Kumekucha: Yanga wamjibu Feisal Salum (Fei Toto)

Kumekucha: Yanga wamjibu Feisal Salum (Fei Toto)

SABABU FEI KUSEPA YANGA

Fei ameamua kujichomoa Yanga kutokana na kutotekelezwa kwa ishu yake ya kimasilahi ikiwamo ombi la ongezeko la mshahara anaolipwa.

Fei amewaeleza hana furaha kuona wachezaji kadhaa wa kigeni wakilipwa fedha nyingi, huku wakiwa wanaishia kukaa jukwaani tu
20221224_212626.jpg
 
SABABU FEI KUSEPA YANGA

Fei ameamua kujichomoa Yanga kutokana na kutotekelezwa kwa ishu yake ya kimasilahi ikiwamo ombi la ongezeko la mshahara anaolipwa.

Fei amewaeleza hana furaha kuona wachezaji kadhaa wa kigeni wakilipwa fedha nyingi, huku wakiwa wanaishia kukaa jukwaani tuView attachment 2457024
 
Ndo kanunua sasa huo mkataba wenu wa kimaskini!!!....hamuelewe nini???au mmevurugwa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hamna hela vinyesi fc..na wanamtaka na job sjui itakuaje[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna taratibu za kununua mkataba wa mchezaji sio kisa una hela tu bas unaweza kufanya chochote,
 
Kwamba Feitoto akiwa JKU alikuwa maarufu kuliko ambavyo yupo Yanga?
Ninachoamini hakuna mchezaji wa kisasa anacheza kisa umaarufu. Yanga haijamkuta anauza makopo, imempata anacheza mpira na ameondoka alikothaminiwa zaidi.
Azam sio wajinga walipe milioni 112 kwenye hamna, hawana utamaduni wa kutoa boko kwenye mikataba. Yanga ikafungue kesi kama haikubaliani na kinachoendelea
 
Kuna taratibu za kununua mkataba wa mchezaji sio kisa una hela tu bas unaweza kufanya chochote,
Hizo taratibu Azam wanazijua vizuri sana. Na kwenye michezo ingawa sina hakika kwa Tanzania ilivyo, kisheria huwezi mlazimisha mchezaji abaki kama hataki. Hii ni kuondoa ile hali ya timu kujimilikisha na kuwalazimisha wachezaji kama vile mateka. Mchezaji analindwa akae kwenye timu kwa consent.

Mikataba ya michezo kama ilivyo mikataba yote inabana pande mbili, mchezaji asingecheza labda kutoroka angechukuliwa hatua gani na timu isipomlipa ingechukuliwa hatua gani kama wangeenda jino kwa jino. Na release clause inasema fika kipi kifanyike, Yanga kutaka kukaa mezani sio takwa la kisheria. Hela imelipwa kama ilivyoainishwa, wazungumzie kitu gani?

Kwanza sio lazima tukivunja mkataba tukubaliane, cha msingi vifungu vya kuvunja mkataba vimetimizwa. Yanga ikitaka kumfukuza kocha wether anataka au hataki endapo masharti ya kuvunja mkataba yametimia basi ataondoka. Na Faisal kafanya hivyo, Bernard Morrison alifanya hivyo na wengine watafuata
 
Kama kweli analipwa mshahara wa 4m ni bora tu aondoke, Morrison hawezi kulipwa mshahara mara 4 ya Fei, huu ni uonevu uliopindukia! Mpira ni kazi kama zilivyo kazi nyingine ipo siku nguvu zitamuishia Fei atajivunia nini kama sio maslahi mazuri atakayatengeneza sasa! Life is now Fei fuata taratibu nenda kavute mshahara mzuri au ongea na mwajiri wako Yanga akuongezee mshahara wanaotaka kukulipa Azam period!!
Wakati anasaini hakujua kuwa ni ndogo?
 
Nakumbuka sakata la Neyma na barc, kabla ya Ney kuvunja mkataba na barc alisainishwa dili na qutar ili ionekana pesa ya kuvunja mkataba ameitolea huko na wanasheria wa Ney hawakudumbukiza pesa zile kwenye account za barc bali walienda na cheki mpaka ofisi za barc kuwaambia pesa iko tunataka kuvunja mkataba. Ikabidi wajadiliane wote kwanza waone kama mashariti ya mkataba yametimizwa kwa pande zote mbili, japo barc hawakutaka kumuuza Ney lakini baada ya kuona hamna kipengele kilichokiukwa ikabidi waandike barua ya kuachana naye. Huyu mzanzibari aangalie sana hasijekuja kuponzwa na mawakala wasaka cha juu baada ya kufuata taratibu zilizopo yeye anaruka step.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Mbona hizi habari zimekuwa zenye kjzungumkuuti wakati ni jambo jepesi.........watu wakae mezani wayamalize kwa amani....hakuna haja ya kulazimishana.......
Hakuna mkataba usiokuwa na kipengele Cha kuvunjwa..la sivyo utakuwa ni utumwa..dogo hajakurupuka..
Hapa viongozi wanajaribu kuficha udhaifu wao kwa kumchonganisha feisal na mashabiki wa yanga..
Ninaamini Hadi anaamua ku sign na Azam alishaongea na hwa viongozi wakampuuzia..wamwache akatengeneze maisha yake..maisha ya soka mafupi sana
 
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
Mkataba ni makubaliano ya pande mbili, huwezi walipa sawa watu wote, ukisema hivyo basi timu yote iwe na standard rate kwa wachezaji wote.
Hapa umetumia matako kuandika na sio kichwa.
 
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
Umemaliza mjadala..viongozi wanajaribu mchonganisha dogo na mashabiki..ni upumbavu wa Hali ya juu....
 
Kama kweli analipwa mshahara wa 4m ni bora tu aondoke, Morrison hawezi kulipwa mshahara mara 4 ya Fei, huu ni uonevu uliopindukia! Mpira ni kazi kama zilivyo kazi nyingine ipo siku nguvu zitamuishia Fei atajivunia nini kama sio maslahi mazuri atakayatengeneza sasa! Life is now Fei fuata taratibu nenda kavute mshahara mzuri au ongea na mwajiri wako Yanga akuongezee mshahara wanaotaka kukulipa Azam period!!
Unaujua mshahara wa Morrison wewe?
 
Ni kwa vile tu huko Yanga wote ni hamnazo, busara ya kawaida tu wangeachana naye kwani ni dhahiri Feisal hana moyo tena kuichezea Yanga na hata wakimpa mshahara anaotaka itazua mgogoro mpyaaaa kwa wachezaji wao nyota wazawa kwani watataka kuongezewa mishahara ilingane na hao matx. Kifupi dogo kawaweka la kati.
 
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
Umesema???
FB_IMG_1671396151308.jpg
 
Back
Top Bottom