Kumekua na ongezeko kubwa la Wanawake wenye msongo wa mawazo

Ni kweli wanawake wanahitaji faraja ya hali ya juu sana. Kwanza wapo wengi kuliko sisi alafu mashoga nao wamechukua nafasi yao sikuhizi. Jumlisha vikoba, hedhi kila mwezi, wanyonge maana hawana nguvu kuliko sisi
 
Hebu jaribu kuvaa viatu vyao, una watoto wawili halafu huna kazi ya kueleweka. Ila wanawake nao bana, unaruhusu vipi watoto wawili na hujaolewa?
Mwingine anaolewa anaachika na hapo hapo aliolewa akiwa single mom anaachika ana mtoto mwingine! Wengine wazaa hawawezi kuvumilia dharau za kuonekana hajazaa siunajua jamii yetu ilivyo huku uswahilini
 
Mkuu sijui “utafiti” wako umeufanyia wapi lakini jinsia inayo ongoza kwa stress za kimaisha ni WANAUME na sio wanawake

Mkuu mwanaume ukikwama na maisha mzigo anaoubeba wa familia na ndugu anaweza kutembea anaongea peke yake barabarani..... acha kabisa
 
Kweli nakubaliana nawewe yaani wenzetu ke uwezo wao wa kupunguza au kuovercome stress ni mdogo ndio maana wanapoteana mapema
 
Hili la wanaume kua na mzigo wanaoubeba kwenye familia na ukoo kusaidia watoto, ndugu, jamaa na marafiki sio kwamba halipo ila nitakuja kulielezea ni jinsi gani wanaume wana msongo wa mawazo ila wanaweza kuishi na kukabiriana na huo msongo wa mawazo tofauti na jinsi ilivyo kwa wanawake walio wengi. Ingiwa unapozungumzia mzigo lazima uangalie pande zote mbili yaan wanaume na wanawake kila mmoja ana nafasi yake kwa namna yake.

Nikituulia nitakuja kueleza kwanini wanaume wanaishi na msongo wa mawazo ila hawaonyeshi km wana msongo wa mawazo na huwezi jua km ana msongo wa mawazo tofauti na ilivyo kwa mwanamke. Mwanamke akiwa na msongo wa mawazo utajua na lazima atakuonyesha aidha kwa maneno, kwa vitendo au kwa ishara.
 
Duh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…