Kumekucha: Yanga wamjibu Feisal Salum (Fei Toto)

Wakati Feisal akiwaaga wachezaji wenzake, mashaabiki wa Yanga, na uongozi kwa ujumla, Yanga wameibuka na madai mazito.

Habari hii hapa:

KLABU ya Yanga inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.

Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.

Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;

Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa
Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.

Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.

Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji.

Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024

Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.

Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.

Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.

Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans SC (YANGA).

Yanga, inasisitiza kuwa, Feisal Salum Abdallah ni mchezaji halali ya Yanga na ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024.

Imetolewa na Idara ya Habari
Young Africans Sports Club.

KUTOKA YANGA SC.
Hivi kuna tofauti ya maelezo na barua? Saini na muhuri viko wapi?
 
Ngassa alipotea sababu alileta dharau.

Feisal kafata pesa maana anakuwa na uhakika wa mshahara wa miaka 3

Mpira ni maisha mafupi sana

Feisal keshawaaga tayari

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Yes ni vizuri kucheza mpira kwa malengo na kikubwa zaidi pesa kwa sababu mpira wa sasa si wa ridhaa...

Lakini ninaona kama kuna step Feisal kaikosea, hapo alipoweka hadharani mustakabali wake kabla ya tamko la klabu yake iliyompa jina...

Hizo timu za Kariakoo zina fitna sana...
 
Nyie wajinga wajinga msioelewa kitu mnatusumbua sana, wakati fei toto anasaini mkataba huo wa kulipwa m.4 walikuwa wamemwekea bunduki kichwani? Kosa ni la yanga au la wasimamizi wake waĺishindwa kumpa thamani inayotakiwa? Leo hii mnarukia mambo kwenye vitu msivyovielewa, Nini maana ya makubaliano ya kimkataba,

Ndo kanunua sasa huo mkataba wenu wa kimaskini!!!....hamuelewe nini???au mmevurugwa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hamna hela vinyesi fc..na wanamtaka na job sjui itakuaje[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakati Feisal akiwaaga wachezaji wenzake, mashaabiki wa Yanga, na uongozi kwa ujumla, Yanga wameibuka na madai mazito.

Habari hii hapa:

KLABU ya Yanga inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.

Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.

Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;

Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa
Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.

Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.

Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji.

Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024

Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.

Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.

Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.

Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans SC (YANGA).

Yanga, inasisitiza kuwa, Feisal Salum Abdallah ni mchezaji halali ya Yanga na ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024.

Imetolewa na Idara ya Habari
Young Africans Sports Club.

KUTOKA YANGA SC.
Ahahahahah!! Wakati mlikuwa mnang'ang'ania kuwa Simba kuna mgogoro kumbe kwenu ndio mona haikai, mbili haikai!!! Ahahahahah!!!!
 
si walisema mshahara ni siri ya mwajiriwa?? sasa watulie ubwabwa umemwagwa kuku wanadonoa kwa kiwango chao sasa
 
Mwigulu aongee na dogo, atapotea kama walivyopotea kina Ngasa na wengine waliochezea sharubu ya timu kongwe Simba na Yanga...

Hizo timu zipo radhi hata zikuroge lakini usiziletee 'zereu'

Ww ungeacha milion 16? Ubaki kwenye milion 4
 
Acha uongo we kimba fc ,feisal kaaga Leo Tena muda sio mrefu nenda kwa page yake .
Mpeni pesa ya maana muone Kama ataondoka .Yaan Morrison alambe 18m alafu fei 4m huu si ni upumbavu kabisa.

Kwanza fei alipaswa awazid wachezaji wote hapo kwa salary ,maana yeye ndie injin ya timu .
Mmezoea kuwanyonya watanzania wenzenu na kuwapaparikia wageni ambao wanakua wakawaida tu kiuchezaji.

Na hili liwe fundisho hata kwa vilabu vingine ,wathamin wazawa wenye vipaji Kama fei.

Na hata akibaki fei hapo yanga lazima alipwe sawa na akina aucho au aziz key ,Mambo ya wageni wanakatwa Kodi nyingi hiyo haipo ,lipa pesa sawa na kiwango Cha mhusika
Kama unayoyasema ni kweli, kuna shida na club zetu
 
Suala sio kuacha hela bali ni namna ya kuondoka kwa mwajiri aliyekupa platform...

Platform kapata JKU, na ameondoka Kwa kuaga vizuri, hata usingeelewa ungeambiwa Acha 16 chukua 4
 
Sikutegemea Faisal na angeingia kwenye hili jinamizi...
Sipingi yeye kwenda Azam kwa huo mshahara hata Kama ni mimi ningesepa vizuri Ila Sasa angefata taratibu...
Walichofanya Yanga Ni kumgombanisha Fei na mashabiki na kwa hilo wamefanikiwa Sana.
Anyway kila la kheri kwake

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Sasa mashabiki mnamlipa nini Fei nyinyi mbn mnapenda kujitia umuhimu kwenye maisha ya watu au unafikiri nchi hii ina madhabiki wa Yanga tu
 
Yes ni vizuri kucheza mpira kwa malengo na kikubwa zaidi pesa kwa sababu mpira wa sasa si wa ridhaa...

Lakini ninaona kama kuna step Feisal kaikosea, hapo alipoweka hadharani mustakabali wake kabla ya tamko la klabu yake iliyompa jina...

Hizo timu za Kariakoo zina fitna sana...
Kama kweli analipwa mshahara wa 4m ni bora tu aondoke, Morrison hawezi kulipwa mshahara mara 4 ya Fei, huu ni uonevu uliopindukia! Mpira ni kazi kama zilivyo kazi nyingine ipo siku nguvu zitamuishia Fei atajivunia nini kama sio maslahi mazuri atakayatengeneza sasa! Life is now Fei fuata taratibu nenda kavute mshahara mzuri au ongea na mwajiri wako Yanga akuongezee mshahara wanaotaka kukulipa Azam period!!
 
Back
Top Bottom