Kumekucha Mbagala: Kampuni ya MOFAT imetuma ombi LATRA kuziondoa Daladala

Kumekucha Mbagala: Kampuni ya MOFAT imetuma ombi LATRA kuziondoa Daladala

Mambo ya hovyo sana,
Wakiachiwa hiyo route sasa hivi sio ajabu hawawezi kuhudumia hata nusu ya nahitaji ya abiria.
 
Hakuna
Ni wakati watu wakubaliane na uhalisia, tukiweka siasa kando, daladala, boda boda, machinga wanapaswa dhibitiwa
Kwa sasa boda boda na machinga ni kama wanafanya kila waonalo ni sawa
Huwezi kuwadhibiti wakati hakuna mbadala wa kutosha na uhakika kuhudumia abiria. Kama hizo bus za mwendokasi zingekuwa zinakidhi mahitaji abiria wenyewe wangeachana na Bajaji na bodaboda.
 
Ubaya nchi yetu inaongozwa Kwa siasa sana


Zilizuiliwa daladala za kipanya kuingia mjini ambazo zilikuwa zinabeba watu 10-20 ila wakaruhusu bajaji zinazobebq watu watatu. Sasa unashindwa kuelewa. Bado wakaruhusu Bodaboda Tena.


Nilijua tu huo mradi lazima ufeli hata kama ukipata serious investor haiwezekani njia ya BRT kuwa na daladala za kawaida na Bodaboda kama zote halafu utegemee muwelezaji apatae faida.


Hii yote ni kutaka kuridhisha wananchi kuwa daladala ziingie mijino na Bodaboda waingie mijini. Yani kutaka kuridhisha Kila mtu.


Cha msingi investor aongeze magari ya kutosha na wamanchi wapate huduma Kwa uhakika.
 
Kumbuka kwa sasa wanachaji nauli sh 1000 kituo hadi kituo, hiyo haitoshi kwa sasa wametuma ombi kwa LATRA kuwa wanafanya kazi kwa hasara hivyo wameomba kuzifungia daladala na bajaji zote njia ya Mbagala Kariakoo wabaki wenyewe

Je, wataweza?
Mbona 1,000 bado ndogo, ilipaswa angalau iwe 2,000!
 
Watu wengi wanaweka hisia mbele. Imagine eti bajaj zinakuwa kama daladala zinatoka tegeta hadi posta!
Nani mwenye elfu mbili yake anataka kupanda daladala zinazojaza watu kama viazi kwenye gunia kazi inakuwa kupakana jasho na kubambiana tu. Sheria ya kwanza nyepesi kabisa waliyoshindwa ni kudhibiti dalaladala kusimamisha abiria, waanzie kwanza hapo.
 
Kumbuka kwa sasa wanachaji nauli sh 1000 kituo hadi kituo, hiyo haitoshi kwa sasa wametuma ombi kwa LATRA kuwa wanafanya kazi kwa hasara hivyo wameomba kuzifungia daladala na bajaji zote njia ya Mbagala Kariakoo wabaki wenyewe

Je, wataweza?
Waondoe daladala
Kwa ufanisi gani walionao?
 
Uongozi waiomba serikkali kuwatimua bajaji, daladala na bodaboda kila Road kwani ushindani umkua mkubwa hivyo kupelekea hasara kubwa na kushindwa kulipa madeni ya mikopo pamoja na mishahara ya madereva.

Ikumbukwe kwamba Mofat imeanza kazi rasmi October 2025 ni mabasi 40 tu yanafanya kazi na 160 wameyapark tu 😂 . Wananchi wamepinga vikali sana hawataki au shida rangi 😂
 
Habari kamili Hii hapa

FB_IMG_17687681667956087.jpg
 
Back
Top Bottom