Kumfunga pingu Mwekezaji wa Mabasi ya Tilisho ni udhalilishaji, Vitisho na Ulevi wa madaraka

Huwezi kumtoa abiria Mbagala aende kupanda bus Magufuli stand wakati bus hilo hilo linalala kufanyiwa service Mbagala.
Uko sahihi. Kuongezea tu, kama moja ya malengo ni kupunguza foleni, Chalamila hapo ameshafeli. Sababu una abiria say watano wako mbagala, hawajuani, na wote wanapaswa waende magufuli kupanda basi, kila mmoja anachukua usafiri wake. Kwa hiyo una gari tano zinatoka mbagala kuelekea magufuli wakati wangeweza kuchukuliwa pale na basi (gari moja tu barabarani)
 
Kuanzia leo basi langu nikipata safari ya kanda ya kaskazini ni Tilisho
 
Acha ushamba,jamaa alivunja sheria tena chala kamfanyia uungwana tu,nchi inayofuata sheria bila kujali ww ni nani yule jamaa saa hizi angekua kashashtakiwa,siku yake vunja sheria halafu uone kama utapewa barua eti ukaripoti mwenyewe
Kwa hiyo sheria nchini aliyepewa mamlaka ya kuzitekeleza na kuzisimamia ni viongozi wa ccm na chalamila wake? Hicho kitendo cha kumfunga mhalifu kama wewe unayemsema na kumzungusha stendi sheria namba ngapi ya mwaka gani?
 
M’bongo ni kiumbe ambacho kujitambua ni mtiti kwelikweli, anatakiwa kiongozi wa action lakini akitokea kiongozi wa action anaanza kuonekana mbaya kwa sababu ndogo tu. Sasa mtu kuvalishwa pingu ndo inafanya mtu aache kuwaza uamuzi wa muhimu wa kurudisha mabasi stendi kuu? Yaani pingu ambayo mtu unaweza ukavalishwa na ukavuliwa na maisha yakaendelea!? Cumon man Bongo inahitaji kujadili mambo ya msingi kuliko hayo mkuu hasa yanayowahusu vigogo
 
Kupigwa pingu sio shida,ila hao fukara wanaopiga kelele hapo ndio ambao haswaa wanasikitisha.Vibali vya Stand binafsi za mabasi vinatolewa kwa mujibu wa Sheria na sio kwa bahati mbaya.Magufuli Terminal ni nzuri ila haiondoi uhitaja wa Private Terminals.

Chalamila ana shida zake nyingine.Hii nchi tukiwaambia bado sana mnashangaa shangaa
 
I see!
 
Tuko leo wewe unazungumzia zamani?

Zamani palikuwa na gharama hizi za usafiri zilizopo leo?

Zamani palikuwa na usumbufu kwa abiria uliopo leo kutokana na kuongezeka idadi ya watu?

Acha kufikiria kizamani.
 
Mbuzi kama Hizi Ndio zinafanya Nchie iendelee kupiga Reverse.

Issue sio mabasi kwenda Mbezi issue ni Uhitajia wa Stand Binafsi.Kitu cha muhimu ni kuhakikisha kwamba Vigezo vya Private stand vinakuwa vya hadhi ya Juu,Mazingira mazuri.Pale Magufuli iwe ni Reporting Station kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila gari lazima ama lipite pale au limalizie safari pale
 
Kwa hiyo sheria nchini aliyepewa mamlaka ya kuzitekeleza na kuzisimamia ni viongozi wa ccm na chalamila wake? Hicho kitendo cha kumfunga mhalifu kama wewe unayemsema na kumzungusha stendi sheria namba ngapi ya mwaka gani?
Ni kufuata tu sheria bila shuruti,ukishavunja sheria au kutuhumiwa kitu inabidi ufuate tu mamlaka inachotaka,ogopa sana serikali inapokutumia unapotenda kosa uwe mfano kwa wengine
 
Hivi vyeo vya Mkuu wa Mkoa na Wilaya, wananchi tulishavikataa kwenye ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba. Kinachoendelea kutokea hata sasa ni ushahidi tosha vimepitwa na wakati.
 
Sio kila amri ya serikali ni halali, nyingine ni haramu, ni bahati mbaya tu huwezi kupeleka kesi mahakamani dhidi ya serikali ukashinda.
Amri haramu zina njia zake kisheria kuzi challenge na watu wengi tu wameishinda serikali, alichokifanya tilisho kisipodhibitiwa nchi itakuwa kama congo kila mtu mtemi, tusitetee ujinga
 
Ni kufuata tu sheria bila shuruti,ukishavunja sheria au kutuhumiwa kitu inabidi ufuate tu mamlaka inachotaka,ogopa sana serikali inapokutumia unapotenda kosa uwe mfano kwa wengine
Siyo kazi ya executive kutoa hukumu. Tanzania siyo banana Republic. Babu zetu hawakupigania uvunjifu wa sheria na serikali
 
Yes na amestahili alichofanyiwa, sasa mabasi yalishapewa notice na serikali kwamba ikifika tarehe hii msionekane shekilango yeye ni kiburi kinamsumbua, na ana bahati sana,alitakiwa akae hata aiku tatu ili iwe fundisho kwa watu wanaofharau amri halali za serikali kisa hela, mbona kina bakhressa hawana tabia kama hizi
 
Yule hana akili ni mropokaji hana hekima wala busara, Dsm inahitaji watu kama Mtaka wa Njombe wanao reason kulingana real life situation of the lower class people siyo kujitutumua na kukuza ubabe wa kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…