n-propanol
JF-Expert Member
- Apr 7, 2019
- 5,349
- 7,000
Wizi ni tabia za kiume?. Mbona siku hizi kuna wamama wezi wengi tu.Wanawake wengine wana tabia za kiume!💔
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wizi ni tabia za kiume?. Mbona siku hizi kuna wamama wezi wengi tu.Wanawake wengine wana tabia za kiume!💔
Pesa tamu lakini😀Kinachoonekana rushwa ilinoga, akaona ambane zaidi director wa kazi kwa kutaka badala ya 10% aongezewe iwe 20% maana biashara ya kwanza walifanya vizuri tu. Director akaona sio kweli 20% hatoi na kama mbaya wacha iwe mbaya tu.
Tamu ila tamaa imemponza CEOPesa tamu lakini😀
Ila wabongo wengi tunafanya madeal ya kupiga pesa sehemu za kazi.Tamu ila tamaa imemponza CEO
Mbona siku hizi kuna wanaume wanagongwa!Wizi ni tabia za kiume?. Mbona siku hizi kuna wamama wezi wengi tu.
Kupiga pesa isivyo halali kwa namna yeyote ile ni kubaya.Ila wabongo wengi tunafanya madeal ya kupiga pesa sehemu za kazi.
Ila kupiga pesa kwa mtindo wa kumuonea mtu sio kitu kizuri hata kidogo.
Wewe hujawahi kupiga pesa kwa namna yoyote ile?Kupiga pesa isivyo halali kwa namna yeyote ile ni kubaya.
Unapopiga hela maana yake unadhulumu haki ya mtu au unaipora haki yake. Situation ziko aina mbili, anaepigwa anajua ama anaepigwa hajui chochote. Hii aina ya pili ndio angalau ina unafuu maana masononeko ya mpigwaji hayakufikii moja kwa moja ila aina ya kwanza ile mpigwaji anakuwa na masononeko muda wote na uchungu unaopelekea yeye kuchukua hatua dhidi yako.
Kupiga pesa mimi huwa napiga in situations ambapo naempiga anakuwa hafahamu chochote.Wewe hujawahi kupiga pesa kwa namna yoyote ile?
Ha haaa huna tofauti na wengine banaKupiga pesa mimi huwa napiga in situations ambapo naempiga anakuwa hafahamu chochote.
Ila ile kutengeneza mazingira kwamba mpigwaji ajue kabisa kwamba nampiga ishu za hivyo huwa sifanyi. Zile style kama za kiafande kwamba niungie tukamilishe jambo hizo huwa sifanyagi.
Ila unataka mzigo flani na najua unapopatikana hapo lazma nikuongezee sifuri mbele kisha ukituma hela najilipa juu kwa juu.
Ni kweli ila haiumizi kama una matatizo nakwambia leta laki 3 kwanza ili niweze kufikisha jambo lako kwa boss.Ha haaa huna tofauti na wengine bana
Very true....cheque inatolewa ya million 200 ila mpaka inamfikia mwenye tamthilia yake hapo si haba mtu anakunja 50M tu. Aanze kuwagaia wachezaji movie utashangaa kila mtu kapata million 3 tamthilia nzima [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ukikosa hiyo laki 3 hukosi huduma na unastahiliNi kweli ila haiumizi kama una matatizo nakwambia leta laki 3 kwanza ili niweze kufikisha jambo lako kwa boss.
Hapa jf habari picha huwa hainogi kabisa🤣🤣Hivi mkoje jamani? Mbona kila mmoja amedata na Barbara?
Siku nyingine nitaweka habari bila picha. 😂
Hapana sijakutana nae huko , ila kuna harufu ya upigaji kulikuwa na sintofahamu imeonekana ila haipo ktk category ya media ila ni mule mule katika kampuniKwani amewahi kukupiga na wewe Mkuu?
Bwana isike pesa za tamthilia zilimzidi,akawapangia nyumba machoko sinza,aliona wanawake hawafai,ukipeleka tamthilia hapo,wahuni wanakwambia tutakupa 8m kwa episode,Ila utabaki na sita,mbili zaoHii habari nimeiandika kwa ufundi mkubwa sana!
Kama asingetokea wa kusema hivi, ningevunjika moyo.
Nashukuru sana Mkuu
Nahisi haujawahi kutosha hata siku 1, duniani kote, maana kila nasikia lazima mtu uwe side hustles! 😄
Hizo side hustle sasa hapo kila mtu anatafuta/anajiongeza the easiest way kulingana na urefu wa kamba yake, hata km ni riskier! 😄
Ni maoni tu nisipigwe mawe tafadhali!
Isike ndiyo amekua mbaba hivyo alikuwaga mdogo sana kipindi anaigiza igizo la Ukimwi ITVThis is exclusive!
Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.
Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.
Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!
Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.
Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!
Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…
Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.
Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.
Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.
Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,
Nifah.
View attachment 2825510View attachment 2825511