bikira latifah
JF-Expert Member
- Oct 27, 2016
- 836
- 2,805
Kumbuka kwa sasa wanachaji nauli sh 1000 kituo hadi kituo, hiyo haitoshi kwa sasa wametuma ombi kwa LATRA kuwa wanafanya kazi kwa hasara hivyo wameomba kuzifungia daladala na bajaji zote njia ya Mbagala Kariakoo wabaki wenyewe
Je, wataweza?
--
Wakati Kampuni ya Mofat inayotoa huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika Barabara ya Kilwa ikiomba daladala ziondolewe katika njia hiyo, wadau na wananchi wamelipinga ombi hilo, wakisema mahitaji ya usafiri ni makubwa kuliko idadi ya mabasi hayo ya mwendokasi.
Tayari kampuni hiyo, imeshawasilisha ombi kwa Mamlaka ya Usafiri Ardhini (Latra), kuomba daladala, bodaboda na bajaji ziondolewe katika njia hiyo, ili ibaki pekee kutoa huduma za usafiri kwa njia hiyo.
Katikati ya malalamiko hayo ya Mofat, wananchi na wadau wa usafiri wamesema hautakuwa uamuzi sahihi kuiruhusu kampuni hiyo pekee itoe huduma katika njia hiyo, wakirejea yaliyotokea kwa Barabara ya Morogoro na kuzua adha ya usafiri kwa wananchi.
Wananchi hao wamekwenda mbali, wakisema baadhi yao usafiri wa mabasi yaendayo haraka unawagharimu zaidi kwani, unawatoza Sh1, 000 kwa safari tofauti na daladala na bajaji zinazotoza Sh500 hadi Sh700.
Mwananchi