Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tamaa tu!mshahara hautoshi...
Aaaah wapi! Hizo ni tamaa tu!Mshahara haujawahi kutosha
Ukiingiq kw3 payroll ndo utajua, saa hz endelea kula vya shemeji!Aaaah wapi! Hizo ni tamaa tu!
Hivi mtitu wa Game first Quality yupo wapi maana ni moja ya director bora wa films lakini hapendi spotlight kabisaa.Mkuu nimecheka sana, sana!
Lols
Kwakweli maua yake tumpe, amegeuka Mtitu wa kike.
Anaruka Azam TV now,sinema zetuHivi mtitu wa Game first Quality yupo wapi maana ni moja ya director bora wa films lakini hapendi spotlight kabisaa.
Hapati maua anayostahili
MkuuWalizidi wakajisahau.
Mkuu
Wale jamaa niliwakuta.
Kumbe wanajificha kwenye magazeti mule..hatari sana.
Nisingewakuta ningekupora moja.
Nimechukua za kutosha.Ungechukuq mbili mkuu
nifah pitapita na pale azamtv. nasikia msimamizi wa chaneli ya sinema zetu ambayo imepewa jukumu la kuonyesha local tv series, ana michezo kama ya huyo wa dstv.This is exclusive!
Mkurugenzi wa vipindi wa kitengo cha tamthilia za kiswahili zinazoruka kupitia kisimbuzi cha DSTV mwanamama Mtanzania Barbara Kambogi sambamba na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite yeye akiwa ni Mkenya wamesimamishwa kazi kwa tuhuma nzito za rushwa.
Mwanamama huyo na msaidizi wake walijijengea mfumo wao mahususi wa kuwezesha kuruka kwa sinema hizo za Kiswahili ndani ya kitengo hicho.
Mfumo huo ukiwa ni upigaji kwa pande zote, kwa madairekta kutakiwa kutoa hongo tamthilia zao zipate nafasi ndani ya DSTV, na huku haohao madairekta watakachopokea kutoka DSTV walitakiwa kugawana fungu na Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Hali hiyo ilidumu kwa kipindi kirefu, ikapelekea hadi wakawa sehemu ndani ya tamthilia za Jua Kali pamoja na Huba.
Ndio maana tamthilia hizo zinaikaribia Isidingo kwa ukaribu kwa mlolongo wa vipindi vyake visivyoisha!
Wazalishaji wa tamthilia hizo maarufu wanaofahamika ni mwanamama aliyejizolea sifa kubwa Leah Mwendamseke (Lamata) na Aziz Mohamed, ila nyuma ya pazia walikuwepo Mkurugenzi na msaidizi wake.
Ubadhirifu huo wa madaraka katika kitengo hicho uliingia sura mpya baada ya ingizo jipya la tamthilia ya Chanda.
Mkurugenzi kama ilivyo ada alitaka fungu liwekwe kama ulivyo utaratibu, mtayarishaji wa tamthilia hiyo bwana Isike Samweli alikataa kutoa ‘ushirikiano’
Ndipo balaa lilipozuka!
Mtayarishaji huyo (Isike Samweli) hapo awali alitayarisha tamthilia ya Pazia, na alitoa ushirikiano hadi alipokataa kwenye tamthilia yake mpya ya Chanda.
Alipokataa akaundiwa zengwe la kukatishwa kwa tamthilia yake hiyo ambayo bado ilikuwa inaendelea…
Bwana Isike hakukubalina na hilo, na kwa kuwa walikuwa na ‘ushirikiano’ hapo awali kwenye tamthilia ya Pazia alitunza ushahidi wote wa ushirikiano aliowahi kuwapa Mkurugenzi huyo na msaidizi wake.
Bwana Isike alienda mbali zaidi kwa kumwaga ugali baada ya Mkurugenzi kutishia kumwaga mboga yake.
Alituma email kwenda makao makuu Afrika ya Kusini akiambatanisha na ushahidi wote wa miamala ya ‘ushirikiano’ aliowahi kuutoa.
Baada ya tuhuma hizo nzito zenye ushahidi kufika makao makuu, ndipo Mkurugenzi huyo na msaidizi wake waliposimamishwa kazi kwa haraka kupisha utaratibu mwingine kufanyika wa kushuhulikia hilo.
Pichani ni mwanamama Barbara Kambogi, na mtayarishaji aliyeundiwa zengwe bwana Isike Samweli.
Nikiripoti kutokea hapa JF kupitia chanzo changu makini,
Nifah.
View attachment 2825510View attachment 2825511
Nimechukua za kutosha.
Uzuri wa haya madude hayaharibiki.
Hadi frem ichoke iachie.
Yaani niliyokuwa nayo ni ya tangu mwaka jana..zilikuwa mbili,nilikuwa nabadili nadhani ndo maana zimedumu.
Hio ndio ya kiafande zaidi unapigwa kilazima,Hapo kwa maafande Huwa pananiumiza sana, hivi kwanini askari wabongo kutimiza wajibu wake mpaka umfurahishe kwa kumpa hongo kidogo? Kiukweli hakuna askari aliyewahi kunisaidia pasipo kumrefushia mkono!
Sasa huko kunaitwa kujiongeza na Wala sio upigaji huo maana mtoaji wa hela kaitoa bila manung'uniko ya aina yoyote[/red]
Mbongo anakwambia pesa ni pesa haijalishi umeipata vipi maana hakuna sehemu utakayoenda kuitumia wataikataa kisa umeipata kwa njia isiyokuwa ya halali.
Inshaallah 🙏Shaka ondoa, pele limepata mkunaji.
Tuombe uzima tu, tutakuwa na wakati mzuri.
Kuna mtitu ambaye naye huwa anaigiza kwenye tamthilia zake na mwingine wa Game first quality ambaye alitoa sana movies.Anaruka Azam TV now,sinema zetu
Tamthilia yake ya Lolita imeshika kasi sana sasahivi.
J3 hadi alhamisi saa1 na nusu jioni.
Jamaa hana kazi mbovu.
Duh aiseWewe unashangaa hilo wakati ana App yake na anatoza hela kuona content zake na watu wanalipia wengi sana.
Nifah mwenyewe huyoHuyo Lamata na mwenzie Aziz
Zile nyimbo zao mpaka nimezikariri bila kupenda.
Kumbe!Kuna mtitu ambaye naye huwa anaigiza kwenye tamthilia zake na mwingine wa Game first quality ambaye alitoa sana movies.
Kama ni game first nihakikishie, nitafute king'amuzi cha azam chaap