Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Kumekucha DSTV, Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo na msaidizi wake wasimamishwa kwa rushwa!

Ila wabongo wengi tunafanya madeal ya kupiga pesa sehemu za kazi.
Ila kupiga pesa kwa mtindo wa kumuonea mtu sio kitu kizuri hata kidogo.
Kupiga pesa isivyo halali kwa namna yeyote ile ni kubaya.

Unapopiga hela maana yake unadhulumu haki ya mtu au unaipora haki yake. Situation ziko aina mbili, anaepigwa anajua ama anaepigwa hajui chochote. Hii aina ya pili ndio angalau ina unafuu maana masononeko ya mpigwaji hayakufikii moja kwa moja ila aina ya kwanza ile mpigwaji anakuwa na masononeko muda wote na uchungu unaopelekea yeye kuchukua hatua dhidi yako.
 
Wewe hujawahi kupiga pesa kwa namna yoyote ile?
 
Wewe hujawahi kupiga pesa kwa namna yoyote ile?
Kupiga pesa mimi huwa napiga in situations ambapo naempiga anakuwa hafahamu chochote.

Ila ile kutengeneza mazingira kwamba mpigwaji ajue kabisa kwamba nampiga ishu za hivyo huwa sifanyi. Zile style kama za kiafande kwamba niungie tukamilishe jambo hizo huwa sifanyagi.

Ila unataka mzigo flani na najua unapopatikana hapo lazma nikuongezee sifuri mbele kisha ukituma hela najilipa juu kwa juu. Au kwenye supplies ya bidhaa huwa tunafanya sana michezo sisi watu wa sales.
 
Kupiga pesa mimi huwa napiga in situations ambapo naempiga anakuwa hafahamu chochote.

Ila ile kutengeneza mazingira kwamba mpigwaji ajue kabisa kwamba nampiga ishu za hivyo huwa sifanyi. Zile style kama za kiafande kwamba niungie tukamilishe jambo hizo huwa sifanyagi.

Ila unataka mzigo flani na najua unapopatikana hapo lazma nikuongezee sifuri mbele kisha ukituma hela najilipa juu kwa juu.
Ha haaa huna tofauti na wengine bana
 
Hii habari nimeiandika kwa ufundi mkubwa sana!
Kama asingetokea wa kusema hivi, ningevunjika moyo.

Nashukuru sana Mkuu
Bwana isike pesa za tamthilia zilimzidi,akawapangia nyumba machoko sinza,aliona wanawake hawafai,ukipeleka tamthilia hapo,wahuni wanakwambia tutakupa 8m kwa episode,Ila utabaki na sita,mbili zao
 
Tutakupiga tu tukikukamata kama sio leo ni kesho, ni kweli mshahara hujawahi kutosha Yani sio mshahara ni kitu kinaitwa pesa haijawahi kutosha even a single minute
Nahisi haujawahi kutosha hata siku 1, duniani kote, maana kila nasikia lazima mtu uwe side hustles! 😄

Hizo side hustle sasa hapo kila mtu anatafuta/anajiongeza the easiest way kulingana na urefu wa kamba yake, hata km ni riskier! 😄
Ni maoni tu nisipigwe mawe tafadhali!
 
This is exclusive!

Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.

Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.

Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!

Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.

Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!

Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…

Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.

Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.

Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.

Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.

Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,

Nifah.

View attachment 2825510View attachment 2825511
Isike ndiyo amekua mbaba hivyo alikuwaga mdogo sana kipindi anaigiza igizo la Ukimwi ITV
 
Back
Top Bottom