Kumkaribisha Haji Manara Jangwani Ni Kosa Kubwa Sana!

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Wanajanvi.

Sina shaka na uwezo wa Haji kwenye matumizi ya kimkakati ya Kimasoko. Ila kwa kutumia jicho la tatu ninaona kama ni kosa kubwa sana kumkaribisha huyu Mwamba pale Jangwani kwa sababu ya historia yake kwenye eneo la nidhamu na weledi.

Ni kweli kuwa ametokea kwenye familia yenye vina saba na Yanga SC lakini kwa bahati mbaya amekwisha chafuka akiwa Simba SC kwa tabia zake za kinidhamu ambazo kila mwanasoka amepata kuzishuhudia.

Sijatambua ni nini klabu kama klabu imepanga kunufaika na huyu mwamba ikiwa klabu iko kwenye safari ya kuwa klabu yenye kuendeshwa kwa ueledi mkubwa.

wengi tunafurahi leo kwa kuwa inaonekana kama tumewashinda wapinzani katika hili, (Ni kweli kwasababu alikuwa mtu muhimu sana kiuhamasishaji katika klabu yao) lakini sioni jambo chanya la kiutofauti sana ambalo atalileta Jangwani zaidi ya maneno ya Taarab ambayo tulikwisha amua kujitenga nayo tangu tulipo mfukuza Jerry Muro.
 
Unajua binadam sisi kila mmoja kazaliwa na kitu chake na nguvu fulani iliyo ndani mwake.

Tunatofautiana kuitumia.

Haji Manara, haraharaka ukimchek sio kitu ILA JAMAA ANA NGUVU KUBWA SANA , NGUVU YA KIUONGOZI NDANI YAKE, JAMAA ANA MAMLAKA.

nandicho kinamuweka mjini, Sisi tunapiga kelele, hafai hafai, ila ndio ivo imeshakua !!!.

Usishangae siku akatoka Yanga, akaenda Azam na BADO AKAKUBALIKA.
 
Umeongea vyema sana mkuu.

Ila naamini pia haji atakua amejifunza kwa namna moja ama nyingine.

Acha tuone mkuu,ila kikubwa tumpe ushirikiano wote na mapenzi yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Sawa ulichokisema! Hofu yangu kubwa ilikuwa ni weledi wake tu. Unajua huku sisi hatujazoea "UHUNI"
 
Kwa kilichotokea na kwa umri wake lazima kuna namna amejifunza kuna vitu atarekebisha na pia lazima kuna mazungumzo mengi sana yamefanyika kabla ya kufikia hapa
 
Tutumaini kuwa iko hivyo! Itapendeza zaidi.
 
Unajua binadam sisi kila mmoja kazaliwa na kitu chake na nguvu fulani iliyo ndani mwake.

Tunatofautiana kuitumia.

Haji Manara, haraharaka ukimchek sio kitu ILA JAMAA ANA NGUVU KUBWA SANA , NGUVU YA KIUONGOZI NDANI YAKE, JAMAA ANA MAMLAKA.

nandicho kinamuweka mjini, Sisi tunapiga kelele, hafai hafai, ila ndio ivo imeshakua !!!.

Usishangae siku akatoka Yanga, akaenda Azam na BADO AKAKUBALIKA.
Haji Manara ana Power kubwa katika soka letu, kinywa chake ni dhahabu naanza kuamini alikuwa anafanya wachezaji wa simba wapate nguvu ya kujituma uwanjani, spirit aliyonayo katika kuzungumza ni ya kiwango kikubwa sana

Acha aendelee kupata Mkate wake
 
Sina shaka na uwezo wake katika eneo lake. Lakini kitendo cha kuvuka mipaka ni jambo ambalo linatupatia hofu baadhi ya mashabiki wa Yanga SC.
 
Sisi Yanga Tumempokea Vema
Hatafanya Kama Simba Ila Atakuwa Na Nidhamu Kubwa
 
Back
Top Bottom