Tetesi: Kumekucha: 'Kelele' za watanzania zawafikia DP World, watuma maofisa wao kujiridhisha

LAKINI mafundisho ya dini yana mshape mtu
Kwahiyo unataka kusema mafundisho ya dini yali mshape hata John P Magufuli ili aue watu?

Mimi nafikiri tupambane kuitoa CCM madarakani lakini tusije kuangukia kwenye mitego yao ambayo ni Devide and rule.

Samia hata hiyo hijabu kaanza kuivaa baada ya kulazimishwa na Wazee wa CCM..
 
Eti mazungumzo SIRINI!! Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka bandari yetu tu.
Asante
 
Nimesikia yule Mwanasheria Msomi Mwabukusi ameitwa polisi Mbeya.
 
all in all nimefuta hiyo portion ya dini....
 
Watu wapo tayari kuvunja katiba na kubadili sheria zote za nchi ili mradi tu kampuni moja ipewe tenda.

Jiulize kuna nini hapo.
 
zamani........alipitia seminari, sidhani kama alifundishwa kuua watu.
Dini zote zina mafundisho dhidi ya dini nyingine na kuitana majina ni moja ya mafundisho hayo kwa mfano heathens au kafiri.

Tujaribu kufanya mijadala bila kuingiza imani za watu tujikite kwenye hoja zenye kujenga.
 
Rais Samia, nini maoni yako kuhusiana na Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na DP World?[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kafanye homework yako vizuri. DP World wapo siku nyingi. Kila siku wanakuja na kuondoka, wana mengi sana ya kufanya.

kwa kkujuza tu, kuna mkataba utatangzwa siku mbili hizi.
 
Eti maafisa Dp- world

Kimsingi serikali imekuja kivingine baada ya Dili kubuma na kujinasua Sasa imewatuma mgongo wa nyuma Dp-world
 
mazungumzo hayo yawe live ili tujue nini kinaongelewa au ni mafurushi ya pesa yanagawiwa. tujue.
 
Serikali kupitia wakala wake imekuwa ikisisitiza kuwa IGA ni kati ya Serikali mbili yaani Tanzania Government and U.A.E Government ikiwa inamaanisha ndio maana halisi ya Inter-Government Agreement. Wakati tunaona mkataba umesainiwa na Kampuni ya Dubai na Serikali ikiwa tayari ni dosari!


Tumeambiwa D.P.W wataingia mikataba aina ya HGA na TPA. Na hivyo tusiwe na hofu DPW kujipachika kuwa ni Serikali-kwasababu Wananchi wamehoji-Ni kwanini mkataba huu usiwe baina ya Nchi mbili na badala yake umekuwa baina ya Serikali na Shirika la Bandari la Dubai!

Kwanini waje maafisa wa Bandari wa D.P.W kwanini isiwe Waziri wa Uchukuzi wa U.A.E au Mfalme wa Dubai? ambao ndio tunaaminishwa kuwa tumekubaliana katika mkataba huu? yaani IGA

Nawataadharisha(kwa nia njema kabisa) watu wenye hekima zao na Busara kutokufanya hivyo. (kukutana na hao maafisa uchwara)Na sema hivyo kwasababu baada ya kukutana huko kutaashiria Viongozi hao kutoa ridhaa na baraka zao isitoshe, watakuwa wamedhalilishwa sana-msijidhalilishe kukutana na "Maafisa wa D.P.W" shirika? kweli?

Serikali ya U.A.E au iwe ni ile ya Dubai kuwatuma Maafisa wa shirika la bandari yao kuja kufanya makubaliano, ushauriani, au "Mazungumzo" ni Kutudharau. Watanzania Msije kujidharaulisha. wacheni hao waliozikusanya firijini wafanye hivyo


Hii ni Dharau kubwa sana.
 
Haitasaidia maana wanazungumza na wale wale walioingia mkataba
 
Wamekuja na mpunga wa kutosha kwa ajili ya kujionea na kujiridhisha ya kwamba wale wanaopinga ukiwekwa mpunga wa kutosha mezani na mihadi kedekede,,Watachomoa au la??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…