Kumchokoza Tundu Lissu ni sawa na kuwasha moto nyikani

Kumchokoza Tundu Lissu ni sawa na kuwasha moto nyikani

Mtu kawajibu kua akirudi anaenda kuwakabili waliomwandikia wito hadi hapo hamjiulizi tu Lissu hana cha kupoteza kwenye siasa za nchi hii kwa aliyoyapitia, utamfanyia tena nini ili kumtisha?
Lissu haogopi tena shaba
 
Angekuwepo mchungaji Mtikila hili la bandari waarabu wangekimbia nchi.
 
Nilicho gundua Janga kubwa nchi hii sio Lissu wala upinzani bali ni chama cha kijani, nafikiri kuondikana na matatizo yote haya Tanzania inapitia ni kuondoa kwanza hawa watu, otherwise ni kupoteza muda, hata mkiwekeza kila kitu hadi ikulu as long as Kijani wapo mtaambulia hasara.

Hivi mtu anae toa maoni kwa ajiri ya kuboresha ni adui wa taifa hili kweli? Kama kweli dhumuni ni kuwekeza, huu muda mnao tumia nguvu na police kuita watu kama mngetunia kuchukua maoni ya watalaam na kuyaingiza kwenye mkataba ule na mkaendelea na mazungumzo na DP word mna pungukiwa na nini? watu wana toa maoni for free ili serikali ifanye vizuri wote tufaidike .

Rais mjanja na mpenda maendeleo angekuwa ameunda team ndogo akaleta watalaam wa pande zote kupitia huo mkataba na kuja kitu kizuri zaidi , sasa mambo ya police ni ishara tosha kuwa huo mkataba kweli ni mbovu ambao mmeingia kima gumashi ila mnatumia nguvu kuficha ukweli.

Ndio maana hili ni taifa kubwa lakini halina maendeleo miaka yote , lime dumaa kwa sababu hamtaki mawazo mapya, hakuna hata sector au wizard inayofanya vizuri Tanzania, tuna bahatisha kila jambo.
 
Lissu ni kichaa anayevaa suti, tai na miwani. Ni kichaa mwenye kuheshimiwa, huwa unamtambua mpaka akianza kufungua mdomo.

Heshima aliyopewa na Mheshimiwa Rais ni hali ya juu sana, kwa mtu mwenye chembechembe za ubinadamu alitakiwa akiheshimu kiti cha urais hata kama anaona SSH hana hadhi ya kuheshimiwa.
Ukiteswa sana kama LISSU mwisho inakuwa sugu, mvua ya risasi kama unaua nyati halafu utishwe Tena.
 
Samia amekuwa mzazi mwema sana kwa Lissu, alimtembelea hospitalini Kenya.

Akakutana nae Brussels Ubelgiji na akahakikisha analipwa pesa zote alizoidai serikali.

Amekuwa Mama mwema sana kwa CDM mpaka akashiriki mkutano wao mkuu, kitu ambacho hakuna rais aliyemtangulia aliyeweza kuthubutu kukifanya.

Lissu yote haya hayaoni, huyu ni kichaa anayevaa suti na tai na kukaa viti vya mbele kwenye ghafla mbalimbali. Huwezi kumtambua kwa kumuona tu ni mpaka afungue kinywa chake ndio utamjua vizuri kwamba kichwani pameharibiwa na zile risasi za Dodoma.
Yaani utoe shukrani kwa waliokumiminia mvua ya risasi?
 
Back
Top Bottom