Kumbukumbu ya miaka 16 tangu kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere


Vice versa yake Ccm wanazigusa?
 
 
Lowassa hafai kabisa ndo mana mikutano yako wanaudhuria watu 7
 

Attachments

  • 1444838262262.jpg
    46.5 KB · Views: 116
Tarehe 25 lazima nikamtende haki baba wa taifa kwa kumkata fisadi lowasa
 
 
Mwalimu alikua ni mtu mhimu sana alikemea ufisadi alikemea rushwa alikemea ukabila lakini haitosi alikua anachukia sana umasikini lakini tizama leo baadhi ya viongozi waliohamia vyama pinzani wamekua wakilitafuna hili taifa na kudai kujisafisha mwl bora ungekuwepo
 
Dr John Pombe Magufuli
 
Mwl nyerere
1.alikua anachukia rushwa
2.alikua anachukia umasikini
3.alikua anachukia ufisadi
4.alikua anachukia viongozi wasio na maadili mema
Haya yote yalikua ni mambo ambayo mwalimu alicgukia na ilifikia mda hata kuwakata baadhi ya viongozi walioonekana wanatumia vibaya madaraka Tizama leo baadhi ya viongozi waliokatwa mwaka 1995 na mwalimu nyerere wameamua kudiriki kugimbea nyadhifa za juu wakati hawana sifa za kuwa viongozi,wamejawa na tamaa na uchu wa madaraka
mungu inusuru nchi yetu tupate kiongozi bora magufuli ambaye ataliendesha taifa letu vizuri na kutufikisha mbali kimaendeleo
 
Daah napata shida sana kukufikiria ila labda umecomment Kwa kutumia akili za Mr Zero(Sumaye)
mda mwingine unapokutana na vijana kama hao usipate tabu anakua hatumii akili yake ya kawaida bali anaendeshwa na akili za ki CDM ambazo hazifikiri wala kutafakari ukweli wa mambo
 

Nyerere alisema wananchi wa tz ni maskini, pamoja na Lowassa
 
Mwl Nyerere alitufunza mengi, ila kuna jambo moja muhimu sana alisahau kufanya.

Aligatua mamlaka kutoka kwa wananchi akakipa chama (chama kushika hatamu). Yeye alimudu kofia mbili kwa wakati mmoja (kuwa m/kiti wa chama-dola akiwa pia rais wa nchi) lakini waliompokea kijiti hilo limewashinda.

Bahati mbaya wakati anang'atuka hakuyarejesha mamlaka kwa wananchi, na hili ndilo linalotugharimu mpaka leo hii.
 
Nyerere ni Mtu wakwanza alie Tawala tanganyika na Tanzania kwa wakati mrefu sana na huku alipo amuwa kunyatuka ilionekana kwamba alikuwa Bado ana Tawala ndani ya chama na serekali, mfano ni nyerere peke yake alie amuwa kwamba lowasa asigombei uraisi mwaka wa 1995, ni nyerere pekee alie mleta mkapa kuwa Raisi wa Tanzania! Sasa hii ina Maana huyu jamaa kiundani alikuwa na sehemu ya udikteta fulani hivi, na wakati wote wa utawala wa nyerere nchi hii ilikuwa ndio ya mwisho kiumaskini pamoja na kukaa kwake muda mrefu serekalini bado hakuna hatuwa iliyo pikwa kima endeleo, wakati wa nyerere ufukara ulikuwa wa kupitiliza. Na aina ya uchumi wake ulikuwa niwaku nyanyasa Raia na kuendeleza umasikini kwa Raia wa nchi hii, Nakumbuka mimi baba yangu aliwai kufungwa katika kata ya ilagala mkoani kigoma kwa kosa la kukataa kwenda kulima shamba la serekali(pamba) na wakati huo baba yangu alikuwa mgonjwa ambaye haruhusiwi kufanya kazi za nguvu na madaktari wali mpa kibali cha kuepuka kufanya kazi za nguvu Lakini kijiji cha Karago kiliona kama alitowa hongo ili asifanyi kazi za serekali! Wakati huo ni wakati ambao sheria zake zilikuwa na nguvu na watu walikuwa watiifu sana kuliko sasa ila kiukweli alichangia pakubwa kubwetesha akili za watanzania na ndio hii hali inayo endelea hadi sasa kwamba watanzania walio wengi ni wajinga
 

wakitenganisha kofia hizi mbili ccm kitakuwa chama changu.
kipindi cha bwana mkubwa huyu waliua eidha kwa kujua au la vyama vya ushirika kitu kilichokua nyenzo muhimu kumuinua mnyonge, kosa ambalo mpaka sasa halija rekebishwa.
 
Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Hivi ulipata wapi ujasiri wa kumuuliza nyerere wa pili masuala ya kikatiba siku ile kwenye mkutano na waandishi wa habari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…