambo moja muhimu sana alisahau kufanya.

Aligatua mamlaka kutoka kwa wananchi akakipa chama (chama kushika hatamu). Yeye alimudu kofia mbili kwa wakati mmoja (kuwa m/kiti wa chama-dola akiwa pia rais wa nchi) lakini waliompokea kijiti hilo limewashinda.

Bahati mbaya wakati anang'atuka hakuyarejesha mamlaka kwa wananchi, na hili ndilo linalotugharimu mpaka leo hii.
 
Nyerere ni Mtu wakwanza alie Tawala tanganyika na Tanzania kwa wakati mrefu sana na huku alipo amuwa kunyatuka ilionekana kwamba alikuwa Bado ana Tawala ndani ya chama na serekali, mfano ni nyerere peke yake alie amuwa kwamba lowasa asigombei uraisi mwaka wa 1995, ni nyerere pekee alie mleta mkapa kuwa Raisi wa Tanzania! Sasa hii ina Maana huyu jamaa kiundani alikuwa na sehemu ya udikteta fulani hivi, na wakati wote wa utawala wa nyerere nchi hii ilikuwa ndio ya mwisho kiumaskini pamoja na kukaa kwake muda mrefu serekalini bado hakuna hatuwa iliyo pikwa kima endeleo, wakati wa nyerere ufukara ulikuwa wa kupitiliza. Na aina ya uchumi wake ulikuwa niwaku nyanyasa Raia na kuendeleza umasikini kwa Raia wa nchi hii, Nakumbuka mimi baba yangu aliwai kufungwa katika kata ya ilagala mkoani kigoma kwa kosa la kukataa kwenda kulima shamba la serekali(pamba) na wakati huo baba yangu alikuwa mgonjwa ambaye haruhusiwi kufanya kazi za nguvu na madaktari wali mpa kibali cha kuepuka kufanya kazi za nguvu Lakini kijiji cha Karago kiliona kama alitowa hongo ili asifanyi kazi za serekali! Wakati huo ni wakati ambao sheria zake zilikuwa na nguvu na watu walikuwa watiifu sana kuliko sasa ila kiukweli alichangia pakubwa kubwetesha akili za watanzania na ndio hii hali inayo endelea hadi sasa kwamba watanzania walio wengi ni wajinga
 
Mwl Nyerere alitufunza mengi, ila kuna jambo moja muhimu sana alisahau kufanya.

Aligatua mamlaka kutoka kwa wananchi akakipa chama (chama kushika hatamu). Yeye alimudu kofia mbili kwa wakati mmoja (kuwa m/kiti wa chama-dola akiwa pia rais wa nchi) lakini waliompokea kijiti hilo limewashinda.

Bahati mbaya wakati anang'atuka hakuyarejesha mamlaka kwa wananchi, na hili ndilo linalotugharimu mpaka leo hii.

wakitenganisha kofia hizi mbili ccm kitakuwa chama changu.
kipindi cha bwana mkubwa huyu waliua eidha kwa kujua au la vyama vya ushirika kitu kilichokua nyenzo muhimu kumuinua mnyonge, kosa ambalo mpaka sasa halija rekebishwa.
 
Wanabodi,

Leo tunaadhimisha miaka 16 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere, swali langu ni kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai hadi leo, jee angeendelea kuwepo CCM?!.

Niliwahi kupandisha uzi humu, kuelezea kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai hadi leo, angemuunga nani mkono, mode wakaufuta huo uzi, japo mimi kama mwana jf, siruhusiwi kuingilia mamlaka ya mode kuifunga thread yoyote, ila pia tufike mahali, mwanajf yoyote ambaye ni thread starter, awe na the right to information kuwa thread yako imefutwa na kuelezwa sababu za ni kwa nini imefutwa!.

Swali hili ni kufuatia hali halisi iliyopo CCM, kama watu kama Kingunge Ngombale Mwiru na Juma Mwapachu, wameamua kuachana na CCM, Jee Nyerere angebaki?!.

Pasco
Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
Hivi ulipata wapi ujasiri wa kumuuliza nyerere wa pili masuala ya kikatiba siku ile kwenye mkutano na waandishi wa habari?
 
Back
Top Bottom