Kumekucha Mbagala: Kampuni ya MOFAT imetuma ombi LATRA kuziondoa Daladala

Kumekucha Mbagala: Kampuni ya MOFAT imetuma ombi LATRA kuziondoa Daladala

Watoe hizo bajaj. Bajaj haiwezi kuwa daladala. Ni kero na zinaleta vurugu na msongamano barabarani.
 
Ila haters wa Samia bwana, yaani mnaona sawa tu zile vurugu za hovyo hovyo za hao jamaa?!!! Yaani kusiwe na utaratibu kisa tu hatumpendi anayetawala......... pumbavu kabisa!
Kwa njia ya mwendo Kasi ipo kwa ajili ya nani?!!!!
Kwa mara ya kwanza nakubaliana na CHAWA. Hawa watu chuki zinawafanya wasione ukweli. Yaani hii chaos ya bodaboda na bajaj wanaona ni sawa? Hapana ziondolewe.
 
Mkuu umekurupuka kujibu. Mara nyingi huwa napenda kuwaasa watu wajipe muda wa kusoma na kuelewa kabla ya kujibu lolote

Hoja ya mofat wanataka daladala zisifanye kazi kwenye njia ambayo wao wapo Kama ilivyokua kimara. Yaani kusiwepo na gari za mbagala gerezani.

Wananchi wanataka daladala ziendelee uwepo
Njia anbayo brt bus zina operate ni laziima daladala zitoke. Huo ndio utaratibu. Daladala zihudumie route nyingine.
Wakishindwa daladala zitarudi.
 
Lengo la Mwendokasi(Mofat) ni kuondoa usafiri wa vurugu, ovyo na usio na ratiba wa Daladala, na kuweka usafiri wa haraka, salama na unaofuata ratiba.

Iwapo hao Mofat wana mabasi ya kutosha(naamini wanayo), hakuna sababu yoyote ya msingi ya Daladala kuendelea kutoa huduma.

Zaidi muundo wa Mwendokasi sio wa kiushindani! Na ili waweze kujiendesha lazima watataka kuondolewa kwa Daladala katika barabara wanazotoa huduma.
Watu wanapinga hii kwasababu ya hisia. Badala ya kuangalia uhalisia wanatanguluza chuki kwa watawala kutoa maoni yao. Daladala bajaj na bodaboda lazima zitoke.
 
waongeze ubunifu biashara ni ushindani sio kubebana
We ndo umeongea point. Kama wanataka kuziondoa daladala basi washushe bei mpaka 700, mbona zitaondoka zenyewe tu. Halafu baadae wanapandisha bei mpaka 1000 (kwenye uchumi hiyo tunaiita predatory pricing)
 
Watu wanapinga hii kwasababu ya hisia. Badala ya kuangalia uhalisia wanatanguluza chuki kwa watawala kutoa maoni yao. Daladala bajaj na bodaboda lazima zitoke.

Uhalisia ni kwamba Mwendokasi wanakabiliwa na ushindani kwa uwepo wa daladala kwenye route zao.
 
Uhalisia ni kwamba Mwendokasi wanakabiliwa na ushindani kwa uwepo wa daladala kwenye route zao.
Mwendokasi imeletwa kuondoa daladala. Hivyo njia yoyote ya mwendokasi ikikamilika daladala lazima ziondoke. Wapo watakaoathirika lakini ndio hali halisi daldala lazima ziondoke mpemde msipende.
 
wenzetu walioendelea wana trams na subways lakini mabasi bado yapo yanayosimama kituo hadi kituo. hapo nnachokiona mimi ni upigaji dili tu, kwn madaladala wao mabasi walipewa bure? si biashara kama hao Mofat? kwn daladala waliomba kutumia njia za brt? maoni yangu ni kuwa wacha biashara iwe shindanishi, TRA ikusanye kodi mnyonge ataeshindwa ushindani ata undergo natural death.
 
Kwa mara ya kwanza nakubaliana na CHAWA. Hawa watu chuki zinawafanya wasione ukweli. Yaani hii chaos ya bodaboda na bajaj wanaona ni sawa? Hapana ziondolewe.
Zipigwe ban importation basi

Ova
 
Mwendokasi imeletwa kuondoa daladala. Hivyo njia yoyote ya mwendokasi ikikamilika daladala lazima ziondoke. Wapo watakaoathirika lakini ndio hali halisi daldala lazima ziondoke mpemde msipende.

Sawa mkuu.. 😊
 
Mimi siungi mkono kufuta zote ila ipigwe hesabu ya kisomi juu ya uhitaji bodaboda tu ziachwe bajaji na daladala zipunguzwe kwa nakisi wasiyoiweza wao
 
Wajue daladala bajaj na bodaboda zikiondolewa wajiandae na kupambana na VIBAKA na masuara ya WIZI.
Rasivo watoe AJIRA za kutosha.

Baba wa Kaya ameshakufa, kaya inajiendesha haina msimamiz
 
Back
Top Bottom