Kumfunga Maria jela miaka 22 kisa nyama ya swala ni matokeo ya kuwa na wanasheria waliokosa hekima na busara

Hili suala limeniumiza sana
 
Unajali wanyama pori kuliko mtu!?..ongeza ulinzi kwenye hizo mbuga siyo kulostisha watu masikini..miaka 22!!!
 
Ni laana kbs
 
Ukiua tembo mmoja miaka 50 jela na utalipa fidia ya millioni 50.

Ila tembo akikuua familia yako itapata pole ya sh. Million 1 tu.

Ndo kinachofanyika huko kusini . People are die daily
Kuna kitu tunakosea sana kuhusu wanyama pori. Raia hawana elimu ya kuishi nao pale wanapoingia mazingira yao au wanyama wanapokuja mazingira yao.

Nadhani tunahitaji wataalamu wanaowafahamu hawa wanyama vema ili raia waweze kuelekezwa namna ya kuishi nao na kuweza ku:co exist.

Mnyama kama tembo akija eneo la makazi ya watu basi amepata harufu ya chakula kama mahindi, viazi, mihogo na kadhalika. So raia wanatakiwa kujua yule ni mnyama kitendo xha kumletea shari au kutaka kumfukuza itamlazimu kujitetea na ndipo hapo madhara hutokea.

Nimeshaona video ya tembo wanaokwenda kwenye hoteli ya kitalii na wapishi huwa wanaandaa mazaga wanawawekea hapo pembeni maana walifumua paa la jiko na ndipo hapo chakula wanaweka so wakija wanakula wakiwa wamesimama kwa nje na kupenyeza mikonge yao kwa ndani ya chumba cha jiko.

Imeshakuwa mazoea na hao tembo huwa wanakuja hapo mara kwa mara. Aiseee ukiwa muoga huwezi kukaa hilo eneo maana unakuta bonge la tembo linachungulia juu ya paa linaingiza mkonga wake kupapasa msosi. Halafu wanakuja kimya kimya.

Tembo anaweza pita nyuma ya jengo na usijue kama wapo nyuma ya nyumba hapo sasa tokea huko nyuma bila mahesabu utashangaa umempiga kikumbo. Me wakisema sehemu fulani tembo huwa wanapita au kuja sana huwa sishauri mtu aende hayo maeneo kama ana umakini mdogo maana ukizingua wanapita na wewe na kukudedisha ni dakika chache tu.
 
Mkuu kumbuka hiyo ni economic case [uhujumu uchumi]. Je case za aina hiyo zina hukumu ya conditional discharge?

Nadhani ungesema kwamba sheria zetu zina mapungufu kwa mfano kifungu cha 258[1] na 265 kinachohusu kosa la wizi hakitanabaishi thamani ya mali iliyoibiwa kwa maana kwamba mwizi wa Tshs 1b anafungwa kifungo sawa na mwizi wa Tshs 1m
 
Yupo muhukumu wa haki. Duniani watu wanapendeleana ndio maana ndugu zangu tumtazame bwana katika Kila teso la moyo wetu unapo onewa mwangalie muhukumu wa haki. Pili, siku Moja watashangaa wote Kwa hukumu walizo tuhukumu pasipo haki sisi masikini. Tumtazame yesu.
 
Hukumu ina kipengele cha faini?
Km kipo ni TSH ngapi mkuu?
 
Hichi kitu hiki? though nijuavyo, hapo kuna option ya fine, akilipa fine atatoka na swala hana thamani sana, anaweza kugharibu kama milioni tu (kama sikosei). though hata kulipa tu hiyo ati kwasababu ya swala, ni sheria ya kijinga kabisa hiyo.
 
Kilo 22 si ni nyama ya kuchoma na kutengeneza rosti kidogo kula na mumewe na watoto wake?

Ni uduanzi sana majitu ya ripoti ya CAG yanatingisha makalio kwa raha zao hawajaenda sero wala jela.
 
Nenda jela wewe kwa niaba yake km umemwonea huruma, mnafki mkubwa sheria ni msumemo haiangalii hali ya mtu. Sheria haijatungwa kwa maskini wala tajiri. Km we unajijua ni maskini tii sheria. Ufanye uhalifu halafu ndio uachwe kisa maskini? We kweli ni kenge tena mnafki tu unatafuta umaarufu wa kilofa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…