Kumfunga pingu Mwekezaji wa Mabasi ya Tilisho ni udhalilishaji, Vitisho na Ulevi wa madaraka

Kumfunga pingu Mwekezaji wa Mabasi ya Tilisho ni udhalilishaji, Vitisho na Ulevi wa madaraka

Huwezi kumtoa abiria Mbagala aende kupanda bus Magufuli stand wakati bus hilo hilo linalala kufanyiwa service Mbagala.
Uko sahihi. Kuongezea tu, kama moja ya malengo ni kupunguza foleni, Chalamila hapo ameshafeli. Sababu una abiria say watano wako mbagala, hawajuani, na wote wanapaswa waende magufuli kupanda basi, kila mmoja anachukua usafiri wake. Kwa hiyo una gari tano zinatoka mbagala kuelekea magufuli wakati wangeweza kuchukuliwa pale na basi (gari moja tu barabarani)
 
Baada ya mkurugenzi wa mabasi ya Tilisho Safari aitwae John Tilisho (aliyevaa suti[angalia chini kwenye Video] ), kufungwa pingu kwa madai ya kukaidi agizo la uongozi wa Juu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu stendi ya kimataifa ya Magufuli,


Mkuu wa Mkoa wa Dar bwana Chalamila kasema;
"...kama alivyosema amepigwa pingu kama sehemu ya onyo, natoa msahama kwa mkurugenzi wa Tilisho leo [Agasti 19,2026], nakwamba leo hii hii pia wamfungulie, na aruhusu mabasi yake yaweze kuingia na kutoka stendi ya magufuli...

kama kuna mtu yeyote anadhani nimekosea kutoa maelekezo haya, anipeleke mahakamani" Kasema Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ndug. Albert Chalamila.

MY TAKE
Chalamila kaagiza Msimamizi wa Mabasi ya Tilisho fungwe pingu kwenye mkutano wa hadhara. Halafu akaambia waandishi wa habari wapige picha wazisambaze. Na wapambe wa Chalamila wakaambiwa wamzomee.
View attachment 3653446
Nahisi wana ugomvi binafsi. Sababu hata Chalamila ni msafirishaji(transporter) kama Tilisho

Hii ni dalili ya serikali isiyofuata Sheria. Mwanasiasa anaamrisha Polisi kufanya chochote. Hata akisema ua wanaua.

Sasa kama Bosi anafamyiwa hivi, vipi sisi walala hoi?

Nalaani alichofamya Chalamila. Kalewa madaraka.

Boss kama kosa, angepewa barua ya wito? Atakimbia aende wapi?

Kapigwa pingu, kazungushwa zungungwa maeneo ya Standi kisha akaachiliwa bila kupelekwa polisi wala mahakamani wala kuchukuliwa maelezo.

Viongozi wa awamu ya Sita wana roho mbaya
View attachment 3653443

WASIO MJUA JOHN TILISHO

John Tilisho ni Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Usafirishaji ya Tilisho Company Limited (Tilisho Safaris) inayofanya safari za mabasi ya mikoani kama vile Dar es Salaam kwenda Arusha, Moshi, na Rombo. Kampuni yake ni mwanachama wa wadau wa sekta ya usafiri na inahusishwa na chama cha wamiliki wa mabasi (TABOA) kupitia shughuli za usafirishaji.

Na wamiliki wa Mabasi walimtuma kwa mkuu wa mkoa awatetee. Alitaka wakae chini wajadiliane na Serikali, matokeo akapigwa pingu.
Kuanzia leo basi langu nikipata safari ya kanda ya kaskazini ni Tilisho
 
Acha ushamba,jamaa alivunja sheria tena chala kamfanyia uungwana tu,nchi inayofuata sheria bila kujali ww ni nani yule jamaa saa hizi angekua kashashtakiwa,siku yake vunja sheria halafu uone kama utapewa barua eti ukaripoti mwenyewe
Kwa hiyo sheria nchini aliyepewa mamlaka ya kuzitekeleza na kuzisimamia ni viongozi wa ccm na chalamila wake? Hicho kitendo cha kumfunga mhalifu kama wewe unayemsema na kumzungusha stendi sheria namba ngapi ya mwaka gani?
 
M’bongo ni kiumbe ambacho kujitambua ni mtiti kwelikweli, anatakiwa kiongozi wa action lakini akitokea kiongozi wa action anaanza kuonekana mbaya kwa sababu ndogo tu. Sasa mtu kuvalishwa pingu ndo inafanya mtu aache kuwaza uamuzi wa muhimu wa kurudisha mabasi stendi kuu? Yaani pingu ambayo mtu unaweza ukavalishwa na ukavuliwa na maisha yakaendelea!? Cumon man Bongo inahitaji kujadili mambo ya msingi kuliko hayo mkuu hasa yanayowahusu vigogo
 
Chalamila anafanana kama Ninja Turtle 😆😆😆

Smart911
Sio kwa ubaya lakini nimeenda google.
Ni kweli anafanana nae
Screenshot_20260820_073322_Chrome.png
 
Kupigwa pingu sio shida,ila hao fukara wanaopiga kelele hapo ndio ambao haswaa wanasikitisha.Vibali vya Stand binafsi za mabasi vinatolewa kwa mujibu wa Sheria na sio kwa bahati mbaya.Magufuli Terminal ni nzuri ila haiondoi uhitaja wa Private Terminals.

Chalamila ana shida zake nyingine.Hii nchi tukiwaambia bado sana mnashangaa shangaa
 
Uko sahihi. Kuongezea tu, kama moja ya malengo ni kupunguza foleni, Chalamila hapo ameshafeli. Sababu una abiria say watano wako mbagala, hawajuani, na wote wanapaswa waende magufuli kupanda basi, kila mmoja anachukua usafiri wake. Kwa hiyo una gari tano zinatoka mbagala kuelekea magufuli wakati wangeweza kuchukuliwa pale na basi (gari moja tu barabarani)
I see!
 
Zamani wakati stendi zipo kisutu na mnazi mmoja watu walikuwa wanapandaje mabus na stand mitaani ilikuwa hakuna?

Wacheni kufanya mazoea iwe sheria.
Fateni utaratibu...

Kama unaishi mbagala na usafiri wako ni Magufuli terminal hyo ni changamoto uliyojitakia mwenyewe.
Jenga au panga chumba kutokana na location ya kwenu..
Mkuu wa mkoa yupo sahihi kutumia nguvu.
Mbona wakati wa Magufuli watu wote walitii amri hii na hakuna aliyelalamika kwamba stand ipo mbali na makazi?
Na kwann 90% ya wanaokaidi na kulalamika ni wamiliki wa mabus?kuna nn nyuma ya kuweka stand mitaani?
Tuko leo wewe unazungumzia zamani?

Zamani palikuwa na gharama hizi za usafiri zilizopo leo?

Zamani palikuwa na usumbufu kwa abiria uliopo leo kutokana na kuongezeka idadi ya watu?

Acha kufikiria kizamani.
 
Zamani wakati stendi zipo kisutu na mnazi mmoja watu walikuwa wanapandaje mabus na stand mitaani ilikuwa hakuna?

Wacheni kufanya mazoea iwe sheria.
Fateni utaratibu...

Kama unaishi mbagala na usafiri wako ni Magufuli terminal hyo ni changamoto uliyojitakia mwenyewe.
Jenga au panga chumba kutokana na location ya kwenu..
Mkuu wa mkoa yupo sahihi kutumia nguvu.
Mbona wakati wa Magufuli watu wote walitii amri hii na hakuna aliyelalamika kwamba stand ipo mbali na makazi?
Na kwann 90% ya wanaokaidi na kulalamika ni wamiliki wa mabus?kuna nn nyuma ya kuweka stand mitaani?
Mbuzi kama Hizi Ndio zinafanya Nchie iendelee kupiga Reverse.

Issue sio mabasi kwenda Mbezi issue ni Uhitajia wa Stand Binafsi.Kitu cha muhimu ni kuhakikisha kwamba Vigezo vya Private stand vinakuwa vya hadhi ya Juu,Mazingira mazuri.Pale Magufuli iwe ni Reporting Station kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila gari lazima ama lipite pale au limalizie safari pale
 
Kwa hiyo sheria nchini aliyepewa mamlaka ya kuzitekeleza na kuzisimamia ni viongozi wa ccm na chalamila wake? Hicho kitendo cha kumfunga mhalifu kama wewe unayemsema na kumzungusha stendi sheria namba ngapi ya mwaka gani?
Ni kufuata tu sheria bila shuruti,ukishavunja sheria au kutuhumiwa kitu inabidi ufuate tu mamlaka inachotaka,ogopa sana serikali inapokutumia unapotenda kosa uwe mfano kwa wengine
 
Hivi vyeo vya Mkuu wa Mkoa na Wilaya, wananchi tulishavikataa kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Kinachoendelea kutokea hata sasa ni ushahidi tosha vimepitwa na wakati.
 
Sio kila amri ya serikali ni halali, nyingine ni haramu, ni bahati mbaya tu huwezi kupeleka kesi mahakamani dhidi ya serikali ukashinda.
Amri haramu zina njia zake kisheria kuzi challenge na watu wengi tu wameishinda serikali, alichokifanya tilisho kisipodhibitiwa nchi itakuwa kama congo kila mtu mtemi, tusitetee ujinga
 
Ni kufuata tu sheria bila shuruti,ukishavunja sheria au kutuhumiwa kitu inabidi ufuate tu mamlaka inachotaka,ogopa sana serikali inapokutumia unapotenda kosa uwe mfano kwa wengine
Siyo kazi ya executive kutoa hukumu. Tanzania siyo banana Republic. Babu zetu hawakupigania uvunjifu wa sheria na serikali
 
sio eneo ni bus lilipigwa cheni ilihali basi hilo lilishakatiwa tiketi lilitakiwa kusepa jamaa akafungua ndo iliyosababisha kupigwa pingu kwa kukaidi amri pia ni akili kubwa sana ametumia otherwise angepata hasara kutokana na bus hilo kutofanya safari kwa siku husika kwa kigezo cha tyre kupigwa cheni tu?.
Yes na amestahili alichofanyiwa, sasa mabasi yalishapewa notice na serikali kwamba ikifika tarehe hii msionekane shekilango yeye ni kiburi kinamsumbua, na ana bahati sana,alitakiwa akae hata aiku tatu ili iwe fundisho kwa watu wanaofharau amri halali za serikali kisa hela, mbona kina bakhressa hawana tabia kama hizi
 
Chalamila anajua kazidiwa hoja na amekosea, sasa ameamua kutumia nguvu.

Uamuzi wake ni wa kijinga na hauvumiliki, unaongeza gharama na usumbufu kwa abiria.

Huwezi kumtoa abiria Mbagala aende kupanda bus Magufuli stand, wakati bus hilo hilo linalala na kufanyiwa service Mbagala.
Yule hana akili ni mropokaji hana hekima wala busara, Dsm inahitaji watu kama Mtaka wa Njombe wanao reason kulingana real life situation of the lower class people siyo kujitutumua na kukuza ubabe wa kijinga
 
Back
Top Bottom