Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Naunga mkono hoja, Chadema pekee yao hawawezi na haitakuja kutokea wakaweza!. Sisi Tanzania tuna tatizo kubwa la kitu kinachoitwa "Managing The Political Diversity" from both parties, CCM na Wapinzani, hadi ndani ya mihimili Bunge, Serikali na Mahakama.
Kwa muda uliobakia, hata kama Chadema inajua NCCR imenunuliwa na CCM, hivyo itajitenga nao, na Wabunge wote wa CUF wanasubiria tuu Bunge livunjwe watur rasmi ACT Wazalendo, Chadema walipaswa wawavumilie tuu, sometimes its good kumvumilia adui yako ili usiwaudhi wale waliokuja kwako kwasababu ya huyo adui yako. Kura milioni 6 za Lowassa ile 2015 sio za wana Chadema pekee.
Kosa kubwa la Chadema kuelekea 2020 ni kujidhania kwenye kambi ya upinzani, Chadema bado ni determinant, it's not!. Kuendelea 2020, Chadema is a dying horse, hivyo kitendo kama hiki cha kuihodhi kambi rasmi ya upinzani Bungeni, it's like a final kick of a dying horse.
Ili upinzani uweze kuvuna mavuno yoyote ya maana 2020 kwanza lazima Chadema wakubali kugawana himaya yake kwa kukubali ku share na vyama vingine vya upinzani.
Kabla ya Bunge kuvunjwa, Chadema ambacho kwa sasa ndio chama kikuu cha upinzani, kifanye SWOT na PEST analysis kwa Wabunge wake wote, halafu ikubali matokeo, wabunge wote wa Chadema watakaojiunga CCM, Chadema ijihesabu hayo majimbo yamepotea unless wana CCM wenyewe ndio waipigie Chadema kura za chuki kutokubali wapinzani waja leo na kusimamishwa kugombea CCM.
Pili wabunge wote wa Chadema watakao hamia vyama vingine, Chadema ikubali to share them na wapinzani wengine kwa kutosimamisha wagombea wengine ili kila jimbo na kila kata mgombea wa CCM apambane na mpinzani mmoja tuu. Ikitokea jimbo lilikuwa Chadema kama Moshi Vijijini na Rombo, wabunge wake wwkahamia NCCR Mageuzi, Chadema ikubali matokeo. Ikisimamisha wagombea wapya, hii itakuwa ni vita vya panzi, furaha ya kunguru, wapinzani wata split kura zao, CCM atayatwaa majimbo ya upinzani kama ameokota dodo chini ya muembe.
Upinzani pamoja na tofauti zao za ndani, lazima wavumiliane by managing diversity kwa kushirikiana hivyo hivyo pamoja na tofauti zao, wasimame united and stand as one against a common enemy, vinginevyo kwa huku bara, tunarudi kuwa nchi ya chama kimoja CCM only and only CCM!.
P
Paskali ww ni mwanahabari na mchambuzi nguli, ila huku kwenye siasa ushauri wako sio wa kuchukuliwa maanani. Ww ni mmoja ya watu waliokuwa wanampigia debe Lowassa kwa nguvu zao zote. Ni kweli umoja ni kitu kizuri, lakini kuwa na umoja kwenye mazingira haya tunayoyaona ni wendawazimu. Mimi ni mmoja kati ya watu tuliokuwa hatuamini katika umoja wa vyama vya upinzani, hasa kuachiana viti vya uchaguzi. Nadhani matokeo halisi ya muungano wa vyama sasa yako wazi peupe. Ni vizuri kila chama kikasimamisha mgombea wake na kipate stahiki yake. Cha muhimu kupatikane tume huru ya uchaguzi. Ni bora cdm wapate hata viti viwili vya ubunge lakini vya uhakika, kuliko vya ushirika wa mashaka.