Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Pengine wanafanya hivyo wakilinda kuanguka kwasababu fedha hazieleweki huwa zinayeyuka ili kulinda hilo inawekezwa kwenye assets lakini ukiwa na roho ya paka ukaizungusha utajikuta umepata mara mbili au tatu yake kwahiyo ukiingia kwenye assets utamiliki nyingi zaidi ya za mwanzo
Lakini hii ni kafara ngumu kuliko zote kuna mawili, kuuza assets uyeyuke au uuze upate mara mbili yake
Upate mara mbili kwa bishara gani hapa Tanzania, wafanya biashara wenyewe wanapunguza mitaji yao kwa kununua aridhi tena wewe uze aridhi uweke kwenye mzunguko usio eleweka, mtu Kaanza na mtaji wa shilling 150m kwa kufungua grocery mbili jijini Dodoma by December mwaka jana stock taking yake ina muonyesha ame bakiza 90m ukimuuliza 60m zimeenda wapi anatigisha kichwa tu bila majibu.
 
Upate mara mbili kwa bishara gani hapa Tanzania, wafanya biashara wenyewe wanapunguza mitaji yao kwa kununua aridhi tena wewe uze aridhi uweke kwenye mzunguko usio eleweka, mtu Kaanza na mtaji wa shilling 150m kwa kifungua grocery mbili by December mwaka jana stock taking yake ina muonyesha ame bakiza 90m ukimuuliza 200m zimeenda wapi anatogisha kichwa tu bila majibu.
Zipo biashara kaa na watu utajua, muuza nyama anaekosa maendeleo ametaka mwenyewe
 
Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri mkubwa, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Mimi Mr Why nataka nishare experience yangu ya umiliki wa nyumba na ardhi

Nimemiliki nyumba na ardhi kwa muda mrefu lakini havikunipa fedha za kutosha

Mwanzo nilidhani kuwa na nyumba au ardhi ni utajiri lakini baada ya kumiliki mzunguko wa fedha ulikufa kabisa kwa maana kwamba baada ya kununua hizi assets fedha nyingi ziliishia kwenye ujenzi huku nyingine zikiishia kwenye ardhi nilimaliza ujenzi lakini sikubakiwa na kitu, mzunguko wa fedha ulikatika kabisa nikawa sawa na fukara

Nilijiuliza maswali mengi kwamba kabla ya kumiliki hizi assets hela ile nilikuwa nikiizungusha nikaona nimepatia maisha manake hela unaiona mkononi

Baada ya kununua assets hela ikakata fedha yote ikalala kwenye majengo na ardhi

Nilidhani majengo yangeniingizia fedha za wapangaji lakini fedha ilikua kidogo sana nikapiga hesabu ni lini majengo hayo yatanipa fedha sawa na niliyojengea nikagundua hamna kitu

Ardhi ile nikajiuliza je nikifanya kilimo itarudisha? Nikagundua hamna kitu
Nikajiuliza je nikiuza itarudisha ile fedha? Nikagundua hamna kitu
Niligundua ardhi inapanda kidogo kidogo pia nikagundua wanunuzi wa ardhi wengi wanakuwa na hela kidogo ambazo zinapelea kidogo katika zile ulizonunulia, sana sana wanalia kupunguziwa kwa mtu mwenye uhitaji wa hela ya haraka unaanguka

Nikajiuliza je nikichukulia mikopo benk italipa? Nikagundua hamna kitu fedha ambazo benk ingenipa ni sawa na lita moja ndani ya lita tano kwahiyo ni sawa na kufaidisha bank

Basi nikakwama sana kifedha ingawa watu walipokuwa wakiona assets zangu walidhani mimi ni tajiri kumbe hamna kitu

Nikachukua uamuzi mgumu sana wa kupiga bei assets zote na kutumia ile fedha katika mizunguko yangu

Ingawa niliogopa sana nikiwaza nimejiangusha lakini nilikaza roho sawa na paka

Mwisho nilipata fedha zenye thamani ya kumiliki mara mbili ya assets nilizokuwa nazo mwanzo kwasababu nilipozungusha fedha zile nilipata mara mbili ½ ni kwasababu ya kuwa na roho ya paka, ukiwa mwoga hii kafara hutaiweza

Mpaka sasa sioni kama assets inaweza kunipa hela kwa haraka wala sina mpango wa kumiliki assets kwasasa nimegundua assets zinalaza hela afadhali nimiliki hela kuliko assets kwasababu fedha nitazungusha navyotaka mimi

Nikagundua kuwa woga ni adui wa mafanikio ningekumbatia woga mpaka sasa ningekuwa na zile assets kidogo za mwanzo

Je umeshapitia hii experience yangu? Je ulichukua hatua gani
Hizo zilikuwa liabilities na siyo assets kama unavoziita
 
Zipo biashara kaa na watu utajua, muuza nyama anaekosa maendeleo ametaka mwenyewe
Bucha au nyama gani? hapa dar kama unataka kujua hamana wateja wanyama njoo mwisho wa mwezi ujionee watimishi wanavo stock maharage ya mwezi mzima nyumbani nyama inaliwa mara moja kwa wiki, bucha zinakua bzy mwisho wa mwezi wiki ya kwanza tu dagaa maharage na mboga za majani ndo mboga za watu wengi mjini
 
Kwanza binadamu unawezaje kujenga sehemu ambayo wewe sio mkaaji wa kudumu? Ikumbukwe kwamba duniani sote tunapita na hapa duniani hatujaja kujenga
Sasa unajenga ili iweje
Duniani unatakiwa kupata hela na kuzitumia kula bata!
Masuala ya kujenga niachie serikali ijenge miundombinu kwa ajili ya vizazi
Ndio maana wazungu wengi hawajihangaishi kujenga.

Wazungu wengi ulaya na Amerika wanaishi kwenye apartments.

Pia wengi wana nunua nyumba na kulipa mortgage.

Wanao jenga ni wachache sana.

Wao muda mwingi ni kufanya kazi, wakipata fedha ni kula bata na kusafiri.

Waafrika ndio wanajihangaisha kujenga wakihofia eti watoto watalala wapi.

Kwa wazungu, mtoto akishafika umri wa kujitegemea anaenda kwenye apartment yake na yeye. Akapambane kulipa bills.
 
Bucha au nyama gani? hapa dar kama unataka kujua hamana wateja wanyama njoo mwisho wa mwezi ujionee watimishi wanavo stock maharage ya mwezi mzima nyumbani nyama inaliwa mara moja kwa wiki, bucha zinakua bzy mwisho wa mwezi wiki ya kwanza tu dagaa maharage na mboga za majani ndo mboga za watu wengi mjini
Nyama ya ng'ombe, ukitaka kuona hela yake fanya vijijini, mjini watu wajanja kila kitu hawapo tayari kukupa hela yao
Kijijini nilikozaliwa wauza bucha wana nyumba za kisasa
 
Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri mkubwa, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Mimi Mr Why nataka nishare experience yangu ya umiliki wa nyumba na ardhi

Nimemiliki nyumba na ardhi kwa muda mrefu lakini havikunipa fedha za kutosha

Mwanzo nilidhani kuwa na nyumba au ardhi ni utajiri lakini baada ya kumiliki mzunguko wa fedha ulikufa kabisa kwa maana kwamba baada ya kununua hizi assets fedha nyingi ziliishia kwenye ujenzi huku nyingine zikiishia kwenye ardhi nilimaliza ujenzi lakini sikubakiwa na kitu, mzunguko wa fedha ulikatika kabisa nikawa sawa na fukara

Nilijiuliza maswali mengi kwamba kabla ya kumiliki hizi assets hela ile nilikuwa nikiizungusha nikaona nimepatia maisha manake hela unaiona mkononi

Baada ya kununua assets hela ikakata fedha yote ikalala kwenye majengo na ardhi

Nilidhani majengo yangeniingizia fedha za wapangaji lakini fedha ilikua kidogo sana nikapiga hesabu ni lini majengo hayo yatanipa fedha sawa na niliyojengea nikagundua hamna kitu

Ardhi ile nikajiuliza je nikifanya kilimo itarudisha? Nikagundua hamna kitu
Nikajiuliza je nikiuza itarudisha ile fedha? Nikagundua hamna kitu
Niligundua ardhi inapanda kidogo kidogo pia nikagundua wanunuzi wa ardhi wengi wanakuwa na hela kidogo ambazo zinapelea kidogo katika zile ulizonunulia, sana sana wanalia kupunguziwa kwa mtu mwenye uhitaji wa hela ya haraka unaanguka

Nikajiuliza je nikichukulia mikopo benk italipa? Nikagundua hamna kitu fedha ambazo benk ingenipa ni sawa na lita moja ndani ya lita tano kwahiyo ni sawa na kufaidisha bank

Basi nikakwama sana kifedha ingawa watu walipokuwa wakiona assets zangu walidhani mimi ni tajiri kumbe hamna kitu

Nikachukua uamuzi mgumu sana wa kupiga bei assets zote na kutumia ile fedha katika mizunguko yangu

Ingawa niliogopa sana nikiwaza nimejiangusha lakini nilikaza roho sawa na paka

Mwisho nilipata fedha zenye thamani ya kumiliki mara mbili ya assets nilizokuwa nazo mwanzo kwasababu nilipozungusha fedha zile nilipata mara mbili ½ ni kwasababu ya kuwa na roho ya paka, ukiwa mwoga hii kafara hutaiweza

Mpaka sasa sioni kama assets inaweza kunipa hela kwa haraka wala sina mpango wa kumiliki assets kwasasa nimegundua assets zinalaza hela afadhali nimiliki hela kuliko assets kwasababu fedha nitazungusha navyotaka mimi

Nikagundua kuwa woga ni adui wa mafanikio ningekumbatia woga mpaka sasa ningekuwa na zile assets kidogo za mwanzo

Je umeshapitia hii experience yangu? Je ulichukua hatua gani
Ni sawa. Wewe ulilazimisha kuwa mmiliki wa real estate wakati bado hujafika levels hizo. Ili uwekeze kwenye real estate bila stress, ni lazima uwe na mzunguko mkubwa, na sio uwe mtu wa 'hand to mouth', hapo lazima ulie. Ni muhimu kujitambua level uliyopo ili ufanye maamuzi sahihi ya uwekezaji unaotaka kufanya na kwa kiasi gani.
Kwa ulivyoelezea bado upo kwenye hatua za hand to mouth, uweke hela hapa, izunguke siku moja, mbili, tatu itoke upate faida, ule faida, nyingine irudi kwenye mzunguko.
 
Mimi nina ombi Mr Why
Kwanini usitoe uzi wa biashara ulioifanya kuzungusha pesa baada ya kuuza asset zote? Nadhani kuna mengi ya kujifunza hapo^
Haina kufichaficha nilitumbukia biashara kachumbari kununua miti kuchana na kuuza, butchery, spea, pombe, cigarettes na takataka nyingine
Maisha nikuunga unga usifanye biashara moja changanya
Hakuna biashara moja itayokupa fedha nyingi ukitaka nyingi fanya bishara nyingi tofauti
 
Niligundua ardhi inapanda kidogo kidogo pia nikagundua wanunuzi wa ardhi wengi wanakuwa na hela kidogo ambazo zinapelea kidogo katika zile ulizonunulia, sana sana wanalia kupunguziwa kwa mtu mwenye uhitaji wa hela ya haraka unaanguka
Nahisi ukijua kufanya tathimini vizuri, ardhi anaweza kukulipa vizuri, sio kimiliki ardhi popote.. wengine kama real estate agent wanaangaliaga hata mipango ya serikali kuboresha eneo hilo sabab wanajua kama eneo halikuwa na maji na umeme, siku vikiwekwa thamani ya ardhi inapanda mno
 
Back
Top Bottom