Kumfunga Sabaya huku mamlaka zikimtetea Paul Makonda hii haikubaliki

Kumfunga Sabaya huku mamlaka zikimtetea Paul Makonda hii haikubaliki

hapo alipo Makonda moja haikai mbili haisimami,full presha yaani ……..
 
Habari,

Mimi ni miongoni mwa watu wachache tuliokuwa tukiuchukia uongozi wa Magufuli.

Matendo maovu na viburi kutoka kwa wateule wa Magufuli akiwemo Sabaya na Makonda ndivyo vilichochea zaidi kuichukia serikali ya Magufuli.

Hawa vijana waliojizolea utajiri kwa kutumia mamlaka yao hawafai kabisa.

Sasa inakuwaje mamlaka inamfunga Sabaya na mamlaka hiyohiyo inatoka hadharani kusema Makonda ni kijana msafi mchapa kazi ilhali dhambi za hawa vijana ziko wazi?

Yule afisa wa PCCB aliyemsafisha Makonda mchana kweupe alitumwa na nani?

Aliweka kizuizi kwetu wananchi ili tusiende kuripoti matendo maovu kwenye ofisi yake?

Basi Sabaya aachiwe tujue kuwa hii nchi dhulma na uovu si dhambi.
Wewe utajiletea magonjwa ya moyo kwa chuki binafsi na Makonda,wakikuambia lete ushaidi kuhusu Makonda huna,labda utaanza kusema eti alionekana Dodoma wakati Lissu akipigwa lisasi na uongo kibao,vita ya Makonda ni kuwataja wauzaji wa madawa ya kulevya akimo Mbowe basi tu,Uzuri wa Makonda ktk utawala wake wa mkuu wa mkoa, alikuwa haogopi mtu mladi uwe na kosa.
 
Jinai hiakomi,ngoja msoga line washike hatamu watamfix.
Ukiwa kijana fanya mambo kwa kuangalia na mbele yako je.
Tawala ubadilika leo musiba hawezi funua mdomo tena aliowananga ndo mabosi sasa.
 
Back
Top Bottom