The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Joyce Banda (Malawi) kama Samia, aliangukia urais baada ya kufa rais naye akiwa makamu wake akatawazwa.
Banda aligombea urais na kubwagwa na Profesa Peter Mutharika mdogo wake marehemu Bingu wa Mutharika mwaka 2014.
Nchi ya jirani ya Zambia, Banda mwingine, yaani makamu wa rais Rupia Banda aliingia madarakani baada ya kifo cha Levy Mwanawasa na kubwagwa na Michael Sata mwaka 2011.
Je yawezekana CCM na Samia waliogopa kilichowapata akina Banda waliokuwa wameangukia urais baada ya kufa marais waliochaguliwa hadi wakaona ni bora wamfunge Lissu na kusababisha CHADEMA ishiriki uchaguzi?