Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,566
- 2,549
Lengo la Mwendokasi(Mofat) ni kuondoa usafiri wa vurugu, ovyo na usio na ratiba wa Daladala, na kuweka usafiri wa haraka, salama na unaofuata ratiba.
Iwapo hao Mofat wana mabasi ya kutosha(naamini wanayo), hakuna sababu yoyote ya msingi ya Daladala kuendelea kutoa huduma.
Zaidi muundo wa Mwendokasi sio wa kiushindani! Na ili waweze kujiendesha lazima watataka kuondolewa kwa Daladala katika barabara wanazotoa huduma.