Kumfunga Sabaya huku mamlaka zikimtetea Paul Makonda hii haikubaliki

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari,

Mimi ni miongoni mwa watu wachache tuliokuwa tukiuchukia uongozi wa Magufuli.

Matendo maovu na viburi kutoka kwa wateule wa Magufuli akiwemo Sabaya na Makonda ndivyo vilichochea zaidi kuichukia serikali ya Magufuli.

Hawa vijana waliojizolea utajiri kwa kutumia mamlaka yao hawafai kabisa.

Sasa inakuwaje mamlaka inamfunga Sabaya na mamlaka hiyohiyo inatoka hadharani kusema Makonda ni kijana msafi mchapa kazi ilhali dhambi za hawa vijana ziko wazi?

Yule afisa wa PCCB aliyemsafisha Makonda mchana kweupe alitumwa na nani?

Aliweka kizuizi kwetu wananchi ili tusiende kuripoti matendo maovu kwenye ofisi yake?

Basi Sabaya aachiwe tujue kuwa hii nchi dhulma na uovu si dhambi.

==
Soma Kesi ya Uporaji wa Gari inayomkabili Makonda yaanza kuunguruma Mahakamani. Apewa siku 14 kuwasilisha utetezi wake
 
Hivi chade hawakuwa wanamuita mamvi fisadi! Mbona walimuunga mkono wakampa ugombea!.. vipi nae hafungwi..?
 
Mizizi ya makonda itakuwa imejichimbia zaidi tangu familia ya msoga(japo aliwachezea rafu mpaka rizmoko kulalamika) hadi ile ya chatto

Kumbuka bumge la katiba kuna kijikauli alikitamka ambacho nadhani mama anakichukulia kama utabiri uliotimia vyote hivyo vina wapa kigugumizi cha kuamua
 
Acha unaa wewe, kama fisadi ccm wamemfanya nini?

Serikali ya ccm
Vyombo vya Dola vyote vya ccm

Hebu tuambie ufisadi wake upo wapi?
Hao ccm wao ndo walisema kuwa ni fisadi..?
 
Subiri takuletea na video
2801281_Screenshot_20210607-213832_Facebook.jpg

Tunaomba ushahidi wa hii kauli yako?
 
Hivi chade hawakuwa wanamuita mamvi fisadi! Mbona walimuunga mkono wakampa ugombea!.. vipi nae hafungwi..?
Mbona baada ya kwenda chadema ccm walikua wanamuita Lowasa ni fisadi? Lakini leo lowasa yuko wapi?
 
Habari,

Mimi ni miongoni mwa watu wachache tuliokuwa tukiuchukia uongozi wa Magufuli.

Matendo maovu na viburi kutoka kwa wateule wa Magufuli akiwemo Sabaya na Makonda ndivyo vilichochea zaidi kuichukia serikali ya Magufuli.

Hawa vijana waliojizolea utajiri kwa kutumia mamlaka yao hawafai kabisa.

Sasa inakuwaje mamlaka inamfunga Sabaya na mamlaka hiyohiyo inatoka hadharani kusema Makonda ni kijana msafi mchapa kazi ilhali dhambi za hawa vijana ziko wazi?

Yule afisa wa PCCB aliyemsafisha Makonda mchana kweupe alitumwa na nani?

Aliweka kizuizi kwetu wananchi ili tusiende kuripoti matendo maovu kwenye ofisi yake?

Basi Sabaya aachiwe tujue kuwa hii nchi dhulma na uovu si dhambi.
Siku Makonda akishtakiwa na akahukumiwa kifungo kuanzia hapo ntaamini uchawi haupo na sintowaamini waganga Tena!
 
Makosa ya Sabaya ni ya uporaji na utesaji .
Yako wazi sana.

Ila Makonda makosa yake yalifichika sana na alikua anatumia zaidi vyombo husika.

Makonda alikua anajirekebisha kwa kadri siku zilivyokua zinasonga mbele.

Alikua ameanza kuwa Mstarabu kama Mrisho Gambo.
Ndio maana alitaka kuwa Mbunge ili aepukane na maagizo toka juu.

Kidogo Makonda tunaweza kumwachia Mungu tu . Lakini pia amejipoteza kwenye siasa za kistarabu katika ulimwengu wa waungwana.
Atubu na kuwaomba msamaha watanzania.
Ikiwezekana aunge mkono juhudi za kupata katiba mpya ili Mzimu wa Warioba usije ukaendelea kumwandama.

Mbowe hana hata kauli ya ugaidi.
fREeMboWe.

Kumweka Mbowe gerezani pamoja na Mhalifu Jambazi Sabaya ni kunajisi Uhuru na Utu wa mtanzania . Ni kumkejeli baba wa Taifa aliyeilea kwa uadilifu na kushirikiana na Familia ya Mbowe.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Habari,

Mimi ni miongoni mwa watu wachache tuliokuwa tukiuchukia uongozi wa Magufuli.

Matendo maovu na viburi kutoka kwa wateule wa Magufuli akiwemo Sabaya na Makonda ndivyo vilichochea zaidi kuichukia serikali ya Magufuli.

Hawa vijana waliojizolea utajiri kwa kutumia mamlaka yao hawafai kabisa.

Sasa inakuwaje mamlaka inamfunga Sabaya na mamlaka hiyohiyo inatoka hadharani kusema Makonda ni kijana msafi mchapa kazi ilhali dhambi za hawa vijana ziko wazi?

Yule afisa wa PCCB aliyemsafisha Makonda mchana kweupe alitumwa na nani?

Aliweka kizuizi kwetu wananchi ili tusiende kuripoti matendo maovu kwenye ofisi yake?

Basi Sabaya aachiwe tujue kuwa hii nchi dhulma na uovu si dhambi.
ALIYOYATENDA SABAYA HATA MAKONDA KAYATENDA
 
Hivi chade hawakuwa wanamuita mamvi fisadi! Mbona walimuunga mkono wakampa ugombea!.. vipi nae hafungwi..?
Huyo manvi sasa hivi yupo wapi??? Mbona alipokelewa na raisi aliyejiita mchukia rushwa????
Raisi magufuli alimpokea Lowasa kama nani?????
 
Makosa ya Sabaya ni ya uporaji na utesaji .
Yako wazi sana.

Ila Makonda makosa yake yalifichika sana na alikua anatumia zaidi vyombo husika.

Makonda alikua anajirekebisha kwa kadri siku zilivyokua zinasonga mbele.

Alikua ameanza kuwa Mstarabu kama Mrisho Gambo.
Ndio maana alitaka kuwa Mbunge ili aepukane na maagizo toka juu.

Kidogo Makonda tunaweza kumwachia Mungu tu . Lakini pia amejipoteza kwenye siasa za kistarabu katika ulimwengu wa waungwana.
Atubu na kuwaomba msamaha watanzania.
Ikiwezekana aunge mkono juhudi za kupata katiba mpya ili Mzimu wa Warioba usije ukaendelea kumwandama.

Mbowe hana hata kauli ya ugaidi.
fREeMboWe.

Kumweka Mbowe gerezani pamoja na Mhalifu Jambazi Sabaya ni kunajisi Uhuru na Utu wa mtanzania . Ni kumkejeli baba wa Taifa aliyeilea kwa uadilifu na kushirikiana na Familia ya Mbowe.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Makonda alivamia kituo cha radio/tv cha clouds. Ushahidi ni CCTV cameras. Badala ya makonda kuwajibishwa dunia ikashangaa anawajibishwa NAPE!
Magufuli alifika mbali zaidi hadi kudukua Simi za watu na alivyokuwa mpuuzi anajitaja hahdharani!
Makonda kafanya mabaya mengi zaidi ya Sabaya
 
Nakubaliana na uliemnukuu hapo.
Ishu ya Makonda na Sabaya ni tofauti halafu kumbuka hilo la kuvamia CLOUDS lilikuwa ndani ya himaya yake ya kiutawala tofsuti na Sabaya aliekuwa anavuka mipaka yake.

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom