Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

basi usifanye
 
Mimi naona sababu kubwa kuwafanyia watu wa afya hasahasa MDs ni kutaka kujua walio na utayari wa kazi. Wengi wamekuwa wakipangiwa kazi chini ya TAMISEMI sehemu za mbali na wamekuwa hawaendi. Hii husababisha serikali kuingia kwenye database na kuajiri madaktari wengine tena

Ukiona mtu katumia gharama zake kwenda kufanya interview labda Mtwara huko au Kigoma ujue huyo yupo tayari kufanya kazi sehemu husika

Kwahiyo kikubwa hapo ni kupima utayari wa wahusika. Na ndivyo nilivyo tonywa na kiongozi mmoja wa utumishi
 
Kwa mtu aliyesoma medical school na akaivaa hawezi hofia usaili ,usaili lengo ni kutengeneza fair ground kwa wahitaji wengi huku nafasi zikiwa chache , haimanishi ukikosa ndio haujaiva hapana ni kwamba tunataka mtu mmoja kati ya mia kwahyo lazima tutengeneze mazingira ya huyo mtu kupatikana ,hata fani ya veterinary medicine wanasoma miaka mitano kipindi cha nyuma ya 2013 Ajira zilikuwa moja kwa moja lakini walikuwa wachache ukute darasa linamaliza wanafunzi chini ya 20 sasa ,sahivi wanamaliza 50plus kwanini wasifanyiwe usaili?
Kwangu mimi bila usaili nadhani tutatengeneza upendeleo sana
 
Yani mzee nimeichukia fani ya afya na siwezi kumshauri kijana asome.

Shuruba ya maana alafu mshahara kidogo sana.
Mi naambiaga watu soon hii fani inaanza kuwa kama fani ya Uwalimu(Elimu). Kazi ina shurba na lawama kibao lakini ndio hivyo mishahara ya ajabu sana.

Kitaa unaonekana daktari smart lakini moyoni una stress za madeni huku ukiangalia gharama ulizotumia kusomea huo udaktari miaka mitano na unachokipata mwisho wa mwezi hakuna uwiano kabisa
 
Acha sifa za kihaya mkuu
 
Kwa daktari wa binadamu huhitaji chochote zaidi ya leseni yake ya udaktari, kwa kazi za CPA interview ni sahihi kwa sababu kuna kupiga maneno/siasa pia katika kazi zao tofauti na udaktari wa binadamu.
 
Daktari hahitaji usahili, leseni yake ya MCT inatosha.
 
Ukweli mchungu sana huu,
 
Daktari wa binadamu hahitaji interview ya kazi, leseni yake ya udaktari inatosha.
Uchache wa kazi ndio unasababisha interviews kuwepo, pia Daktari aliyefaulu kwa kiwango cha juu darasani kwa A nyingi ndiye Daktari bora hata kama atafeli usahili wa kupiga/kuuza maneno.
 
Kwenye udaktari muhimu ni ufaulu na experience, mambo ya ukarimu na personality ni kazi za siasa na fani nyingine za ngwini. Kwenye science jambo muhimu ni ufaulu, wanasayansi wakubwa zaidi duniani mfano washindi wa Nobel na vumbuzi mbalimbali ni watu fulani wasio na ukarimu au personality nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…