Kumekucha: Baraza la Mawaziri kivuli - Mbatia out


Paskali ww ni mwanahabari na mchambuzi nguli, ila huku kwenye siasa ushauri wako sio wa kuchukuliwa maanani. Ww ni mmoja ya watu waliokuwa wanampigia debe Lowassa kwa nguvu zao zote. Ni kweli umoja ni kitu kizuri, lakini kuwa na umoja kwenye mazingira haya tunayoyaona ni wendawazimu. Mimi ni mmoja kati ya watu tuliokuwa hatuamini katika umoja wa vyama vya upinzani, hasa kuachiana viti vya uchaguzi. Nadhani matokeo halisi ya muungano wa vyama sasa yako wazi peupe. Ni vizuri kila chama kikasimamisha mgombea wake na kipate stahiki yake. Cha muhimu kupatikane tume huru ya uchaguzi. Ni bora cdm wapate hata viti viwili vya ubunge lakini vya uhakika, kuliko vya ushirika wa mashaka.
 
Hivi,Hawa mawaziri vivuli Kuna malipo ya ziada wanayolipwa?
Hivi kuwa waziri kivuli kwani kuna malipo?
KUB ni Waziri Mkuu kivuli, anapaswa kupewa sehemu za marupurupu kama ya PM ikiwemo
  1. Ofisi yenye wafanyakazi na wahudumu
  2. Nyumba ya serikali yenye hadhi ya PM
  3. Watumishi wa hiyo nyumba akiwemo mpishi, Mtunza nyumba, Walinzi
  4. Gari na dereva, mafuta
  5. Mlinzi body guard
  6. Msaidizi
  7. Allowances
  8. Waziri Mkuu akisafiri safari za kiserikali anapaswa awepo
Vyote hivi vinagharimiwa na serikali.
Sasa jana huku kwetu vinafanyika au la sijui.

Mawaziri vivuli nao wanatakiwa kupewa marupurupu kama ya mawaziri wa ksmili ila wao ni a little bit less.
P
 
Kweli upinzani Tanzania ni upuuzi mtupu. Kweli hivi ndio vyama vinavyotaka kuongoza nchi. CCM haina mpinzani watangoja sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ccm haina mpinzani maana haishindani kisiasa tena, bali inatumia vyombo vya dola kufanya siasa. Namna bora ya kushindana na ccm kwa sasa ni kuwa na vikundi vya kigaidi. Wakati wao wakituma vyombo vya dola kupiga mabomu mikutano ya wapinzani, na wao kwenye mikutano yao kuwe ni vikundi vya kigaidi vikijibu mapigo kwa mtindo huo huo. Kisha baada ya hapo kuwe na tume huru ya uchaguzi halafu uje utoe mrejesho
 
Naomba nikuulize, umewahi kuwa kiongozi wa darasa au familia??
 
Nimeangalia Hao Walioteuliwa Hakuna mtu calibre ya Mbatia...Mama Tanzania..upinzani Africa ni shida tupu.
 
Hizi si ishara nzuri hata kidogo, hivi ni Kwa nini huwa hatuna kawaida ya kusuruhishana! Mkakaa mezani mkazungumza Kwanza, baada ya hapo ndipo maamzi yafuate?

Wapinzani, kama kweli Tageti yenu ni kuchukua nchi, basi hamna budi kuongeza vikao, na kama itakuwa kila anayeona upungufu katikati ya safari, na badala yake aamue kunyoa au kusuka, basi hakuna mtakachoweza zaidi ya kila mmoja kutaka ulaji na misifa ya kijinga

Anapoondoka mmoja, wapili, wa tatu na wanne bado tu mnasema mko salama ni kufumbwa macho na akili Kwa Uongozi, huwezi kufurahia hata kidogo

Umoja ni nguvu
 

Hayo uliyotaja hapo juu yapo tu kisheria au kikanuni lakini hayafanyiki, na hayafanyiki kwa sababu cdm ndio chama cha upinzani, na Magufuli ana nongwa na chuki ya wazi dhidi ya cdm. Sasa unapoona Mbatia kakutana na Magufuli, kisha Mbatia kuanza hujuma za wazi dhidi ya cdm, unategemea nini? Hivi ni kwanini Paskali hukuanzisha uzi kumshauri Mbatia asubiri mpaka muda uishe, ndio afanye anayoyafanya? Au ushauri wako ni kwa ajili ya cdm tu?
 
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavuwa, you are very right, this is the final kick of a dying horse.
P
Mkuu, nikushauri tu ungeendelea kukaa kimya kama ulivyoahidi hasa ukizingatia lile bandiko lako la juzi kuhusu unapotaka kwenda.

Kwa mtazamo wangu, umeshapoteza ile identity yako ya kujiita hauna chama and all that, kwasababu dhamira yako ulishaionesha na inajulikana wapi unataka kwenda.

Hivyo basi, hiki ulichokiandika kwa mtazamo wangu, na wa wengine wanaojielewa, ni wewe kuendelea kujisafishia njia uweze kupokelewa vizuri huko ulipoamua kwenda (unless useme wazi lile bandiko lilikuwa fake, vinginevyo litabaki valid).

Kutokana na hilo hapo juu, usitegemee michango yako humu JF ikapokelewa kwa uzito uliokuwa nao hapo awali, coz now umeshaonesha mahaba yako yapo mtaa wa Lumumba, suala la kusubiri mpaka Pole Pole akupokee halina maana yoyote.

Unaleta habari ya wapinzani kugawana kura then CCM ishinde kirahisi, kwani ni lazima wapinzani wakigombea jimbo moja CCM ishinde? if that's the case, kwanini CCM wasiwe wanaweka wapinzani kila jimbo ili wao washinde kirahisi waache kutumia nguvu ya dola?!, ndio maana nimekushauri, sasa ni wakati wako wakukaa kimya.

Back to the topic; kuhusu kile Mbowe alichokifanya, huo ndio muendelezo wa ujasiri anaouonesha Mbowe, ameshafanya calculation zake, anajua jibu alilolipata, na hilo jibu kwa namna moja lazima liwe kwa manufaa ya Chadema, wewe Paskali na wenzio mnaendelea kuimba Chadema inakufa, huku mkijidanganya CCM inakubalika, wakati wewe Paskali mwenyewe kwenye lile bandiko lako la juzi una mpango wa kutenga mil. 100 ili umhonge mkurugenzi wa uchaguzi wapinzani waenguliwe, upite bila kupingwa.

Anyway, ni ushauri tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo la KUB walau nilikuwa najifahamu kwa upana huo,ila hao mawaziri wengine sikuwahi jua Kama nao Kuna marupurupu ya ziada.
 
Huwezi kumlazimisha asie na nia kukaa nae meza moja, ukifanya hivyo, jiandae ajione mjuaji/mkubwa zaidi yako; hivyo ili ku-maintain standard ya kiuongozi, kiongozi lazima afuate principles zinazowaongoza, ndicho Mbowe alichofanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ushauri wako ni mzuri, ila hauendani na hali halisi. Mbatia kakutana na Magufuli, kisha kesho yake kapewa favour ambazo wapinzani wa kweli hawapewi. Mara kapokea madiwani wa cdm, leo hii ndani ya muda mfupi, inaonekana wahama cdm wanahamia NCCR! Hapo unahitaji maelewano gani hapo? Kwanza ujue hivyo vyama havijaungana kisheria, bali kwa makubaliano ya mdomo, sasa unapoona jirani yako anabaka watoto wako hapo bado kuna ujirani wa kuulinda? Ushauri ujikite kwenye uhalisia, na sio kwenye hofu isiyo na maana.
 
Upumbavu nao ni sifa, nakupongeza kwa sifa hiyo.
Magufuli alishindwaje kuwavumilia aliowatumbua, wote walifanya makosa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chief wenda ukawa sahihi but politics now is the tougher game
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Tindo, that is selfishness!.
Politics is a science, political science, nimewashauri Chadema wafanye SWOT na PEST ya wabunge wao wote. Matokeo yakionyesha mfano Lema anakubalika Arusha as Lema, Selasini Rombo as Selasini, Sugu Mbeya as Sugu, Prof. J Mikumi as J wa Mitulinga, hawa jamaa watachaguliwa tena vyama vyovyote watakavyo simama. Hivyo wakihama Chadema, Chadema ikubali ikatae itapoteza jimbo hilo. Wakihamia CCM, then Chadema isimamishe watu kuwapinga, lakini wakihamia NCCR, then Chadema usisimamishe mtu, maana ikisimamisha, hii itakuwa ni vita vya panzi, furaha kwa kunguru, kura za opposition zita split na wote watakosa na CCM kuibuka mshindi kwa kura chache kama ameokota dodo chini ya muembe.

Ni bora warejee Bungeni as NCCR kuliko kukosa wote na CCM kutwaa viti vyote. Hata kama Chadema na NCCR hawapikiki chungu kimoja, lazima wafanya political managing Diversity zao and work together against a common enemy.
Kwa hapo ilipo Chadema is already done, the only way out kwa Chadema to keep existing is towards working together, otherwise Chadema will perish na opposition Tanzania will perish, Bunge lijalo kwa huku bara litakuwa ni Bunge la CCM and CCM only!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…