Kuna watu wengi sana huomba ushauri wa kumiliki bastola.
Wakiamini usalama wao utaongezeka wakiwa na bastola.
Kama kuna huo ulazima wa kumiliki silaha unaothibitika, nashauri mamlaka irahisishe mchakato wa kuwapatia silaha wale watu wanaothibitisha wako mazingira hatarishi ya uvamizi, utaratibu wa muda kuwapatia silaha upunguzwe angalau ndani ya mwezi mmoja au wiki moja mtu mwenye ulazima sana apewe kibali cha kumiliki silaha kutokana na udharula wa mazingira aliyopo! (Apewe hata kibali cha dharula/temporary)
Lakini nje ya hapo silaha ni HATARI NA NI MZIGO MKUBWA SANA kuwa nao!
Ukweli ni kwamba bastola haiongezi usalama wowote bali inaongeza hatari ya usalama wako.
Kumiliki silaha ni mzigo mkubwa sana tena sana!
Bora umiliki Rungu kuliko bastola!
Halafu Ukiwa huna silaha mwili huwa una nguvu zaidi kuliko ukiwa na silaha! (Walegevu hubeba silaha, walio shupavu hupata silaha katika uwanja wa vita)
Mfano!
Tundu lissu angekuwa na silaha siku ile uwezekano wa kufa ungekuwa mkubwa zaidi, maana angepata ujasiri wa kutoka kujibu mapigo jambo ambalo lingerahisisha yeye kupigwa zaidi (Na ingesomeka ni mapigano)
Kukosa kwake Silaha kulimpa akili ya kumtegemea Mungu zaidi na kujificha.
Kumiliki silaha ni sawa na kibubu cha hela chumbani ambacho muda wote roho inakereketa kutamani kukipasua hata ukisikia muuza mayai anapita nje!
Ndiyo maana asilimia kubwa ya watu wanaomiliki silaha huishia kujimaliza wenyewe, wenza au watoto wao kwa jambo dogo tu.
Sababu kubwa ni kwamba silaha inapumbaza akili kwa kuifanya uiwaze muda wote.
Uzuri wa silaha ni jeshini ambako huko silaha ni kitendea kazi namba moja! Kama una silaha ni bora kuikabidhi jeshini vinginevyo ni suala la muda tu siku utajua haujui.

- Ukiwa na silaha lazima uzingatie mavazi
- Ukiwa na silaha muda wote kuificha (Ilinde ikulinde)
- Ukiwa na silaha muda wote kuilinda ili adui asikupokonye
- Ukiwa na silaha ni rahisi kujishtukia kwamba huenda kuna majambazi wanajua unayo hivyo watakuja kuipora ili wakaitumie kufanya uhalifu (ili waichukue lazima wakuue kwanza)
- Kumiliki silaha ukipoteza au kuisahau mahali unawajibishwa kwa kosa la kutokuitunza silaha (kosa kisheria)
- Ukiwa na silaha ni rahisi kuitumia ili kuwatisha watu (kosa). Bastola inatakiwa ukiitoa unapiga unless kimbia hapo
- Ukiwa na silaha hutakubali kuumizwa kwa chochote hata kama ni mapenzi
- Kama unapenda michepuko ndo kabisa hufai kumiliki silaha
- Ukiwa na silaha ukiamka usingizini badala ya kuwaza sala unawaza bastola IPO haipo
- Hutakiwi kugombea usafiri ukiwa na silaha
- Ukiwa na mwenza mshenzi akijua una silaha mkigombana anaificha ili upagawe vizuri
- Malaria ikipanda kichwani kidogo tu unajimaliza
- Wanaotumia dawa za ukimwi siwashauri kabisa wawe na silaha.
- Kumiliki silaha ni zaidi ya kulinda hirizi ya mganga!