Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri bali vinalaza hela, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Utawaponza...

Binafsi natak nimiliki Ardhi kadri itakavyowezekana..

Dsm tyr nina plot mbili, Mlandizi Mbili, Arusha nipo mbioni.. Kahama, Shinyanga moja moja..

Ardhi ina raha yake sana ukimiliki... ni heshima.
 
Sitaki nishikiwe na mtu Hela yangu. Nataka niwe nayo mwenyewe, niizungushe navyojua mimi. Kila nikiihitaji niweze kuitumia kwa wakati.
💯
Ni watu tu wanachukulia poa mitandao ya simu lakini unaweza kutunza mamilioni ya hela kwenye Mobile Money sio kwenda kusumbuana na bank kila kukicha mara ufike uambiwe mtandao upo chini mara foleni mara wakupangie kiasi cha kuchukua kana kwamba unaomba
 
Utawaponza...

Binafsi natak nimiliki Ardhi kadri itakavyowezekana..

Dsm tyr nina plot mbili, Mlandizi Mbili, Arusha nipo mbioni.. Kahama, Shinyanga moja moja..

Ardhi ina raha yake sana ukimiliki... ni heshima.
Ni jambo zuri boss ina heshima yake ni nzuri sana kwa mtu mwenye utulivu/subra nikama kupanda mti uje kula matunda huko mbeleni
Kuna watu wenye kichaa cha hela kama sisi huwa tunataka hela za moto huwa tunapata sana shida kusubiri
 
Mr why ni kweli usemalo,uwekezaji wa majengo ukitegemea hela ya wapangaji,unapata hela ndogo na kwa mda mrefu sana,,lkn navyoona mimi si mbaya ukawekeza ktk hayo majengo lkn isiwe kwa asilimia kubwa, asilimia kubwa wekeza katika mzunguko mkubwa,utatoboa pia kimaisha,
Lkn pia naomba kujua ilikuwaje mtu kama Trump amepata faida kubwa kwa uwekezaji wa majengo?,je amefanyaje?,hadi kuanzisha biashara ingine tokana na hayo majengo (kama sijakosea).
Kwa Trump, it was more of a 'preparation meets opportunity' kind of thing.

Kulikuwa na Real estate booming bussiness kipindi hicho na yeye alikuwa na capital ya kuwekeza

watu wanashindwa kuelewa kuwa business model ya real estates inategemea zaidi mwenendo wa uchumi wa nchi husika

Ndo maana sasa hivi watu wamegundua "Robert kiyasoki" na kitabu chake cha rich dad poor dad ukifata alichosema mle kuanzia chapter two imekula kwako sababu kile kitabu alifocus kwenye bussiness model za 70's to 90's na sio sasa ndo maana hata yeye kafilisika mara mbili..

Real estate ni bussiness nzuri sana ila lazima iwe ni awamu ya pili ya biashara yako tafuta biashara mama kwanza biashara ya real estate inaathiriwa sana na mwenendo wa uchumi wa nchi.. marekani miaka kadhaa nyuma watu walikuwa wanalia wengine wakasanda majengo, ofcourse kwa Afrika na uchumi wetu wa kujikimu mtu hataisanda nyumba ila mazingira ya eneo ndio yatakupangia bei ya kupangisha.. ndo maana kwa Bongo jenga uza ndio bussiness model ambayo watu wanafanya kuliko kupangisha so biashara yako ya kwanza isiwe real estate maana kupata faida kwake itabidi usubiri sana anza na biashara ingine kisha ukishasimama unaingia kwenye real estate ambapo unakuwa na malengo mawili moja kwa kupangisha pili as a collateral
 
💯
Ni watu tu wanachukulia poa mitandao ya simu lakini unaweza kutunza mamilioni ya hela kwenye Mobile Money sio kwenda kusumbuana na bank kila kukicha mara ufike uambiwe mtandao upo chini mara foleni mara wakupangie kiasi cha kuchukua kana kwamba unaomba
Kabisa kaka... Ndyo mambo ambayo siyapendi hata kidogo.. Eti hela yangu mwenyewe naanza kupangiwa utaratibu wa kuipata,.. Mara kusubiri, mara hivi mara vilee
 
Kumiliki nyumba au ardhi haviwezi kukupa utajiri mkubwa, fuatana nami ujifunze experience yangu ya umiliki wa hizi mali

Mimi Mr Why nataka nishare experience yangu ya umiliki wa nyumba na ardhi

Nimemiliki nyumba na ardhi kwa muda mrefu lakini havikunipa fedha za kutosha

Mwanzo nilidhani kuwa na nyumba au ardhi ni utajiri lakini baada ya kumiliki mzunguko wa fedha ulikufa kabisa kwa maana kwamba baada ya kununua hizi assets fedha nyingi ziliishia kwenye ujenzi huku nyingine zikiishia kwenye ardhi nilimaliza ujenzi lakini sikubakiwa na kitu, mzunguko wa fedha ulikatika kabisa nikawa sawa na fukara

Nilijiuliza maswali mengi kwamba kabla ya kumiliki hizi assets hela ile nilikuwa nikiizungusha nikaona nimepatia maisha manake hela unaiona mkononi

Baada ya kununua assets hela ikakata fedha yote ikalala kwenye majengo na ardhi

Nilidhani majengo yangeniingizia fedha za wapangaji lakini fedha ilikua kidogo sana nikapiga hesabu ni lini majengo hayo yatanipa fedha sawa na niliyojengea nikagundua hamna kitu

Ardhi ile nikajiuliza je nikifanya kilimo itarudisha? Nikagundua hamna kitu
Nikajiuliza je nikiuza itarudisha ile fedha? Nikagundua hamna kitu
Niligundua ardhi inapanda kidogo kidogo pia nikagundua wanunuzi wa ardhi wengi wanakuwa na hela kidogo ambazo zinapelea kidogo katika zile ulizonunulia, sana sana wanalia kupunguziwa kwa mtu mwenye uhitaji wa hela ya haraka unaanguka

Nikajiuliza je nikichukulia mikopo benk italipa? Nikagundua hamna kitu fedha ambazo benk ingenipa ni sawa na lita moja ndani ya lita tano kwahiyo ni sawa na kufaidisha bank

Basi nikakwama sana kifedha ingawa watu walipokuwa wakiona assets zangu walidhani mimi ni tajiri kumbe hamna kitu

Nikachukua uamuzi mgumu sana wa kupiga bei assets zote na kutumia ile fedha katika mizunguko yangu

Ingawa niliogopa sana nikiwaza nimejiangusha lakini nilikaza roho sawa na paka

Mwisho nilipata fedha zenye thamani ya kumiliki mara mbili ya assets nilizokuwa nazo mwanzo kwasababu nilipozungusha fedha zile nilipata mara mbili ½ ni kwasababu ya kuwa na roho ya paka, ukiwa mwoga hii kafara hutaiweza

Mpaka sasa sioni kama assets inaweza kunipa hela kwa haraka wala sina mpango wa kumiliki assets kwasasa nimegundua assets zinalaza hela afadhali nimiliki hela kuliko assets kwasababu fedha nitazungusha navyotaka mimi

Nikagundua kuwa woga ni adui wa mafanikio ningekumbatia woga mpaka sasa ningekuwa na zile assets kidogo za mwanzo

Je umeshapitia hii experience yangu? Je ulichukua hatua gani
Hapo ndio utajua binadamu tunatofautiana pakubwa sana.
Wengine hivyo vitu vinetufanya tuone kuwa tulichelewa kuvipata.

Kwangu ardhi sintaacha kununua, nyumba sintaacha kujenga.
 
Kwa Trump, it was more of a 'preparation meets opportunity' kind of thing.

Kulikuwa na Real estate booming bussiness kipindi hicho na yeye alikuwa na capital ya kuwekeza

watu wanashindwa kuelewa kuwa business model ya real estates inategemea zaidi mwenendo wa uchumi wa nchi husika

Ndo maana sasa hivi watu wamegundua "Robert kiyasoki" na kitabu chake cha rich dad poor dad ukifata alichosema mle kuanzia chapter two imekula kwako sababu kile kitabu alifocus kwenye bussiness model za 70's to 90's na sio sasa ndo maana hata yeye kafilisika mara mbili..

Real estate ni bussiness nzuri sana ila lazima iwe ni awamu ya pili ya biashara yako tafuta biashara mama kwanza biashara ya real estate inaathiriwa sana na mwenendo wa uchumi wa nchi.. marekani miaka kadhaa nyuma watu walikuwa wanalia wengine wakasanda majengo, ofcourse kwa Afrika na uchumi wetu wa kujikimu mtu hataisanda nyumba ila mazingira ya eneo ndio yatakupangia bei ya kupangisha.. ndo maana kwa Bongo jenga uza ndio bussiness model ambayo watu wanafanya kuliko kupangisha so biashara yako ya kwanza isiwe real estate maana kupata faida kwake itabidi usubiri sana anza na biashara ingine kisha ukishasimama unaingia kwenye real estate ambapo unakuwa na malengo mawili moja kwa kupangisha pili as a collateral
💯
 
Hapo ndio utajua binadamu tunatofautiana pakubwa sana.
Wengine hivyo vitu vinetufanya tuone kuwa tulichelewa kuvipata.

Kwangu ardhi sintaacha kununua, nyumba sintaacha kujenga.
💯
Binafsi mm ni wale watu wenye kichaa cha hela hela ya moto kabla haijapoa ndiyo maana napata tabu kusubiri ninyi mnaweza ndugu zangu na mnatoboa
 
Funzo nzuri sana hili. Thanks Mkuu. Mimi ndiyo maana hata vikundi vya vikoba huwa sichezi. Pesa napenda niwe nayo mkononi mwenyewe, niipangilie na kuizungusha mwenyewe.
Kama mimI, sijui ni ubinafsi au ni nini, lakini sijawahi kucheza hiyo michezo, wala kuwa kwenye vikundi coz najiona nakua mtumwa
Mimi mzigo nikitaka ku save naweka UTT, au nanunua asset kama ardhi n.k
 
Kuna mzee alinunua kiwanja 600,000 huko Daslamu nasikia alikiuza 370m+ sijui nilitaka kusema nini🐼
Ataje na time range kati ya mwaka alionunua hiko kiwanja mpaka mwaka anakuja kuuza
 
Utawaponza...

Binafsi natak nimiliki Ardhi kadri itakavyowezekana..

Dsm tyr nina plot mbili, Mlandizi Mbili, Arusha nipo mbioni.. Kahama, Shinyanga moja moja..

Ardhi ina raha yake sana ukimiliki... ni heshima.
Mkuu zingatia sana plot zako ziwe zina documents muhimu, Hati ya wizarani ndo kila kitu,
Hizi mambo kuandikishana kwa mwenyekiti zinatia mashaka sana, mimi nikiwa sina hati ya wizarani naona bado sijamiliki
 
Kwenye biashara ya majengo jambo muhimu zaidi ni kufahamu uchumi wa sehemu husika, hii itakusaidia kujua unatakiwa ujenge jengo lenye thamani gani

Hata jenga uza usipozingatia location inakula kwako. Mfano unaenda chamazi, kibulugwa, kongowe, kimbiji, mwasonga, mapinga ama chanika unajenga nyumba ya mil 200, ukitaka kuiuza ama kuipangisha itakupa stress

Kuna jamaa anafanya kazi posta alikuwa kapanga sinza, akaona kodi iko juu akanunua kiwanja mapinga na kujenga nyumba ya maana kwa ajili ya makazi. Akajikuta bill ya mafuta ni kubwa kuliko kodi aliyokuwa analipa sinza, hivyo akaamua kurudi sinza. Ile nyumba alikosa mpangaji hata wa laki 2 mwisho akaamua kumpa mtu aishi bure ili ailinde.
 
Nna kisoma story kama hz, hu

Nikisoma story kama hz, huwa naziona za kufikirika tu, kwanza hazina ualisia, maana wasimuliaji hawajiweki wazi,
Pili kuna matajiri wakubwa, walionufaika na , nyumba na ardhi,Donald Trump, William Ruto, unawezaje kusema ardhi sio investment, wakati akili kubwa zimewekeza huko?
Kuna familia za mkubwa mmoja, kule dar, zina miriki majumba, apartment za kifahari kibao, na hayo majumba, yamepangishwa kwa taasisi kubwa kubwa tu, balozi, UN,
Niki Jenga nyumba Leo kwa 100M, nikaipangisha kwa millions 6 kwa mwaka,itachukua miaka kama 20 kurudisha pesa, kwa, mie dingi wa miaka 37! May be nitakufa kabla pesa hazijarudi! Lakini kwa binti yangu wa miaka 12,huu mjengo kwake ni faidi kwa 100%
Well said Mkuu
Najiuliza hiyo biashara ambayo unazungusha unapata faida ambayo ni mara mbili ya mtaji sipati jibu.

Kila biashara na tija na changamoto zake:
Ardhi!
Tija ya Ardhi inategemea na factor kuu tatu, location kwa maana market value ya eneo (Kata), location kwa maana ya mtaa ardhi ilipo na locality kwa maana sehemu gani ya mtaa (je ni beach plot! corner plot! au kinagusa barabara kuu maarufu). Ukifanya maamuzi sahihi kuhusu hili umetoboa. Kibiashara, villa ya vyumba 4 iliyopo Beach Masaki/Oysterbay ina thanani kubwa mara 50 zaidi kuliko kipato cha nyumba ya aina hiyo iliyopo bunju/kimara. ujanja upo katika kununua kiwanja na siyo kujenga. Hivyo hata ujenge jengo zuri kiasi gani kama ulikosea kununua kiwanja imekula kwako. Ndio maana Ubungo plaza, Dege Beach NSSF na Kijichi NSSF projects zimekuwa feilure kubwa kibiashara. Changamoto ya ya investment kwenye ardhi ni initial investment cost ni kubwa na return ni 10 -20 yrs. tija yake ni kuwa baada ya 10-20 ambapo mwenye nyumba huwa anaonekana kula super normal profit with minimum risk and management cost.

Biashara nyinginezo!
Biashara za kuzungusha zina faida na hasara katika muda mfupi. Uzuri wa biashara ya kuzungusha unaweza kuanza na na mtaji mdogo baadaye ukapanda na kuwa mkubwa ndani ya miaka michache (initial investment cost siyo lazima iwe kubwa). Changamoto zake ni pamoja na risk inakuwa kubwa kwa kadiri unavyofanya biashara yenye super normal profit, competition inaibuka na kuua profit kila unapopata mafanikio hivyo mafanikio always ni ya muda mfupi. Hivyo suala la kupata na kukosa vina uzito unaofanana. Ili ufanikiwe kwenye biashara ni sharti kufanya maamuzi sahihi katika wakati sahihi na utekeleze mipango kwa usahihi. Kwenye maamuzi na mipango ndipo panaposababisha faida au hasara, na ndipo panapofanya baadhi wafanikiwe na wengine washindwe. Biashara pekee ambazo zina faida kubwa sawa au zaidi ya mtaji uliowekeza ni illigal business mifano kutoa rushwa ili upewe sehemu nono ya mgodi ambapo inabidi uwadhurumu wananchi na serikali, dawa za kulevya n.k

Hivyo inaweza isiwe sahihi kusema kwa ujumla kuwa biashara ya kuzungusha ni rahisi au inalipa zaidi kuliko kuwekeza kwenye ardhi. Maamuzi na mipango ndio siri ya kutoboa! hivyo tufanye utafiti kabla ya maamuzi ili tufanikiwe.

Mungu atusaidie
 
Kwenye biashara ya majengo jambo muhimu zaidi ni kufahamu uchumi wa sehemu husika, hii itakusaidia kujua unatakiwa ujenge jengo lenye thamani gani

Hata jenga uza usipozingatia location inakula kwako. Mfano unaenda chamazi, kibulugwa, kongowe, kimbiji, mwasonga, mapinga ama chanika unajenga nyumba ya mil 200, ukitaka kuiuza ama kuipangisha itakupa stress

Kuna jamaa anafanya kazi posta alikuwa kapanga sinza, akaona kodi iko juu akanunua kiwanja mapinga na kujenga nyumba ya maana kwa ajili ya makazi. Akajikuta bill ya mafuta ni kubwa kuliko kodi aliyokuwa analipa sinza, hivyo akaamua kurudi sinza. Ile nyumba alikosa mpangaji hata wa laki 2 mwisho akaamua kumpa mtu aishi bure ili ailinde.
Well said mkuu
 
Nahisi ukijua kufanya tathimini vizuri, ardhi anaweza kukulipa vizuri, sio kimiliki ardhi popote.. wengine kama real estate agent wanaangaliaga hata mipango ya serikali kuboresha eneo hilo sabab wanajua kama eneo halikuwa na maji na umeme, siku vikiwekwa thamani ya ardhi inapanda mno
Ni kweli kabisa Mkuu. Mfano ni Dodoma, sasa hivi viwanja vya mjini kati havikamatiki. Hata fremu za biashara ni bei mbaya sana. Uchaguzi wa sehemu ya kuwekeza kwenye masuala ya ardhi ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom