Kumiliki bastola ni mzigo; ni salama zaidi ukiwa huna

Kumbe kabla ya kukulinda wewe inabidi uilinde yenyewe kwanza🤔


Kumbe bastola ni kama hirizi tu😅😂
 
Tatizo la wengi mnamiliki silaha halafu hamjaandaa mazingira ya kumiliki silaha.

Silaha haitunzwi chini ya mto gorodo au
droo ya kitanda.
 
Bora uajiri mlinzi mwenye silaha kuliko wewe kumiliki silaha; liability itakuwa kwa mlinzi pale mambo yatakavyokuwa ndivyo sivyo
 
Uzi haujawagusa nyie wawindaji na majangili !
Tunazungumzia silaha binafsi za kujilinda ni mzigo!
[emoji3][emoji3][emoji3] watu mna majibu ya vituko sana... Ila silaha ni muhimu pamoja na changamoto zake, vibaka kama hawa panya road akisogea unamwaga ubongo kesi hamna maana wanasumbua jamii
 
Ukimiliki pesa wanakuja wenye siraha wanakudunda..

Ili uweke balance miliki uchawi kabla hawajaja tu steringi unakuwa ushajua kuna majambazi..[emoji23]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hayo mabastola ni mimzigo sio sifa kuwa nayo kama unahitaji kumiliki uwe nayo pale unapoona upo hatarini kweli kweli unafanya biashara ya madini kama dhahabu au muda mwingi unakuwa na pesa nyingi sio milioni tano au kumi lakini vinginevyo bastola kukupeleka jela kifungo cha maisha ni sekunde,kuiacha chumbani na kukuta haipo sio kitu cha ajabu jiandae kwenda mahabusu na mwisho gereza litakuhusu,mkeo akijua unamchepuko anaweza kuvizia umelala akakuchapa risasi,mwanao au mdogo wako anaweza ichukua bila wewe kujua akaenda mchapa mtu risasi na msala ukawa kwako kwamba ni mzembe umeshindwa kuhifadhi silaha yako.Kama unampango wa kununua silaha uwatambie jamaa zako kwamba unamiliki mguu wa kuku achana nayo ni mzigo tena mzito sio kawaida na huwezi kuwa huru.
 
Hizo ni story za kusadikika,mara 2 imeniokoa njia ya bagamoyo chini ruvu saa 9 ucku...siku ingine mererani nimelala hotel ucku mkali wakavamia ila rum yangu wakashindwa mana nilitupia 2 mlangoni
 
Umesema kweli tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…