Kumfuatilia mumeo kila hatua kwa kisingizio cha upendo kunakera sana

Kumfuatilia mumeo kila hatua kwa kisingizio cha upendo kunakera sana

Ipo siku ataacha kukuuliza chochote. Utatamani aanze tena kuuliza ndo itakuwa imeisha hiyo.
 
Kwanza kabisa msimamo wangu, kama huo ni upendo naukataaa.

Uko kazini, unaulizwa unarudi saa ngapi? Umefika wapi? Mbona umechelewa kurudi? Angalia muda lakini!! Nashindwa kulala sababu yako.

Uko na nani? Mko Baa gani? Leo mpira unaangalia wapi? Usichelewe kurudi lakini, mtoto anasumbua amekumiss, anakutaka wewe.

Hujakaa sawa kapigiwa mshkaji ambaye uko naye, anaanza kuulizwa, "shem uko na fulani". Hii kitu imenishinda kwa kweli.

Wake mliopo ndoani au mnaishi na waume nauliza maswali kwenu naomba majibu.

1. Mume anapaswa kurudi nyumbani saa ngapi?

2. Ni sehemu gani inamfaa kuangalia mpira, banda umiza Baa yenye watoto wazuri?

3. Ikiwa umeagwa na kupewa location aliyopo kuna haja ya kucomfirm yuko na fulani kweli kwa kupiga simu?

Binafsi naona kwa level hii ni utumwa kwa mume na ni udhalilishaji pia.

Niko sawa au nazingua kwa mtazamo wangu?
Uko wapi
mbona nasikia sauti za wanawake hapo

za wanaume hawasikiagi 🤣🤣🤣
 
Uachwe kufuatiliwa ili ujipindue kwa makandokando yako ya zamani?

Usihofu mkizoeana hutafuatiliwa hata ulale nje poa tu. Subiri mzoeane hakuna rangi utaacha kuona kwa mkeo.

Pendo bado bichi utafuatiliwa kila ulipo shukuru kwa hilo maana yuaja wakati utaonekana kama nyanya masalo
Bora umemwambiaaa😅😅penzi bichii hiloo
 
Mnanitisha sasa
Ni kweli inakera lakini nakwambia ipo siku ataacha na kukupuuza. Chochote utakachofanya ataona sawa hatakasirika tena. Atakuwa busy na "mambo yake" mengine. Usirudi hapa kulalamika kwamba hakujali
 
Jambo lolote likizidi ni kero,hiyo ni kero na si mapenzi tena,kama inafikia mtu unaona karaha hapa pana shida

Tatizo si la mwanamke bali la mwanaume,mwanaume jifunze kuweka mipaka katika maisha yako ya mapenzi,tatizo wengi wetu hatujiamini ndio maana tunaacha mambo yaende tu hata kama hatuyapendi

Wanawake wana tabia ya kuleta drama kwahiyo ukikubali drama zake umekwisha,ndiyo hayo ya mleta mada sasa,mimi mke wangu mtarajiwa kwa ndoa ya pili,alianza kawaida ya kunipigia simu saa kumi na mbili asubuhi,nikamwambia huu utaratibu siupendi,maana unanifanya nihisi kama kuna dharura labda mtoto anaumwa kumbe salamu tu

Kanielewa na mapenzi yapo pale pale,hiyo tabia ya mkeo mimi siiwezi yan zamani angeacha huo upuuzi,sikatai kuchekiana lkn hiyo imezidi
 
Ni kweli inakera lakini nakwambia ipo siku ataacha na kukupuuza. Chochote utakachofanya ataona sawa hatakasirika tena. Atakuwa busy na "mambo yake" mengine. Usirudi hapa kulalamika kwamba hakujali
Hakuna ubaya kuliza uko wap lakini ndio iwe kila hatua kweli?
 
Jambo lolote likizidi ni kero,hiyo ni kero na si mapenzi tena,kama inafikia mtu unaona karaha hapa pana shida

Tatizo si la mwanamke bali la mwanaume,mwanaume jifunze kuweka mipaka katika maisha yako ya mapenzi,tatizo wengi wetu hatujiamini ndio maana tunaacha mambo yaende tu hata kama hatuyapendi

Wanawake wana tabia ya kuleta drama kwahiyo ukikubali drama zake umekwisha,ndiyo hayo ya mleta mada sasa,mimi mke wangu mtarajiwa kwa ndoa ya pili,alianza kawaida ya kunipigia simu saa kumi na mbili asubuhi,nikamwambia huu utaratibu siupendi,maana unanifanya nihisi kama kuna dharura labda mtoto anaumwa kumbe salamu tu

Kanielewa na mapenzi yapo pale pale,hiyo tabia ya mkeo mimi siiwezi yan zamani angeacha huo upuuzi,sikatai kuchekiana lkn hiyo imezidi
Kama mkeo ni msikivu, shukuru Mungu, wengine wataforce tu
 
Mke Wangu akat nakutana nae alikua anakunywa... Mbali zaid alikua ata akivuta sigara sio bangi.... Nilimvumilia na mm nilikua nakunywa lkn sigara hapana..

Sijui yalimkuta yapi tulipoingia Ndoanu mwenzangu Kawa mlokole

Mm sijabadilika Bado nakunywa
Ninavohubiriwa kama uyo shetan ndo Mimi

Wanawake wengi ni wabinafsi sana wanapenda tupende wanavyopenda wao
Ulioa mwanamke anayevuta sigara?
Mmh ulijilipua
 
Kama mkeo ni msikivu, shukuru Mungu, wengine wataforce tu
Wataforce kivipi

Inategemea unaongeaje naye,ukionyesha upo serious na maneno yako na matendo mbona atakuelewa tu,usimweleze kama unashauriana nae au unamuomba ruhusa,mwambie hupendi huo mwenendo mzima wa kutaka kujua niko wapi na nifanya nini,au sijui nipo na nani

Mwambie ni nini kinamfanya awe na mashaka kiasi hicho,ebu mfanye atoe mashaka yake kisha mpe maneno ya kumhakikishia wewe ni mtu mzima unajua nini cha kufanya,ila asikufanye kama mtoto kila wakati uripoti kwake kwamba umeingia hapa umetoka,yani ambayo ungetakiwa ufanye wewe kama mume na msimamizi uyafanye sasa inakuwa kinyume chake

Akiwa anajifanya kapinda basi usipokee simu wala kujibu meseji za hivyo,halafu tuone kama atataka talaka au laa

Mwanamke siku zote hatoacha kutest authority ya mwanaume wake au mume wake,halafu akishinda utasikia mume wangu nimemuweka kiganjani

Natumaini haupendi kufikia huko
 
Akiwa anajifanya kapinda basi usipokee simu wala kujibu meseji za hivyo,halafu tuone kama atataka talaka au laa
Siku hizi nimeona iwe hivyo tu, nikishatoa taarifa sehemu niliko napiga zangu *21*0755# natulia. Ukifika home unakuta kavimba
 
Siku hizi nimeona iwe hivyo tu, nikishatoa taarifa sehemu niliko napiga zangu *21*0755# natulia. Ukifika home unakuta kavimba
Ebu nipe elimu hii code inafanya nini hasa huenda ikatufaa kwa mambo mengi
 
Ebu nipe elimu hii code inafanya nini hasa huenda ikatufaa kwa mambo mengi
Hiyo code inazuia simu zote, bila kuathiri vitu vingine, yan ww unaweza kupiga cm ila haitapatikana yako. Na kutoa ni #21#
 
Back
Top Bottom