Kumekucha: Yanga wamjibu Feisal Salum (Fei Toto)

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
Wakati Feisal akiwaaga wachezaji wenzake, mashaabiki wa Yanga, na uongozi kwa ujumla, Yanga wameibuka na madai mazito.

Habari hii hapa:

KLABU ya Yanga inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.

Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.

Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;

Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa
Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.

Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.

Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji.

Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024

Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.

Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.

Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.

Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans SC (YANGA).

Yanga, inasisitiza kuwa, Feisal Salum Abdallah ni mchezaji halali ya Yanga na ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024.

Imetolewa na Idara ya Habari
Young Africans Sports Club.

KUTOKA YANGA SC.
 
Ameshaaga official kijana. Tafuteni mbadala acheni kulialia utopolo.

20221224_161323.jpg
 
Ameshaaga official kijana. Tafuteni mbadala acheni kulialia utopolo.

View attachment 2456736
Kashaaga jana na mchana huu yupo kambini na wenzake nyinyi Makolo, waliomdanganya avunje mkataba ni nyinyi vihiyo, wenye akili wakamuambia dogo taratibu haziko hivyo chutama nguo zimekuvuka.
Sasa hivi Feisal anawalaumu kina Dauda za Zaka kwa kumuingiza chaka.
 
Sikutegemea Faisal na angeingia kwenye hili jinamizi...
Sipingi yeye kwenda Azam kwa huo mshahara hata Kama ni mimi ningesepa vizuri Ila Sasa angefata taratibu...
Walichofanya Yanga Ni kumgombanisha Fei na mashabiki na kwa hilo wamefanikiwa Sana.
Anyway kila la kheri kwake

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Mwigulu aongee na dogo, atapotea kama walivyopotea kina Ngasa na wengine waliochezea sharubu ya timu kongwe Simba na Yanga...

Hizo timu zipo radhi hata zikuroge lakini usiziletee 'zereu'
Ngassa alipotea sababu alileta dharau.

Feisal kafata pesa maana anakuwa na uhakika wa mshahara wa miaka 3

Mpira ni maisha mafupi sana

Feisal keshawaaga tayari

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Sikutegemea Faisal na angeingia kwenye hili jinamizi...
Sipingi yeye kwenda Azam kwa huo mshahara hata Kama ni mimi ningesepa vizuri Ila Sasa angefata taratibu...
Walichofanya Yanga Ni kumgombanisha Fei na mashabiki na kwa hilo wamefanikiwa Sana.
Anyway kila la kheri kwake

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Feisal keshawaaga

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kashaaga jana na mchana huu yupo kambini na wenzake nyinyi Makolo, waliomdanganya avunje mkataba ni nyinyi vihiyo, wenye akili wakamuambia dogo taratibu haziko hivyo chutama nguo zimekuvuka.
Sasa hivi Feisal anawalaumu kina Dauda za Zaka kwa kumuingiza chaka.
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
 
Mwigulu aongee na dogo, atapotea kama walivyopotea kina Ngasa na wengine waliochezea sharubu ya timu kongwe Simba na Yanga...

Hizo timu zipo radhi hata zikuroge lakini usiziletee 'zereu'
Tatizo la Yanga ni roho mbaya kwa wazawa tena ambao unaona kabisa wana uwezo mkubwa uwanjani kuzidi hao foreigners

Impact ya Feisal pale Yanga ni kubwa sana lakini ukiambiwa mshahara wake ni 4M unaweza ukashangaa.

Kuna uwezekano Kisinda akawa anapokea mshahara mkubwa kuliko Feisal, yule Azizi Ki ndio hata usiseme nadhani yupo on top hata kwa Mayele

Kama kulikuwa na wachezaji wengine ambao wako ndani ya Yanga ambao nao wanalipwa pesa ndogo kulingana na thamani yao basi kupitia hili sakata la Feisal naamini Yanga itaenda ku regulate hizo loopholes
 
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
Hilo la kulipwa hela ndefu unafikiri kuna Mtanzania mwenye akili timamu analikataa? Kila mwenye kujua mchango wa Feisal atataka aondoke Yanga hata leo kama kuna hela nzuri sehemu na Club imuachie akape anachostahili sehemu nyingine, ila taratibu zifuatwe wewe Kolobichwa.
Sasa Feisal amerudi kambini afate taratibu za kuvunja mkataba na Azam wenyewe wenye akili timamu wameliona hilo.
 
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
Nyie wajinga wajinga msioelewa kitu mnatusumbua sana, wakati fei toto anasaini mkataba huo wa kulipwa m.4 walikuwa wamemwekea bunduki kichwani? Kosa ni la yanga au la wasimamizi wake waĺishindwa kumpa thamani inayotakiwa? Leo hii mnarukia mambo kwenye vitu msivyovielewa, Nini maana ya makubaliano ya kimkataba,
 
Wakati Feisal akiwaaga wachezaji wenzake, mashaabiki wa Yanga, na uongozi kwa ujumla, Yanga wameibuka na madai mazito.

Habari hii hapa:

KLABU ya Yanga inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.

Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.

Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;

Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa
Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.

Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.

Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji.

Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024

Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.

Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.

Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.

Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans SC (YANGA).

Yanga, inasisitiza kuwa, Feisal Salum Abdallah ni mchezaji halali ya Yanga na ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024.

Imetolewa na Idara ya Habari
Young Africans Sports Club.

KUTOKA YANGA SC.
Weka barua siyo maelezo yako
 
Mbona hizi habari zimekuwa zenye kjzungumkuuti wakati ni jambo jepesi.........watu wakae mezani wayamalize kwa amani....hakuna haja ya kulazimishana.......
Inaonesha vile nchi yetu bado iko gizani kuhusu haya mambo ya mikataba ya wachezaji na klabu, vilabu bado vinaamini wachezaji huchezea timu zao kwa mapenzi badala ya kazi, iko siku wenye timu wataamka tu waache kuishi kwa mazoea.
 
Timu zinaamini kuwa mchezaji kuwatumikia ni kama kumsaidia.....
 
Siamini kama Feisal anaweza kuvunja mkataba kiholela bila kushauriwa na wanasheria, hao Yanga SC wawe makini sana kwenye hili mwisho wa siku wasije kuumbuka, maana kesi za kimkataba huwa wanapigwa chini na wachezaji kama ilivyokuwa kwa Morrison.
Ukiona amejiaminisha hivyo jua mkataba ushapita hadi TFF na wanasheria wengi kabla Azam hajaamua kutoa hela yake

Back
Top Bottom