Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Upate mara mbili kwa bishara gani hapa Tanzania, wafanya biashara wenyewe wanapunguza mitaji yao kwa kununua aridhi tena wewe uze aridhi uweke kwenye mzunguko usio eleweka, mtu Kaanza na mtaji wa shilling 150m kwa kufungua grocery mbili jijini Dodoma by December mwaka jana stock taking yake ina muonyesha ame bakiza 90m ukimuuliza 60m zimeenda wapi anatigisha kichwa tu bila majibu.
 
Zipo biashara kaa na watu utajua, muuza nyama anaekosa maendeleo ametaka mwenyewe
 
Hizo zilikuwa liabilities na siyo assets kama unavoziita
 
Zipo biashara kaa na watu utajua, muuza nyama anaekosa maendeleo ametaka mwenyewe
Bucha au nyama gani? hapa dar kama unataka kujua hamana wateja wanyama njoo mwisho wa mwezi ujionee watimishi wanavo stock maharage ya mwezi mzima nyumbani nyama inaliwa mara moja kwa wiki, bucha zinakua bzy mwisho wa mwezi wiki ya kwanza tu dagaa maharage na mboga za majani ndo mboga za watu wengi mjini
 
Ndio maana wazungu wengi hawajihangaishi kujenga.

Wazungu wengi ulaya na Amerika wanaishi kwenye apartments.

Pia wengi wana nunua nyumba na kulipa mortgage.

Wanao jenga ni wachache sana.

Wao muda mwingi ni kufanya kazi, wakipata fedha ni kula bata na kusafiri.

Waafrika ndio wanajihangaisha kujenga wakihofia eti watoto watalala wapi.

Kwa wazungu, mtoto akishafika umri wa kujitegemea anaenda kwenye apartment yake na yeye. Akapambane kulipa bills.
 
Nyama ya ng'ombe, ukitaka kuona hela yake fanya vijijini, mjini watu wajanja kila kitu hawapo tayari kukupa hela yao
Kijijini nilikozaliwa wauza bucha wana nyumba za kisasa
 
Ni sawa. Wewe ulilazimisha kuwa mmiliki wa real estate wakati bado hujafika levels hizo. Ili uwekeze kwenye real estate bila stress, ni lazima uwe na mzunguko mkubwa, na sio uwe mtu wa 'hand to mouth', hapo lazima ulie. Ni muhimu kujitambua level uliyopo ili ufanye maamuzi sahihi ya uwekezaji unaotaka kufanya na kwa kiasi gani.
Kwa ulivyoelezea bado upo kwenye hatua za hand to mouth, uweke hela hapa, izunguke siku moja, mbili, tatu itoke upate faida, ule faida, nyingine irudi kwenye mzunguko.
 
Mimi nina ombi Mr Why
Kwanini usitoe uzi wa biashara ulioifanya kuzungusha pesa baada ya kuuza asset zote? Nadhani kuna mengi ya kujifunza hapo^
Haina kufichaficha nilitumbukia biashara kachumbari kununua miti kuchana na kuuza, butchery, spea, pombe, cigarettes na takataka nyingine
Maisha nikuunga unga usifanye biashara moja changanya
Hakuna biashara moja itayokupa fedha nyingi ukitaka nyingi fanya bishara nyingi tofauti
 
Niligundua ardhi inapanda kidogo kidogo pia nikagundua wanunuzi wa ardhi wengi wanakuwa na hela kidogo ambazo zinapelea kidogo katika zile ulizonunulia, sana sana wanalia kupunguziwa kwa mtu mwenye uhitaji wa hela ya haraka unaanguka
Nahisi ukijua kufanya tathimini vizuri, ardhi anaweza kukulipa vizuri, sio kimiliki ardhi popote.. wengine kama real estate agent wanaangaliaga hata mipango ya serikali kuboresha eneo hilo sabab wanajua kama eneo halikuwa na maji na umeme, siku vikiwekwa thamani ya ardhi inapanda mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…