Peter Msigwa Amkataa John Mrema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Kanda ya Nyasa ambako anachuana na Sugu kwa madai ya Rushwa na kumpendelea Sugu.
Just imagine hiki ndio chama Cha Upinzani kinachodia kitapambana na Rushwa yet chaguzi zao zote walioshindwa wametumia Rushwa ndio maana kutwa kucha wanashutumiana karibia mbao 😁😁😁😁
My Take
Umaskini wa Msigwa ndio chanzo Cha kutapatapa na kumuogopa taita Sugu.
Kwani nani alimkataza Msigwa kuwa na pesa? 😆😆😆😆
Mwisho Je Chadema Hawana Tume Huru ya Uchaguzi? 😬😬😬😬
---
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Nyasa ambaye pia anagombea kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa amewasilisha malalamiko dhidi ya Mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho John Mrema kwa kile alichokitaja kuwa mgongano wa masilahi katika uchaguzi wa kanda wa chama.
Katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, Msigwa ameeleza kuwa mwenendo wa John Mrema unazua maswali kwani ameonesha dhahiri kuegemea upande wa mgombea mwenza wa uenyekiti wa kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na kuonesha dalili zote za rushwa kinyume na “Kanuni ya 1 (vi) ya Mwongozo wa Chama dhidi ya Rushwa Kwenye Uchaguzi ndani ya Chama Toleo la 2012”.
“Tarehe 24 Mei, 2024 kabla na baada ya uchaguzi wa chama wa Mkoa wa Iringa, kuanzia majira ya asubuhi lakini pia saa kumi na mbili jioni alikutana na mgombea mwenzangu wa Kanda ya Nyasa katika nafasi ya uenyekiti Mhe. Joseph Mbilinyi, Twiga Night Club ambapo mgombea mwenzangu aliweza kununua kreti 4 za bia wakaendelea kunywa na msimamizi huyu wa uchaguzi mpaka majira ya saa sita usiku” Imeeleza barua ya Msigwa.
Ameendelea kueleza kwamba kwa nyakati tofautitofauti, Mrema amekuwa akiwapigia simu wajumbe (Wapiga kura) katika ngazi ya kanda akiwashawishi wasimchague Msigwa bali wamchague Sugu kwa madai kuwa kuwa hayo ni maagizo ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe.
Aidha Msigwa amemtuhumu Mrema kumsaidia mgombea uenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) kanda ya Nyasa Vitusi Nkuna kwa kueleza kuwa tarehe 26 Mei, 2024 Mrema ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi, alipanda gari ya Nkuna kutoka Iringa mpaka Makambako na kwamba siku mbili nyuma alikunywa naye pombe mpaka usiku wa manane.
Kutokana na mambo hayo, Msigwa ameomba Mrema aondolewe kwenye shughuli zinazohusiana na usimamizi wa uchaguzi na waletwe wasimamizi wengine ambao hawana masilahi binafsi katika uchaguzi huo ili haki iweze kutendeka kwa wagombea wote bila ubaguzi wala upendeleo.
Jambo TV