Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Silaha ni muhimu sana kwa ajili ya kujilinda. Kuna situation inakuokoa sanaHizo ni story za kusadikika,mara 2 imeniokoa njia ya bagamoyo chini ruvu saa 9 ucku...siku ingine mererani nimelala hotel ucku mkali wakavamia ila rum yangu wakashindwa mana nilitupia 2 mlangoni
Polisi wenyewe wanasilaha kila siku ila mbungi ikitokea huwa wanasikilizia kwanza mlio! HahahahKwa matukio niliyoyashuhudia kwa wamaomiliki hizo silaha , niliapa sitakuja kumiliki silaha
Zinasaidia kweli ila zinabeba uhuru na kukupa ujasiri mazingira ambayo ilitakiwa utulie
Well said.Kuna watu wengi sana huomba ushauri wa kumiliki bastola!
Wakiamini usalama wao utaongezeka wakiwa na bastola!
Kama kuna huo ulazima wa kumiliki silaha unaothibitika, nashauri mamlaka irahisishe mchakato wa kuwapatia silaha wale watu wanaothibitisha wako mazingira hatarishi yauvamizi, utaratibu wa muda kuwapatia silaha upunguzwe angalau ndani ya mwezi mmoja au wiki moja mtu mwenye ulazima sana apewe kibari cha kumiliki silaha kutokana na udharula wa mazingira aliyopo! (Apewe hata kibari cha dharula/temporary)
Lakini inje ya hapo silaha ni HATARI NA NI MZIGO MKUBWA SANA kuwa nao!
Ukweli ni kwamba bastola haiongezi usalama wowote bali inaongeza hatari ya usalama wako
Kumiliki silaha ni mzigo mkubwa sana tena sana!
Kiufupi kumiliki silaha ni mzigo mzigo mzigo mkubwa sana sishauri hata mtu atamani kumiliki silaha!
- Ukiwa na silaha lazima uzingatie mavazi
- Ukiwa na silaha muda ote kuificha ( Ilinde ikulinde)
- Ukiwa na silaha muda wote kuilinda ili adui asikupokonye
- Ukiwa na silaha ni rahisi kujishtukia kwamba huenda kuna majambazi wanajua unayo hivyo watakuja kuipora ili wakaitumie kufanya uhalifu ( ili waichukue lazima wakuue kwanza)
- Kumiliki silaha ukipoteza au kuisahau mahali unawajibishwa kwa kosa la kutokuitunza silaha (kosa kisheria)
- Ukiwa na silaha ni rahisi kuitumia ili kuwatisha watu (kosa). Bastola inatakiwa ukiitoa unapiga unless kimbia hapo
- Ukiwa na silaha hutakubali kuumizwa kwa chochote hata kama ni mapenzi
- Kama unapenda michepuko ndo kabisa hufai kumiliki silaha
- Ukiwa na silaha ukiamka usingizini badala ya kuwaza sala unawaza bastola IPO haipo
- Hutakiwi kugombea usafili ukiwa na silaha
- Ukiwa na mwenza mshenzi akijua una silaha mkigombana anaificha ili upagawe vizuri
- Malaria ikipanda kichwani kidogo tu unajimaliza
- Wanaotumia dawa za ukimwi siwashauri kabisa wawe na silaha.
- Kumiliki silaha ni zaidi ya kulinda hilizi ya mganga!
Bora umiliki Rungu kuliko bastola!
Halafu Ukiwa huna silaha mwili huwa una nguvu zaidi kuliko ukiwa na silaha! (Walegevu hubeba silaha, walio shupavu hupata silaha katika uwanja wa vita)
Mfano!
Tundu lissu angekuwa na silaha siku ile uwezekano wa kufa ungekuwa mkubwa zaidi, maana angepata ujasiri wa kutoka kujibu mapigo jambo ambalo lingerahisisha yeye kupigwa zaidi ( Na ingesomeka ni mapigano)
Kukosa kwake Silaha kulimpa akili ya kumtegemea Mungu zaidi na kujificha!
Kumiliki silaha ni sawa na kibubu cha hela chumbani ambacho muda wote roho inakereketa kutamani kukipasua hata ukisikia muuza mayai anapita inje!
Ndiyo maana asilimia kubwa ya watu wanaomiliki silaha huishia kujimaliza wenyewe, wenza au watoto wao kwa jambo dogo tu!
Sababu kubwa ni kwamba silaha inapumbaza akili kwa kuifanya uiwaze muda wote!
Uzuri wa silaha ni jeshini ambako huko silaha ni kitendea kazi namba moja!
Kama una silaha ni bora kuikabidhi jeshini vinginevyo ni suala la muda tu siku utajua haujui!
Huyu nae analipwa mshahara kwa Kodi zetu asee,!!Kwani hata hizi short gun zinazoachwa nyumbani ukiwa na akili mbovu si unaweza kumuuwa mkeo? tena hawa wanawake wa sasa waliojaliwa kuchonga mdomo?
Point kubwa hapa ni discipline tu ya mtu mwenyewe.
Wajinga kama huyu hawana sifa ya kumilikishwa fire army ni zero brain, tena hii ni silaha ya serikali siyo yake.
View attachment 2212705
Ndo uone ujinga wa silaha ulivyo, kaomnwa kitambulisho katoa silaha!Huyu nae analipwa mshahara kwa Kodi zetu asee,!!
Huo siyo ujinga wa silaha, ni akili mbovu za mtu binafsi ila ana bonus ya kuwa na silaha.Ndo uone ujinga wa silaha ulivyo, kaomnwa kitambulisho katoa silaha!
Kuna mwingine huko aliombwa kibari/leseni akatoa silaha!
Na advantage kubwa ukijurikana fulani ana moto nyumbani hakuna kima yeyote wa kuisogelea hiyo nyumba kuja kufanya uhalifu.Mkuu kila jambo linatakiwa uzoefu.
Ushauri wako una mashiko kwa baadhi ya watu lakini si kila mtu auosomaye!
Kumiliki silaha kunatakiwa uzoefu na nidhamu, pia afya ya akili.
Silaha ya moto ni kifaa kizuri sana kujilindia dhidi ya mabazazi madhulumati ya roho na mali za watu.
Binafsi nikiwa na bunduki ya aina yoyote inayofanyakazi vizuri bila mapingamizi hasa hizi Auto, siwezi kutishwa na jambazi yeyote ama vikundi vya panya road vinavyovamia makazi ya watu na kupora.
Ukivamiwa na ukatuliza akili, jambazi hata wawe kikundi unawasambaratisha bila wewe kupata madhara yoyote.
Umiliki wa bunduki hauwezi kunibadili tabia kama ulizozieleza hapo juu kwa sababu kwa sababu nina akili timamu.
Serikali iliyopita ilikuwa ya ovyo sana,inakuwaje waziri anafanyiwa kitendo kama hicho!Kwani hata hizi short gun zinazoachwa nyumbani ukiwa na akili mbovu si unaweza kumuuwa mkeo? tena hawa wanawake wa sasa waliojaliwa kuchonga mdomo?
Point kubwa hapa ni discipline tu ya mtu mwenyewe.
Wajinga kama huyu hawana sifa ya kumilikishwa fire army ni zero brain, tena hii ni silaha ya serikali siyo yake.
View attachment 2212705
Walikuwa na baraka zote kutoka kwa mungu wa Chato.Serikali iliyopita ilikuwa ya ovyo sana,inakuwaje waziri anafanyiwa kitendo kama hicho!
Ungekuwa upo jela au kaburini.Mi ningekuwa nayo aisee mpaka sasa ningekuwa nimeuwa wengi sana tena hawa wapora simu na watemi wa bar.
Huu ni ujinga wa mtu binafsi mkuu,Ndo uone ujinga wa silaha ulivyo, kaomnwa kitambulisho katoa silaha!
Kuna mwingine huko aliombwa kibari/leseni akatoa silaha!