Kumekucha: Trump anataka mafaili yote ya siri kuhusu mauaji ya Rais John F. Kennedy na kaka yake Robert F. Kennedy yawekwe wazi kwa umma

Sijaelewa mkuu, yani kama ambavyo sahizi CCM inavyonyeshewa vidole kuhusu mauaji na kupotea kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA. Ambazo hizi tuhuma zinawachafua hadi kimaitaifa halafu wajue Mbowe au Lissu wamehusika na hayo mauaji wawaite wawapongeze?

Dude are you for really?
 
Kuna mziki huyu ujamaa anauwasha sasa jinsi ya kuucheza ndio shida maana midundo yake haijulikani, hata USA wenyewe hawajui wachezeje hiyo midundo. Ngoja sisi watazamaji watembeza bakuli tuangalie tu.
 
Hata ya Magufuli itakuja kuwa released tu siku moja. Hata miaka 100 ijayo ipo siku. Magufuli anatakiwa kuwekewa siku yake ya kumbu kumbu. Magufuli ni alama ya uzalendo kwa taifa.
 
Walete Tu ... Trump ana Moto sahivi Kila siku ni maagizo tu
 
Cha ajabu hataki mafaili ya siri ya Jeffrey Epstein yatolewe hadharani.
 
Huyu kuna watu kwenye system ana vita nao sasa anataka kuwaharibu na kuwavuruga kama walivyotaka kumfanyia yeye....jamaa analipiza kisasi
Watu waliokuwepo enzi za Kennedy kuuwawa wengi watakuwa wameshakyufa na walio hai mpaka sasa hivi watakuwa na miaka zaidi ya 90 wamejistaafia huko na dementia zao hata hawajui kinachoendelea duniani.
 
Tuliza akili soma vizuri uelewa na usikurupuke tu kujibu comments ambazo huna uelewa nazo halafu unahitimisha Kwa interpretation zako unazotaka wewe.

Kuelewa comment yangu kwanza unapaswa kujua mahusiano ya Malcolm X na Louis Farrakhan na Elijah Muhammad yalikuwa vipi alikadharika na Nation Of Islam iliwaunganisha vipi Hawa watatu, pamoja na serikali ya US iliwachukuliaje Hawa watatu miaka hiyo hasa Malcolm X.


Kama huelewi chochote hapo, basi huwezi kunielewa kamwe Kwanin kwenye comment yangu nimehusisha mfano wa Lissu na Mbowe.
 
Kuna utata lakini

Familia yake inadai CIA, FBI na NYPD walihusika
Mwaka 1995 Mmoja wa watoto wa Malcolm X anayeitwa Quibal Shabiz alikamatwa na FBI Kwa kosa la kupanga mauaji ya Louis Farrakhan, ambayo haya kufanikiwa.

Yule binti mpaka leo anaamini viongozi wa NOI akina Louis Farrakhan ndio walihusika na kifo Cha baba yake, na alihaidi at revenge.

So, sidhani kama kweli serikali ya US ilihusika.

Mimi mtu akiniambia serikali ya US ndio ilihusika na kifo Cha 2Pac nitakubali, maana haiwezekani Wala haingii akilini mpaka leo hii muuaji wa 2pac ajajulikana exactly ni nani... Na tukio lilotokea marekani hapo hapo na Tena imeshapita miaka 28.

FBI ina aminika ndio taasisi Bora ya upelelezi ulimwenguni na imeshafanya investigation za matukio mengi sana Kwa mafanikio, Sasa kivipi mpaka leo hii kifo Cha 2Pac Bado hawajakipatia majibu sahihi?
 
Trump anataka kuusambaratisha huo mtandao wa wauaji maana ukiangalia ni kundi la huo mtandao ndo waliomnurisha mara tatu kumuua alipokuwa anagombea uraisi mwaka jana.
 
Uko sahihi Kwa kiasi fulani na upande mwingine hauko sahihi, serikali ya US ilimpa ulinzi wa police baada ya yeye kuwa ameshajitoa kwenye NOI na y kuonesha Hali ya wasi wasi dhidi ya wanachama wa NOI.

Licha ya yeye kupewa walinzi lakini Bado hakuwa na amani, ndio maana alilala na bunduki chini ya mto, maana aliona kama ameongeza idadi ya maadui na aliwaogopa zaidi viongozi wa NOI maana aliondoka akiwatuhumu kwamba wanatumiwa na Klu Klux klan baada ya wao kukataa kufanya maandamano kwenye zile movement za civil rights.

Familia ya Malcolm X yenyewe iliwahi kumshataki Louis Farrakhan Kwa kauli zake tata zilizojaa chuki kuhusu Malcolm X kwamba Malcolm Hana umri mrefu wa kuishi.

Na siku ya tukio la mauaji yake miongoni mwa watu waliokamatwa ni Muhammad Abdul Aziz na Kahil Salim ambao walikuwa ni wanachama kindaki ndaki wa nation of Islam.

Na Kingine kama kweli serikali ya marekani ndio ingekuwa inahusika na mpango mzima, basi binti yake Quibal Shabiz asingeangaika na kulipiza visasi Kwa kutaka kuwaua akina Louis Farrakhan.
 
Unabisha nini wewe?..nani alimuwekea sumu kule misri?.. FBI/cia walimfuatia nini kule makkah?..alipozuiliwa kuingia ufaransa,akasema anajua adui zake ni serikali ya USA,sababu mojawapo ya kuuawa ni alliance yake na africa na baadhi ya viongozi wa africa waliona 'kwa nini tusiwasaidie waafrika wenzetu huko marekani kwa kuwapa silaha'?..waliomuua malcolm ndiyo waliomuua martin luther king jr, malcolm alishaanza kujenga ushirikiano na mlk jr
 
Ninaongea ninachokijua sibishi tu ilimradi kubisha.. wakati wewe unauliza kuwa CIA walimfuata Nini kule Makkah na kutumia kama ground ya kutuaminisha wao ndio waliomuua Malcolm, na Mimi pia nikuulize Kwa hiyo binti yake Qubilah Shabaz alikuwa ni kichaa kwenda kuwalipa hitmen ili wamuue Louis Farrakhan ilihali akijua kabisa waliohusika na mauaji ya baba yake ni CIA/serikali?

Yaani unashindwa hata kutumia utashi wa kawaida kwamba sometimes ukiwa na uhasama na serikali hata maadui zako wengine wa pembeni wanaweza wakatumia huo mwanya kukumaliza wakijua Culprit itakuwa ni serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…