Kumekucha Mbagala: Kampuni ya MOFAT imetuma ombi LATRA kuziondoa Daladala

Kumekucha Mbagala: Kampuni ya MOFAT imetuma ombi LATRA kuziondoa Daladala

Sikubaliano na hilo ombi Kwa sababu hata wakiruhusiwa wabaki peke yao hawana ufanisi.Tumeona kimara ni shida hadi unatamani huu mradi ufutwe.Gari unasubiri nusu saa au zaidi ya saa Moja.Barabara wanapita wenyewe tu na wanachelewesha watu pasipo sababu za msingi.
 
Kumbuka kwa sasa wanachaji nauli sh 1000 kituo hadi kituo, hiyo haitoshi kwa sasa wametuma ombi kwa LATRA kuwa wanafanya kazi kwa hasara hivyo wameomba kuzifungia daladala na bajaji zote njia ya Mbagala Kariakoo wabaki wenyewe

Je, wataweza?
Si waende njia ya Kimara? Maana haina kabisa mabasi. Biashara ni ushindani, ukiritimba hupandisha bei ya bidhaa na kupunguza ubora wa huduma.
 
Kumbuka kwa sasa wanachaji nauli sh 1000 kituo hadi kituo, hiyo haitoshi kwa sasa wametuma ombi kwa LATRA kuwa wanafanya kazi kwa hasara hivyo wameomba kuzifungia daladala na bajaji zote njia ya Mbagala Kariakoo wabaki wenyewe

Je, wataweza?
Hasara kiaje wakati yale magari yanajaza hadi watu wanashindwa kupumua?
Waache ujinga kabisa
 
Kwani hapo mwanzo wakati wanakuja kuomba kibali hawakuziona hizo daladala na bajaj?

Uwanja wao, refa wao, lakini bado wanataka kuhamisha magoli.

Sasa kwa ule mtiti ruti ya Mbagala uondoe daladala???
Sio mchezo.
Huwa naziona hizo Mofat zimejaza hadi pomoni!!
 
Kwani hapo mwanzo wakati wanakuja kuomba kibali hawakuziona hizo daladala na bajaj?

Uwanja wao, refa wao, lakini bado wanataka kuhamisha magoli.

Sasa kwa ule mtiti ruti ya Mbagala uondoe daladala???

Tatizo ni kwamba wakati serikali inapanga kuanzisha hiyo miradi ya BRT, ilikuwa daladala inabidi ziondolewe zibakie kuhudumia njia mbadala "feeder roads"...

Sasa si unajua tena serikali yetu, zilongwa mbali, zitendwa mbali...
 
Maendeleo yoyote yanakuja na hasara kwa wengine hata ujio wa sgr dar~dodoma ulileta hasara kwa wengine.Hivyo hamna budi kukubaliana na uhalisia wala hakuna sababu ya kuyachoma moto.
Huo mfano wa SGR kwani mabasi yameacha kufanya kazi Dar to Dom
Hao wajinga wanataka waachiwe uwanja wenyewe kisha ndio yatatokea ya nauli juu huduma mbovu
 
Wazee wanataka Mbeleko 😂 shenzi taipu. Wakati wanafanya assessment ya biashara yao hawakuona kuwa wanatakiwa ku compete na daladala ambazo zinaenda same route kwa bei nafuu zaidi?
Hakuna competition ya daladala na mwendokasi. Mwendokasi ineletwa ili kuwe na organized transport hivyo kwemye njia iliokamilika daladala lazima ziondoke. Phase zote zikitimia daladala zote zitahamia huko nje ya mji. Hio ndio hali halisi. Sio kwasabbau ya Abdul au Samia huo ndio utaratibu wa brt. Hii ya mbagala kivukoni gerezani imekamilika daladala lazima ziondoke zitaemda route ambayo brt haifiki huko huko Mbagala. Mfano Gerezani Tuangoma,Gerezani Mwandege daladala zitaemdelea kuwepo.
 
Kinacholalamikiwa siyo daladala kubaki
Kinacholalamikiwa ni hawa mabwana wa mwendokasi kukosa ufanisi na huruma kwa jamii wanayoihudumia

Watu wa mbangala wanayajua mateso ya watu kimara hivyo wanaogopa na kwao isije kuwa hivyo na mimi nawa unga mkono

Mwendokasi ikikosa ufanisi huwa inaleta mateso kuliko hata njaa
 
Kwani Kimara Kivukoni/Gerezani kuna daladala?
Daladala zitabaki kuhudumia njia nyingine
Kuna daladala za
mbezi - mnazi mmoja
Hizi Kuna zinazo pita barabaran ya morogoro na
Kuna zinazo pita njia ya korogwe zinatokea external Kisha njia ya kigogo mpaka mnazi1
 
Back
Top Bottom