Kumfanyia interview mwalimu ni kumsumbua na kumpotezea muda tu, ni urasimu

Kumfanyia interview mwalimu ni kumsumbua na kumpotezea muda tu, ni urasimu

Yani ukinambia unawafanyia interview walimu ndo uwaajiri binafsi naona haijakaa sawa.

MWALIMU siyo sawa na mtu wa kada zingine kama afya, tra, procurement na kada zingine.

MWALIMU anakaa na mwanafunzi mwaka mzima, dokta anakaa na mgonjwa mpka either afe au apone.

Point yangu ya msingi ni kwamba MWALIMU ananafasi nyingi ambazo anaweza kuzitumia kujifanyia tathimini na kumfanyia tathimini mwanafunzi wake na mwisho wa siku akamjenga na kumuandaa na akafaulu katika mtihani wa mwisho na akatoka na elimu yenye ubora mzuri.

Waajiriwa katika kada nyingjne hawana au wananafasi chache sana katika kujifanyia tathimini na kujipanga upya ili kuleta matokeo mazuri zaidi.

Mtu wa afya akifanya uzembe mgonjwa kaded hana nafasi ya kurekebisha na kuurudisha uhai wa aliyekufa. Hali kadhalika kada nyingine hakuna chances za kurekebisha ukiharibu umeharibu.

Mimi naona hakuna haja ya interview kwa walimu.
Jiandae na Interview, soon mtaitwa.
 
Usahili ni muhimu sana nilishawahi mara nyingi kuwa kwenye panel,yaani walimu wengine tulikuwa tunashangaa wamefaulu vipi vyuoni...
Tuliwahi kutafuta mwalimu wa hisabati kwa shule ya msingi darasa la tano hadi la saba kwenye huo usahili ilikuwa vichekesho vitupu.
Ukweli mchungu kwa sasa vyuoni kuna mabomu
Kuna media ilifanya challenge pale Udom ikawa inauliza neno "UDOM" lina tarakimu ngapi, huwezi amini hadi wanachuo walio third year walikua wanachemka

Yale majibu yalikua yanaonyesha kabisa Kuna shida kubwa vyuoni
 
Mtu anahoji waalimu kufanyiwa interview😥😥.. Mwalimu. mwalimu 🙄🙄hii nchi inabidi wote tu quit.
Taaluma zote hufanyiwa interview, ilikua kasoro afya na ualimu. Lakini bado mtu anaamini walimu kufanyiwa interview sio fair
 
Back
Top Bottom